Nataka kuchangia kidogo kuhusiana na hii baishara ya mchele niliyowahi kufanya kipindi cha 2017&2018..
Kwanza kabla ya kufata mzigo hakikisha kuwa una mtaji wa kutosha,soko lako lipoje na umewalenga wateja wa sampuli gani.baada ya kuyafahamu hayo ndo unaanza kuingia kwenye biashara yenyewe.
Pili, baada ya kufanya maamuzi ya kufanya hiyo biashara,nakushauri ufate mzigo wewe mwenyewe na usimuagizie mtu kuna upigaji lakini unaweza ukapoteza msingi kwa yule aliyekuagizia kukimbia na mtaji wako.
Nadhani kuna baadhi ya wachangia wameeleza vizuri kuhusu hiyo biashara,lakini na mimi naomba nielezee uzoefu na changamoto za biashara hii...kuna aina mbili za kuweza kupata mchele, njia ya kwanza kwa mfano muda huu maeneo ya ifakara,kilombero wapo kwenye mavuno kwahiyo unaweza kwenda mashambani kwa ajili ya KULENGA MPUNGA(kufikicha mpunga kwa kutumia mikono)..maana yake unakwenda kununua mpunga moja kwa moja toka kwa wakulima,kipindi nafanya hii biashara tulikuwa tunanunua gunia la debe kumi kwa shilingi 80000 lakini pia inategemea na msimu ukiwa mzuri kwa maana ya maeneo mengine mpunga umepatikana kwa wingi bei ya debe la mpunga hushuka..
Hii njia ni nzuri lakini inachangamoto zake kwa maana ili uweze kuyafanya hayo yote lazima uwe na mwenyeji wa kuweza kuku link na wakulima, kumpoza mwenyeji lakini pia hii njia hutumia mikono kwa ajili ya kufikichia mpunga ili uweze kujua mpunga huu nikiupeleka mashineni unaweza kutoka vizuri/vibaya..unaweza ukakuta umeufikicha mpunga na kutoka vizuri lakini ukija kukoboa mchele hutoka vibaya mwishowe usipate ulichokitarajia kupata/ukapata kwa % ndogo.
Njia hii inachangamoto nyingi nimefupisha ziwezi kuzitaja zote,maana kuna usafiri kutoka shambani,viroba,kamba, wabebaji, turubui la kuanikia mpunga n.k
Kuna njia nyingine ambayo ni nzuri kwa sababu inaokoa muda na kufanya biashara kuwa rahisi kabisa.. KUKINGA MPUNGA.njia hii mnunuzi utembelea mashine kwa ajili kutafuta mchele uliokobolewa kutoka kwa madalali au wakulima wanaotaka kuuza mchele huo. Hapa kuna makubaliano baina ya mnunuzi na mkulima/dalali baada ya kukobolewa hapo mashineni,inategemea na aina ya mchele, kuna super,middle na mavulavula kipindi nanua mie supa ilikuwa inauzwa 1400-1300 kwa kilo, middle 1100-1250,na vula vula 1000 kwa kilo ila hapa inategemea na bargaining power yako.
Njia hii changamoto zake ni chache,mfano kuzungukia mashine zote za eneo husika(Muda) kwa ajili ya kupata mchele mzuri,lakini pia pindi utakaponunua mzigo kwenye mashine tofauti kuna gharama za kubeba aidha kwa piki piki au baiskeli ama mkokoteni,lakini usiweze pia kupata mzigo kwa wakati inategemea na unataka mzigo kiasi gani, lakini pia kuna kuangaliana usoni sana haswa kwa watu wanaotoka maeneo ya kilombero,ifakara,mgeta ,mlimba,kuna siku nilikinga mchele na kufikiana muafaka na muuzaji/mkulima lakini kutokana na kuwa mgeni yule mwenye mashine aliweza kuupata ule mzigo malikauli lakini mimi mwenye cash niliishia kutumbua macho na kushikwa na butwaa hiyo ilikuwa maeneo ya kijiji cha Mwaya-Mang'ula na changamoto zingine ni ndogo ndogo,mfano malazi,chakula
Baada ya kupata huo mchele kuna vitu vifuatavyo vinahitajika...Viroba kuhifadhia mchele kiroba =shs700/800,Mafuta kwa ajili kung'arishia mchele wako,mimi nilikuwa natumia mawese na mafuta ya kula ya kawaida nilikuwa natumia Chupa mbili kwa mafuta ya kawaida na mawese nusu chupa kwa tani 1(kg1000),kamba, ushuru wa mazao 30 kwa kilo(3000/kg100) usafiri shs 70 kwa kilo(7000/kg100) wabebaji shs 500/kg 100 kama utahitaji kugrade mchele pamoja na kupaka mafuta tulikuwa tunachajiwa shs 20/kg1 (2000/kg100) nahisi ni hivyo
Nilichogundua kwa walaji wa Dar wanapenda sana kununua michele iliyonyooka ikiwa inang'aa kwa hiyo hakikisha unalifikia soko lako vizuri kwa kuangalia mahitaji ya wateja wako. Naendelea kukushauri kuwa makini unapotaka kununua mchele kutoka kwa wakulima/madalali hakikisha mchele unaonunua ni mzuri maana hata ukitaka kuja ku ugrade unakuwa hupati chenga nyingi,jitahidi kununua mchele ulio supper na middle ambao hutokana na mbegu ndefu kama mfano mbawa mbili,sengo ila inategema unapochiukulia mchele wako ili upate kitu kizuri.
Biashara haina hasara lakini pia haina faida kivile maana wengi wetu tunafikra za kupata kwa kufanya tu kitu kwa mara moja.....Nakushauri ndugu,kwenye biashara walenge mama ntile, shule za nasari, wenye maduka madogo madogo lakini pia kama Una store jaribu kushusha bei kw a wateja wanaoanza kununua kuanzia kg 10 ,itakusaidia ku retain wateja wako na kutengeneza network kwa wateja wengine ..mfano mchele ulikuwa unauza 1700 unaweza kufanya discount ya shs 50 kwa kila kilo ili kumvutia mteja wako.