GE2025 Msafara wa mabasi ya CCM takribani 20 yatinga Chamwino kumsindikiza Rais Samia, sio kodi zetu kweli hizi?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Nimeuona msafara ambao wa mabasi takribani 20 yakimsindikiza Rais Samia akienda kuchukua fomu ya urais Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Aloooo, kweli kodi za wananchi zimewafaidisha sana hawa CCM! Naandika haya nikibubujikwa na machozi ya huzuni

Your browser is not able to display this video.
 
Hakuna kitu kibaya kama mke kujilipia mahari ili aolewe 😂 ndoa yake huwa hana furaha nayo siku zote.
 
Wenzake aliwazuia wasiende na misafara lakini
 
Haya mabasi yaliingizwa nchini kwa tiketi ya JWTZ nashangaa CCM wakajichukulia juu kwa juu
Hayo mabasi nimeona juzi asubuhi yalikuwa vurugu mechi yakiongozana uelekeo wa Morogoro yakiwa na chapa ya "Military Bus" leo hii yamevikwa sticker za kijani yakiwakilisha mbogamboga PP.
 
Hayo mabus ya Yutong F12 yalishuka bandarini 2024 yakiwa na nembo hiyohiyo ya Ccm na ya Jwtz pia yalishushwa baadae kwahiyo Ccm wanayo yao na Jwtz wanayo yao kama ni wizi basi waliiba wakaenda china kununua moja kwa moja na siyo kubadilisha rangi mabus ya jwtz

Picha ya baadhi ya mabus ya ccm yakiteremshwa bandarini
 
Hizo ni tozo za kutoka chadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…