Msajili wa vyama vya siasa amemtaka mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Maalim Seif ajieleze kwanini alisafiri hadi Kilimanjaro na kupanda jukwaa moja na Tundu Lissu wa CHADEMA kumpigia kampeni.
Kiongozi wa chama Zitto Kabwe amesema wanatarajia na mwenyekiti wa TLP mzee Mrema atajieleza pia.
Maendeleo hayana vyama!
View attachment 1608349
======
Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa imekiandikia barua Chama cha ACT Wazalendo ikikitaka kijieleze kwa nini kisichukuliwe hatua baada ya Mwenyekiti wake, Maalim Seif Sharif Hamad kupanda jukwaa la mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu katika mkutano uliofanyika Moshi mjini Oktoba 19, 2020.
Akizungumza na Mwananchi Digital Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alikiri ofisi hiyo kuipatia ACT barua hiyo
Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 22, 2020 na Mwananchi, Naibu Katibu mkuu wa ACT Wazalendo, Joran Bashange amekiri kupokea barua hiyo na amesema wanaijibu.
“Ni kweli tumepokea barua, kosa letu ni mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kusimama jukwaa la mgombea mwingine,” amesema Bashange.
Pia, amesema barua hiyo inahoji ni kwa nini mikutano ya ACT Wazalendo inahudhuriwa na viongozi wa vyama vingine na wa dini wanaowaunga mkono.
“Sheria ya vyama vya siasa iko wazi inasema, mtu anapovunja sheria anahukumiwa, yaani ahukumiwe na mahakama, sasa yeye anatafsiri anataka atupe adhabu, adhabu gani? aende mahakamani,” amesema Bashange.
Chanzo: Mwananchi