Msaada wenu: Baba yangu mzazi anataka kunitimua kwenye nyumba ya babu yetu

Msaada wenu: Baba yangu mzazi anataka kunitimua kwenye nyumba ya babu yetu

Pole sana ndugu yangu, jaribu kuongeana baba yako vizuri na kumuomba msamaha, ila ukiwa umebadili mawazo ya ulichokuwa unataka kukifanya.
 
Nilimsikia Mwalimu Nyerere akiwasimulia Wabunge Wa CCM walipokaa kama kamati ya CHAMA CHA MAPINDUZI pale Karimjee Hall.

Wakati huo kulikuwa na mvutano Wa kidini juu ya bucha za nguruwe , hivyo miongoni mwa maswali yaliyoulizwa yy alijibu juu ya huo mvutano.

Kwanza alikataa kuwa hakuna mvutano ila kuna wahuni 2 akawataja kwa majina ( naomba nisiwataje)

Kisha akaanza kumuelezea mmoja Wa hao aliowaita wahuni. Kuwa huyu kwanza jina la baba yake analotumia sio la baba yake mzazi.

Baba yake alikuwa anaitwa Hassan alikuwa na pacha wake aliyeitwa Hussein, huyu Hassan alikuwa mwanachama Wa TANU hivyo Mwanaye alipojiingiza kwenye siasa alimkataza na kumwambia kama anataka sasa ajiunge TANU.


Lakini mwanaye akakataa, hivyo babaye akamwambia yy sio mwanaye tena kwani alijiunga na chama cha kihuni kilichoitwa UTP , ndipo mtoto alipoamua kutumia jina la pacha Wa babayake yaani HUSSEIN.

Kwahiyo jambo hilo hajianzia kwako . using'ang'anie vya babaako kwa kisingizio cha babu. Wenzio walimenyeka kumsaidia baba yao waache wafaidi usijipendekeze.
 
Yaani Dogo lazima apokee vitasa kwa wanaJF kwa sababu ya neno CCM.

Ila ingekuwa ni story ambayo haihusiani na Ccm angepata japo ushauri kidogo.

Tatizo lake alikuwa anataka sympathy kwa wadau
Ukiangalia mwanzo amesema kuwa “Baba yake alikataa kabisa ajihusishe na mambo ya siasa”
Hayo ni maneno ya baba yake kuwa hapendi siasa na wapo wengi hawapendi siasa kwa ujumla
Ila yeye ameona amtafutie kesi baba yake na kupata sapoti
Hapo amepiga mahesabu kuwa baba atafungwa na yeye atarithi nyumba [emoji23][emoji23]
Kuna watu wanapenda mirathi mpaka wanaweza kuuwa
 
Sehemu yoyote ile yenye hela wala usiachie ipite. Humu kuna watu wamepata degree na kazi kwa kuvua chupi. Hapo tengeneza urafiki na hao wanaccm kwasababu utapata kazi halafu ukizingatia umesoma. Utapewa dili. Hao wanaokutukana humu hawana msaada wowote ule kwako. Kuhusu issue ya mzee wako jaribu kama unataka kula na kipofu. Afrika hakuna demokrasia wala haki, ukijidai unapigania haki Afrika utaishia kufa. Hapo cha msingi ndugu yangu angalia pesa tu.
Hapana mkuu hapo nyumbani kuna chumba ambacho mzee amekifunga na kufuli na kunitolea vitu nje, ananitukana eti bora apangishe hapate kodi kuliko mimi kukaa na kujaza choo
 
Hivi watu mnaazaje kugombea mali za urithi,tena ambazo hamna jasho lako hata tone.
 
Baba ana haki kukufukuza mana nyumba ya baba yake mzazi sio baba yako,na pia nampongeza baba yako kwa aliyoyasema tena
Habarini ndugu zangu wana JamiiForums, matumaini yangu mu wazima wa afya tele.

Nisiwachoshe niende kwenye mada moja kwa moja

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28, nimemaliza chuo kikuu mwaka jana

Tangu nimemaliza chuo, nimehangaika sana kupata kazi bila mafanikio.

Mwaka huu mwezi uliopita nilibahatika kupata kazi ya kuandikisha wapiga kura kwenye uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa.

Baba yangu alikataa kabisa nisijihusishe kwenye mambo yoyote yanayohusiana na siasa kwa hiyo hakupendezwa.

Baada ya hilo zoezi la uandikishaji kuisha, juzi Ijumaa kuna mjumbe wa chama cha mapinduzi (CCM) aliniambia kuwa nimtafutie wanachama 20 tu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, na kuahidi atanipa pesa ya maji.

Pale home jumla tupo watu 7 pamoja na ndugu wengine, nilitaka kwanza kuanza na familia yangu, nilimfuata baba yangu na kumueleza kuwa na yeye awe mmoja wapo katika watu 20 nilioombwa na mjumbe

Ndugu zangu baba alinitukana matusi mazito, siwezi kuyaandika hapa, mpaka kufikia kuniambia nitakuwa nimelaaniwa na dunia.

Kaenda mbali zaidi ananimbia kama ntashilikiana na watu wa CCM na kumhusisha yeye, ataniondoa kwenye nyumba tunayoishi, ukizingatia hiyo nyumba ni ya babu yangu ambaye yeye ni baba yake.

Marehemu babu yangu kabla ya kufariki alisema kabisa na wazi kuwa nisinyanyasike kwenye ule mji.

Wakuu mpaka ninapoandika hapa, baba atoa vitu vyangu nje, anasema nikahamie kwa huyo mjumbe.

Naombeni ushauri wenu wakuu, nataka kuipigania haki yangu, maana babu alisema kile chumba nilichokuwa nakaa ni mali yangu halali.

Nipo katika wakati mkuu, nisaidieni niende polisi au nifanye nini wakuu?

Asanteni.
 
Mtu ana miaka 28 eti analialia kafukuzwa nyumbani,mitoto mingine haina faida kabisa bora kufuga bata.
Huyo Mzee wako kakuchoka tu likely utakuwa kula kulala hayo mambo ya siasa kaona ndo nitoke vipi!

Toka kapigane wapo wengi tu walioletewa hila na wazee wao na leo wana maisha yao.

Kikubwa ukitusua halafu akaja kujilizaliza mfungie vioo liwe fundisho kwa wazee wengine wasiojielewa.

Mtu upo uzeeni halafu una-entertain mifarakano kwa watakaokulea muda si mrefu.
 
Hapana mkuu hapo nyumbani kuna chumba ambacho mzee amekifunga na kufuli na kunitolea vitu nje, ananitukana eti bora apangishe hapate kodi kuliko mimi kukaa na kujaza choo



Huyo kweli ni baba yako mzazi au wa kufikia, nenda kapimeni DNA.🤣
 
Tatizo lake alikuwa anataka sympathy kwa wadau
Ukiangalia mwanzo amesema kuwa “Baba yake alikataa kabisa ajihusishe na mambo ya siasa”
Hayo ni maneno ya baba yake kuwa hapendi siasa na wapo wengi hawapendi siasa kwa ujumla
Ila yeye ameona amtafutie kesi baba yake na kupata sapoti
Hapo amepiga mahesabu kuwa baba atafungwa na yeye atarithi nyumba [emoji23][emoji23]
Kuna watu wanapenda mirathi mpaka wanaweza kuuwa
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Kwahiyo anataka baba yake afungwe ili apate urithi.
 
Mjmbe wa CCM anakuja kukufool mtu na degree yako? Pia, hii kauli ya nyumba ya babu yangu ooh babu alisema nisinyanyasike niachiwe kile chumba imenisikitisha sana! Man!
 
Back
Top Bottom