Dar ukitaka chumba hata kesho unakipata. Hela yako tu, siyo kama unaenda Europe au US.
Madalali kibao wapo Dar, kama una hela kidogo hukosi sehemu ya kukaa kwa miezi angalau 6, na sehemu za kula bei rahisi zipo kibao.
Kwa ufupi, mimi najua Dar es salaam ni mji rahisi sana kuhamia tena sana. Mimi mungu kanipa bahati ya kuishi miji mingi mikubwa tena peke yangu nikiwa sina kitu na kupata tabu hadi kujiweka sawa. Kwa hiyo najua kabisa Dar es salaam ni mji mwepesi sana hasa kwa kijana asiyetaka makuu na mwenye nia ya kujitafuta.
Nakushauri timiza ndoto zako kwa sababu maisha ni yako na yanaenda kasi sana utakuwa mtu mzima muda si mrefu na utaanza kuitwa uncle. Tembelea Dar kwanza uchukue chumba cha bei rahisi uanze kuangalia wapi utafanya biashara yako na uanze taratibu huna haja ya kuchukua Fuso zima unaweza ukafanywa kitu kibaya.
Mimi nakushauri uondoke hapo kijijini kwa sababu tayari hupapendi na huna haja ya kupapenda, siyo lazima utimize ndoto za Baba yako, muombe radhi na mwambie mimi kuna kitu kinaniambia niende dar, nikishindwa nitarudi home usijali.