Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Jukwa kuu wanakaa watu maalum kama Mwenyekiti Mbowe, sasa hao wote walitaka kuingia ili wakakae wapi ? Lazima itifaki izingatiwe
Je walifuata mambo ya itifaki? Maana wasifanye kama msiba wa mtu wa kawaida.
 
Raisi alikuwa hajafika walivyokataliwa

Wamefika saa tatu tena na msafara wa magari yao wakati wanajua fika utaratibu ulikuwa ni kuanzia Karimjeee mnaletwa na magari hadi taifa ..., ukumsikia Dr Abbasi?

Kwani mlivyo ambiwa mtumie geti lingine kwanini mlikataa? Mlitaka kushangiliwa? Mlitaka kiki? Mbona Maalim Seif aliwai?
IMG_0586.jpg
 
Hatuwezi kukubali chadema wanajisi msiba wa marehemu mzee wetu mkapa, nchi hii ina intelijensia kali ambayo tulifahamu kwa muda mrefu kwamba hawa watu wanataka kunajisi msiba.

Siasa za matukio zimepitwa na wakati.
Hiyo intelejensia ilijua Mzee Mkapa atafariki?
 
Wamefika saa tatu tena na msafara wa magari yao wakati wanajua fika utaratibu ulikuwa ni kuanzia Karimjeee mnaletwa na magari hadi taifa ..., ukumsikia Dr Abbasi?

Kwani mlivyo ambiwa mtumie geti lingine kwanini mlikataa? Mlitaka kushangiliwa? Mlitaka kiki? Mbona Maalim Seif aliwai?View attachment 1519643

Maalim Seif ni CCM lialia tu
 
Walikuwa wapi mpaka waingie wakati Rais ameshaingia ndani? Itifaki lazima izingatiwe.
msiba kama huu viogozi wenye busara hutumia nafasi hiyo kuunganisha taifa. ila serikali isiyo elewa wajibu wake hujimaliza kwa kugawa wananchi wake katika makundi makundi. hapa busara ilitakiwa itumike.
 
Ha ha CCM mtakuwa mazuzu no wonder mumelaanika na kukataliwa hadi uwanja kujaza watoto wa shule za msingi maana mumekataliwa kabisa vimebaki vinapiga kelele uwanjani kama ndege
Kwahiyo watoto wa shule za msingi hawatakiwi kumuaga kiongozi wao muasisi wa elimu bure ulitaka wewe tu unae soma memkwa ndio uhudhurie..
 
Nadhani wangewahi mapema kabla ya Rais wangeruhusiwa,ila kwenda wakati mkuu wa nchi ameshafika siyo busara,hata kama hatukubaliani kisiasa ni lazima tuheshimu mamlaka zilizopo haha kama hatuziheshimu
 
Msafara wa Viongozi Wakuu wa CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Freeman Mbowe, wamezuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru walikokuwa wameenda kuhudhuria shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa.

Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Mbowe aliongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Bara), Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mhe. John Mnyika, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Mhe. Hashim Juma Issa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, Mhe. Suzan Kiwanga na viongozi wengine waandamizi kutoka Makao Makuu ya CHADEMA, Viongozi wa Kanda 10 za chama, Viongozi CHADEMAwa Mikoa, Wilaya na Majimbo mbalimbali nchi nzima.


Kutoka Uwanja wa Uhuru hapa, Dar es Salaam.

=====

UPDATES:

CHADEMA yaitaka Serikali itoe maelezo kwanini viongozi wake wakuu wamezuiwa kumuaga hayati Benjamin Mkapa!



Picha na video clips za haya wanazo?
Jana walisema from 6am, 9am walichelewa na msafara wao.
 
jmushi1 relax mkuu..hayo ni maoni ya wadau.

Kama hujaridhika nayo achana nayo tu. Jf ni kama bahari, kuna kila aina ya viumbe...ukitupa kokoro tegemea mazaga kibao.

Wewe chukua samaki hayo mengine tupa.
I’m fine, napambana na timu roho kutu mkuu! We niachie! Hoja iwekwe mezani na siyo upuuzi wa maneno ya kwenye kanga na yenye kukosa utu na ubinadamu!

Mtu ni utu, mtu pasipo utu si mtu!

Sasa mkitaka hoja mtapata, mkileta maji taka, mjitajikuta mnaogelea kwenye vinyesi mkuu!😂
 
Nadhani wangewahi mapema kabla ya Rais wangeruhusiwa,ila kwenda wakati mkuu wa nchi ameshafika siyo busara,hata kama hatukubaliani kisiasa ni lazima tuheshimu mamlaka zilizopo haha kama hatuziheshimu
Rais alihakikisha amewahi kabla yao! Kwanza sasa hivi huyu anahitaji kura nyingine kuwa rais!
 
Raia makini wa nchi jambo kubwa la kwanza kulifanya ni kuitetea nchi yake, kulitetea taifa lake dhidi ya upuuzi, ujinga, unafiki, hila, uonevu unaofanywa na mtu yeyote au taasisi yeyote. Ifike mahali watanzania tukatae kuwa nyumbu, sio kuitwa nyumba bali kuwa nyumbu.

Kila kitu kiliwekwa katika utaratibu, na watu walisikia na kufahamu. Ila kwa kutuona sisi ni manyumbu, wamefanya upumbavu wakijua ni upumbavu wakitegemea kuna mambumbumbu watawaunga mkono. Jamani, imetosha, tushafanywa wajinga kiasi cha kutosha. Hebu sikiliza na ona hii
 
Kwahili viongozi wa chadema mmechemka.Magufuli kaingia uwanjani saa 2 na madakika.nyie mnakuja saa 3 huku si kutafutana lawama? Kwahili hapana mmezingua bana.
 
Viongozi lazima muoneshe mfano kwa kuzingatia itifaki mbona vyama vingine wameingia mapema tuu kabla Rais hajaingia? au na nyie tuwafananishe na wauza karanga na magazeti ambao hawana utaratibu maalum. Hapa mmeteleza hata hiyo barua msingeandika Mwanahabari Huru
 
Back
Top Bottom