Nje ya mada: kwa wale walioko katika lane ya kutafuta ajira, hakiki mara tatu tatu referee unaemuandika. Budda kama unasoma hapa nisamehe;
Kuna jamaa mmoja ameomba kazi shirika la watu wa nchi flani. Sasa interview process ikaenda kama miezi 3. Baadae akaja kupewa feedback amekosa wameamua kuproceed na a better option. Sasa akapata courage ya kuuliza kwanini ili ajirekebishe labda. Akajibiwa, shida imekuja kwenye recommendation letters. Mbili kati ya tatu zimempondea. Lakin kwa madai yake ni watu ambao alikua na ujamaa nao mzuri tu. Na aliwapa taarifa kuwa watatafutwa wakamwambia hata usijali, ondoa shaka!! Lakin ndo akatumiwa barua na yule HR, waliyokuwa wameyaandika ni disaster. Akasema acha aprove tena, akampanga mtu kwamba ajifanye recruiter, apige simu kwa mmoja wa hao referee. Akapondwa vibaya mno. Sisemi hakuwa at fault, nasema mjue referee wako vizuri....ni hilo tu!!!