Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Kwani si walifata utaratibu uliotangazwa Jana Safari ya kwenda taifa inaanzia jikmana kwa magari yaliyoandaliwa na serikali na kwa utaratibu maalimu Kama walifata Basi kunashida sehemu huko serikalini hasa kwenye kuratibu Hilo zoezi la kuaga na kama hawakufuata ule utaratibu Basi chadema wanamzaha na Mambo ambayo hayana mzaha mana viongozi wote wa kitaifa na kimataifa walikuwa na utaratibu maalumu kwa magari ya pamoja nasio binafsi
 
Kama wameona hiyo ndo njia ya kufanya mambo yaende vizuri msibani,basi kheri.
 
Kila jambo ni lazima lifuate UTARATIBU na itifaki. Kiongozi yoyote hawezi kuingia shughuli ya kitaifa kama Rais ameshaingia eneo la tukio. KAMA CHADEMA walitaka kwenda ealitakiwa wawasiliane na KAMATI ya itifaki toka shughuli imeanza ili wapangiwe muda wa kuingia uwanjani. Tofauti na hapo warudi tu nyumbani au waingie kila mmoja kama RAIA wa kawaida. CHADEMA KIBURI kitawaponza.
 
Utaratibu uliwekwa vizuri tu, kwanini viongozi wa kitaifa wa chama kikuu cha upinzani wanakosa busara?
Jana waliambiwa kabisa kuwa viongozi wote wa kisiasa wakitaka kwenda Uwanja wa Uhuru waende pale Karimjee kuna magari maalumu ya kwenda kule na pia leo sio siku ya wananchi kwenda kuaga mwili pale ila viongozi wa Serikali na wageni wengine.
Hivi Mbowe na utu uzima wake anashindwa vip kuepuka hizi taharuki, haya magari yao walitaka wakayaweke wapi?
Kuna wakati tukubali kuacha ujinga kwenye mambo ya maana.
 
Hahah

Viongozi wa nchi walikuwepo? Kama waliwahi kufika kabla mkuu wa nchi ajafika itakuwa wameonewa ila kama wamefika baada ya rais ni sawa tu kuzuiwa.
Aaah mkuu acha hizo, mbona Majaliwa alikuwapo jana? Wala geti halifungwi kwa kisingizio kwamba kuna kiongozi ameshatangulia kuingia.
 
Kwenye post zangu za jana nilishauri Lissu kutokwenda kwenye huo msiba, ninajua vyema mtazamo wa serekali hii chini ya Magufuli dhidi ya Lisu. Hapo tatizo la kuzuiliwa ni Lisu, na kwa vyovyote vile angeingia hapo uwanjani lazima angeshangiliwa vibaya sana, jambo ambalo lingezua fedheha na Karaha kubwa kwa serikali.

Ni nani asiyejua kuwa Lisu na Magufuli kuwa hawaivi chungu kimoja? Hivi hao viongozi wa Chadema walitarajia serikali na ccm, wangekubali cdm wachukue point za mezani mbele yao?
Wameenda kabla Ya Rais au baada, kama ni baada Ya Rais imekula kwao.
 
Kuingia wa mwisho mtu kama lissu ni kuvuruga attention ya watu waliotulia maana uwanja ungelipuka ,ni kama msiba wa ruge diamond alienda wa mwisho wakamrudisha maana alianza kuchukua attention ya watu ,angefika on time kusingekuwa hata na bugdha
Wameonyesha dharau kubwa Sana, na ni utomvu mkubwa wa nidhamu.
 
Na vile wamepata mashabiki akili kama zao basi wanawapelekesha watakavyo. Watu wanatokwa povu hapa wakati viongozi wao ndo wenye makosa.
Siasa za upinzani Tanzania ni za kijinga sana, utaratibu unajulikana ila unavunjwa makusudi ili tu kupata huruma ya raia wasio ujua utaratibu.
 
Hakuna cha kushangaza-uwepo wa Lissu ungeweza kuibua hamasa na shauku tofauti na kile kinacho endelea pale. Umpende Lissu usimpende, watu wangekua na shauku ya kumuona huyo mtu ambae risasi 16 haziku mmaliza-huu nu muujiza. Watu wa protokali wangelimaliza hili na CDM jana, sasa wamelikoroga.
 
Kwahiyo hakuna MTU yeyote aliyeingia baada ya Rais kuingia hapo uwanjani?

Itoshe kusema tu mwenyekiti wa ccm na watu wake ni waoga tu.
#2020
#RIPMzeeMkapa
Kama wamefika baada ya Mh. Rais kuingia ni sawa kuzuiliwa nje. Kiitikadi Mh Rais akisha ingia mahali gate lina fungwa. Poleni ndugu zangu wa Chadema. Wahini Mtwara kwenye mazishi. Na mjithidi pia kufuta protokali.
 
[emoji16][emoji16][emoji16]Yaani hapa ndio huwa siwaelewi watz wenzangu kuwatetea hawa jamaa.

Hawa ni wahuni tu kama manzese,tofauti yao wao ni maarufu na wanavaa suti safi.

Toka jana msemaji wa serikali ametangaza,kwa utaratibu wa viongozi wa uma,wanasiasa na wageni wa alikwa kwenda taifa kuaga mpendwa wetu,wataacha magari karimjee hall na kupanda gari maalum zilizoandaliwa kwenda huko.na muda ni kuanzia saa moja na nusu asubuhi.

Watu wanaingia uwanjani saa tatu na msafara wao binafsi,kama si kutafuta kick za kipuuzi ni nini?
 
Kujitangaza ni kwa hoja na hoja zinajibiwa kwa hoja. CCM msitugawe Tanzania ni moja tofauti yetu ni itikadi tu.
Kuna utaratibu uliotangazwa Jana kwa viongozi wa Taifa na kimataifa kuhusu kwenda Taifa pia kuna vitu vingine havihitaji kujiongoza Bali kuongozwa vipi Chadema tulifuata utaratibu pia kwa familia yenye adabu Mtoto anatakiwa kufika nyumban mwisho saa 12 kabla baba hajaingia ukikuta baba ameshaingia tafuta mbinu nyingine ya kuingia ndani kistaarabu vinginevyo baba atajua umechelewa na fimbo zitakuhusu.
 
Kwahiyo hakuna MTU yeyote aliyeingia baada ya Rais kuingia hapo uwanjani?

Itoshe kusema tu mwenyekiti wa ccm na watu wake ni waoga tu.
#2020
#RIPMzeeMkapa

Yani uingie na msafara wako baada ya kuingia Rais na kuanza kuhutubia? Hii si itakuwa fujo? Mbona Maalim Seif yupo na ameingia? Kwa hiyo chadema wao ni muhimu kuzidi Jakaya ambaye amewai uwanjani mapema?

Kwanni chadema walitaka kujipatia umaarufu kupitia msiba? Kwanini hawakuwai wakaingia?
 
Back
Top Bottom