Msaada: Yeyote anayemjua mtaalam anayeweza kumrejesha ndugu yetu aliyefariki kifo cha kutatanisha

Kubalianeni na ukweli kuwa ndugu yenu amekufa na hatarejea. Hata akionekana bado atazua taharuki kwa Sababu mlimzika hadharani.
 
Mkuu kubali yapite mi tarehe 12/3/2023 nimempoteza mwanangu kwa mazingira tatanishi ameumwa siku 2 na kufia benjamini mkapa ila kuna viashiria vyote na wahusika kujulikana nimeshauriwa sana kulipiza ila nimekataa,acha yapite ni mapito japo picha zake kwenye simu zinaniumiza sana
 
Mkuu nimekubaliana na ndugu zangu na hazijapita siku saba....naomba msaada tafadhali.
 
jeshi la polisi, mahakama, hospital, na ofisi ya mkemia mkuu........hao ndio wataalam wanaoweza kukusaidia kwa sasa.....pole kwa msiba.
 
Pole sana Mungu akutie nguvu na akupe faraja.
 
Kifo ni kifo tu mkurugenzi. Hakuna mganga yeyote yule mwenye huo uwezo. Mtaishia tu kutapeliwa.

Ifikie wakati mkubali tu matokeo! Ingawa inauma sana kumpoteza mtu unayempenda. Msipoufuata huu ushauri wangu, basi mjiandae kuuza mashamba, nyumba, na kila kitu ili tu kumpelekea mganga.

Maana mkipeleka hiki, atawaambia mpeleke kile!! Yaani ni bandika bandua. Akili zikija kuwakaa sawa, mtajikuta hamna kitu.
 

Duh, pole sana brother
 
Pole sana mkuu
 
Poleni sana, nina elewa mnacho pitia nime fikwa na mimi jambo kama hilo na nili wahi uliza humu namna kama ina wezekana hata kuwasiliana na marehemu , nina maumivu makubwa na bado najitahidi sana kuweza kukubaliana na hii hali , ila bado sija ikubali na maumivu ni haya semeki , nampenda sana kijana wangu aliye ondoka , hata kumuita marehemu sitaki. Kama mtafanikiwa kwa hilo naomba pia uni pe taarifa ili na mimi ni jaribu bahati yangu kama ita wezekana . Kama hautajali njoo inbox tuongee zaidi , kuhusu hili suala.
 
Pole Sana mkuu.. maumivu ya kufiwa na mtu unaye mpenda hayana mfano!
Lakini kubali tu ukweli ..hakuna jinsi ...Mimi binafsi Hali hii imenichukua miaka kuikubali.. yaani nilifikia kuumwa karibia kufa!

Utasumbuka Sana .. mshukuru Mungu .tu.

Huwezi kujua Mungu amepusha nini na Ana sababu zake kunichukua kiumbe wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…