Msafara wa Waziri huku Kigoma, ulimgonga mjomba wangu lakini cha ajabu hawakusimama kumuangalia. Hivi ni kweli hii ndo Tanzania tunayoitaka?

Maisha ni fumbo hakuna aijuaye kesho.

Pumzka kwa amani mjomba jamii forums ni jukwaa kuu hakika litafanyiwa kazi na wahusika.
 
Pole Sana ndg,Ila mjomba nae hajui kuwa zile chuma huwa zinasambaa barabara yote na spidi ya hatari maana ukijichanganya tu unakula tairi,whata if tukisema mjomba akitaka kuvamia kiongozi na msafara wake?
 
Pole Sana ndg,Ila mjomba nae hajui kuwa zile chuma huwa zinasambaa barabara yote na spidi ya hatari maana ukijichanganya tu unakula tairi,whata if tukisema mjomba akitaka kuvamia kiongozi na msafara wake?
Alikua kwenye mishe zake na Alikua anapaki bodaboda kando. Swala sio kwamba kwa Nini wamemgonga. Ila shida Ni Ile utu wa kwamba umesababisha ajali inahitaji uonyeshe ushirikiano wowote Hata wa kumjulia Hali muathiriwa. Unafikiri aliyemgonga aliwaza Nini, Kama sio kusema tu "achana nae" ndo maana wakaendelea na safari zao. Hakika utu umetoweka.
 
Watch out
Mwezi wa Saba umepoteza Ndugu kwa kukosa PF 3 means ni kifo cha kuvuja Damu.

Mwezi Septemba umepoteza mjomba kwa ajili ie Kifo cha kuvuja Damu tena.

Msiba wa Kuvuja Damu ie kuchomwa kisu, ajali, kipigo nk nk kwa baadhi ya mila za Kiafrika ni laaana ambayo isipodhibitiwa itawalamba! Fanyeni ibad kadri ya Imani yenu kukomesha!

Msiba wa kujiua kwa Sumu, Kujinyonga nk.

Kuvimba tumbooooo na hatimaye kuondoka.

Mkuu hivi vitu vikiwaandama kwenye ukooo mtaishia kulaumu kila mtu. Unaishi Afrika Bara Jeusi tiiii acha kulalamika.
Fanya ibada!
 
Kwa hiyo wewe ungefanya sherehe au
Hiyo ni nukuu ya shangazi,malkia chura aliyotoa kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya wakala wa chama chake anayedeal na utekaji
 
Nimtaje jina alafu kesho... au bas tu
Sio lazima umtaje kwa jina,unaweza Hata kutaja ziara iliyokuwepo huko Kigoma siku hiyo...yeye mwenyewe anaweza hata kukuambia hakuwemo kwenye gari siku hiyo.au Hata akasema alisikia kboom ila hawakujua ni nini.
 
Kwa Serikali hii!
Nadhani kama aligongwa na kufa basi hakuna namna!
Lakini kama angekuwa majeruhi,baada ya kupona angefunguliwa mashitaka ya kuingilia msafara wa PM.
 
Nimesoma comment za watu flani machawa ambao CCM ni kipaumbele kuliko kitu chochote Duniani.... Kwa kweli nimeshangazwa sana.. Ngoja niishie hapa tu. Basi
 
Pole,
Yale magari huwa yanakimbia mno.
Inatakiwa traffic watangulie kuhakikisha njia ni nyeupe.

Poleni wote.
 
Na wanajinasibu kuwa ni nchi ya amani, Kama amani mbona wanakimbizana hivo, Wanamuogopa nani?

Pole mkuu. Mungu amuadhibu huyo mkimbiza magari na walinzi wake.

Ile kanuni ya "Kifo ni Kifo tu" haiwezi ku-apply hapo katukosea sana.
 
Pole ndg
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…