Mambo yangekua marahisi hivyo ungeshakua milionea wewe mwenyewe,
@Mleta mada,za kuambiwa changanya na zako..
Mchele unatofautiana kuanzia mbegu,upandaji,eneo unapoulima na ardhi husika...
UFAFANUZI:Ref Magugu,Babati
Kuna aina nyingi
Super Kyela:Mzito kwenye mpunga na ukikobolewa,punje ndefu,harufu nzuri,huangalizi maradufu,kipato kizuri
Super Kula na Bwana:Mrefu,harufu,huota muda mfupi,hupungua kidogo @2kg kwenye kila kilo 80 zilizokobolewa
Super Mkomboz:Mzuri,sio mrefu sana kipato kidogo,harufu nzuri sana,haivumilii ukame wala furiko,bua zake nyepesi
Saro:Hizi unatupia ukipanda(yaani ndo kitalu na ndo jaruba),mfupi,hauna harufu,una kipato kwa maana ya uzalishaji,na bei yake ni chini(ndo huo wa 1000/kg alafu mkaupake mafuta(non sense kwa mfanyabiashara serious na anaefanya biashara endelevu).
Super kawaida :Huu ndo wengi tuna ula tukituma wasichana madukani.
Harufu wanayo ongelea sijui ya mafuta,utapaka tani 100?,hiyo harufu si ni ya mchele mzuri ndo mana huo unaopakwa wana "FAKE" ili ufananie na kunukia huo mzuri?
Nasisitiza:
Mchele unatofautiana na upo wenye harufu nzuri naturally