Jamaa hayuko serious! Anataka ushauri kutoka kwa wana Jf kwa kosa la kuisaidia CCM?!!Kesi ya nyani umeileta kwa mkulima!
Acha nijiandae kusoma komenti watakutia hasira huku hadi ujikute unajuta kuandika uzi wako.
Yaani Dogo lazima apokee vitasa kwa wanaJF kwa sababu ya neno CCM.Jamaa hayuko serious! Anataka ushauri kutoka kwa wana Jf kwa kosa la kuisaidia CCM?!!
Kitakacho fuata hapo ni baba na mwanae watakuja kugombania nyumba ya babu, kisha atakuja kuomba tena ushauri kwasababu babu alisha sema asije aka nyanyasikaBaba anaishi kwa babu, duuuu bora ulivyonyamaza Ushi
Yaani Dogo lazima apokee vitasa kwa wanaJF kwa sababu ya neno CCM.
Ila ingekuwa ni story ambayo haihusiani na Ccm angepata japo ushauri kidogo.
Hapana mkuu hapo nyumbani kuna chumba ambacho mzee amekifunga na kufuli na kunitolea vitu nje, ananitukana eti bora apangishe hapate kodi kuliko mimi kukaa na kujaza choo
Habarini ndugu zangu wana JamiiForums, matumaini yangu mu wazima wa afya tele.
Nisiwachoshe niende kwenye mada moja kwa moja
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28, nimemaliza chuo kikuu mwaka jana
Tangu nimemaliza chuo, nimehangaika sana kupata kazi bila mafanikio.
Mwaka huu mwezi uliopita nilibahatika kupata kazi ya kuandikisha wapiga kura kwenye uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa.
Baba yangu alikataa kabisa nisijihusishe kwenye mambo yoyote yanayohusiana na siasa kwa hiyo hakupendezwa.
Baada ya hilo zoezi la uandikishaji kuisha, juzi Ijumaa kuna mjumbe wa chama cha mapinduzi (CCM) aliniambia kuwa nimtafutie wanachama 20 tu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, na kuahidi atanipa pesa ya maji.
Pale home jumla tupo watu 7 pamoja na ndugu wengine, nilitaka kwanza kuanza na familia yangu, nilimfuata baba yangu na kumueleza kuwa na yeye awe mmoja wapo katika watu 20 nilioombwa na mjumbe
Ndugu zangu baba alinitukana matusi mazito, siwezi kuyaandika hapa, mpaka kufikia kuniambia nitakuwa nimelaaniwa na dunia.
Kaenda mbali zaidi ananimbia kama ntashilikiana na watu wa CCM na kumhusisha yeye, ataniondoa kwenye nyumba tunayoishi, ukizingatia hiyo nyumba ni ya babu yangu ambaye yeye ni baba yake.
Marehemu babu yangu kabla ya kufariki alisema kabisa na wazi kuwa nisinyanyasike kwenye ule mji.
Wakuu mpaka ninapoandika hapa, baba atoa vitu vyangu nje, anasema nikahamie kwa huyo mjumbe.
Naombeni ushauri wenu wakuu, nataka kuipigania haki yangu, maana babu alisema kile chumba nilichokuwa nakaa ni mali yangu halali.
Nipo katika wakati mkuu, nisaidieni niende polisi au nifanye nini wakuu?
Asanteni.
Huyo Mzee wako kakuchoka tu likely utakuwa kula kulala hayo mambo ya siasa kaona ndo nitoke vipi!
Toka kapigane wapo wengi tu walioletewa hila na wazee wao na leo wana maisha yao.
Kikubwa ukitusua halafu akaja kujilizaliza mfungie vioo liwe fundisho kwa wazee wengine wasiojielewa.
Mtu upo uzeeni halafu una-entertain mifarakano kwa watakaokulea muda si mrefu.
Hapana mkuu hapo nyumbani kuna chumba ambacho mzee amekifunga na kufuli na kunitolea vitu nje, ananitukana eti bora apangishe hapate kodi kuliko mimi kukaa na kujaza choo
Mtu ana miaka 28 eti analialia kafukuzwa nyumbani,mitoto mingine haina faida kabisa bora kufuga bata.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Kwahiyo anataka baba yake afungwe ili apate urithi.Tatizo lake alikuwa anataka sympathy kwa wadau
Ukiangalia mwanzo amesema kuwa “Baba yake alikataa kabisa ajihusishe na mambo ya siasa”
Hayo ni maneno ya baba yake kuwa hapendi siasa na wapo wengi hawapendi siasa kwa ujumla
Ila yeye ameona amtafutie kesi baba yake na kupata sapoti
Hapo amepiga mahesabu kuwa baba atafungwa na yeye atarithi nyumba [emoji23][emoji23]
Kuna watu wanapenda mirathi mpaka wanaweza kuuwa
Ishi na familia yako kwa upendo ili siku moja usije tia aibu au kulia lia kama baba yake na Diamond.