Uchaguzi 2020 Msajili amwandikia barua Maalim Seif akimtaka ajieleze kwanini kapanda jukwaa moja na Tundu Lissu kule Kilimanjaro!

Uchaguzi 2020 Msajili amwandikia barua Maalim Seif akimtaka ajieleze kwanini kapanda jukwaa moja na Tundu Lissu kule Kilimanjaro!

Msajili wa vyama vya siasa amemtaka mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Maalim Seif ajieleze kwanini alisafiri hadi Kilimanjaro na kupanda jukwaa moja na Tundu Lissu wa CHADEMA kumpigia kampeni.

Kiongozi wa chama Zitto Kabwe amesema wanatarajia na mwenyekiti wa TLP mzee Mrema atajieleza pia.

Maendeleo hayana vyama!
View attachment 1608349

======

Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa imekiandikia barua Chama cha ACT Wazalendo ikikitaka kijieleze kwa nini kisichukuliwe hatua baada ya Mwenyekiti wake, Maalim Seif Sharif Hamad kupanda jukwaa la mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu katika mkutano uliofanyika Moshi mjini Oktoba 19, 2020.

Akizungumza na Mwananchi Digital Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alikiri ofisi hiyo kuipatia ACT barua hiyo

Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 22, 2020 na Mwananchi, Naibu Katibu mkuu wa ACT Wazalendo, Joran Bashange amekiri kupokea barua hiyo na amesema wanaijibu.

“Ni kweli tumepokea barua, kosa letu ni mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kusimama jukwaa la mgombea mwingine,” amesema Bashange.

Pia, amesema barua hiyo inahoji ni kwa nini mikutano ya ACT Wazalendo inahudhuriwa na viongozi wa vyama vingine na wa dini wanaowaunga mkono.

“Sheria ya vyama vya siasa iko wazi inasema, mtu anapovunja sheria anahukumiwa, yaani ahukumiwe na mahakama, sasa yeye anatafsiri anataka atupe adhabu, adhabu gani? aende mahakamani,” amesema Bashange.

Chanzo: Mwananchi
Kwani msajili hataki wanasiasa wapendane? Kupendana ni dhambi? Wasiopenda watu wapendane hawapendi amani.
 
Buberwa, je Seif anagombea nini huku bara. Huku Bara Seif ni moiga kura tu kama wewe au mimi na ana haki ya kwenda mkutano wa mgombea urais yeyote anayetaka yeye, ikiwamo rais Magufuli kusikiliza hotuba zake ili ajue anamchagua nani katika uchaguzi wa rais wa Jamhuri.

F
Kwa mujibu wa ofisi ya msajili wa vyama, seif ni mgombea wa kupitia ACT-WAZALENDO. Ofisi ya msajili ni chombo cha muungano hivyo haijalishi unagombea zanzibar au bara msajili anakusimamieni tuu kama msajili na mlezi wa vyama. Hivyo msajili usimfananishe na ZEC
 
Kumbuka magufuli japo ni mgombea lakini bado ni Rais. Kwahiyo anatekeleza majukumu yake ya urais kama kawaida.Hao marais wengine walikuja kwa ziara za kikazi, siyo kupiga Kampeni. Lakini hakuna sheria iliyokataza marais wa jirani kumuombea kura Rais wa nchi nyingine aliye madarakani.
Huoni hapo ni kuingilia uchaguzi Wetu?
Mbona hao mnaowaita mabeberu wakitoa tahadhari mnasema wanaingilia uchaguzi?
 
Mbona leo Mrema kapanda Jukwaa moja na MAGUFULI huko Kilimanjaro? kama ana ubavu amwandikie na Magufuli sasa....hivyo visheria vyao vya kipumbavu walivyowatungia wapinzani mwisho ni tarehe 28 by any means
Nafikiri Mrema hana Mgombea wa kiti cha Uraisi, yeye binafsi hagombei wala hana Ratiba yake ya kampeni kwa ngazi husika
 
Demokrasia inapitia changamoto nyingi sana
 
Back
Top Bottom