Uchaguzi 2020 Msajili amwandikia barua Maalim Seif akimtaka ajieleze kwanini kapanda jukwaa moja na Tundu Lissu kule Kilimanjaro!

Uchaguzi 2020 Msajili amwandikia barua Maalim Seif akimtaka ajieleze kwanini kapanda jukwaa moja na Tundu Lissu kule Kilimanjaro!

Ukisikia watu weusi tunaitwa manyani unaweza kuchukia lakini ndio ukweli wenyewe. Msajiili anamuandikia mtanzania ajieleze kwanini mtanzania apande jukwaa moja na mtanzania mwenzake, kisha yuko kimya huku watu wa nje wakiwa wamepanda kwenye jukwaa na rais kumuombea kura ndani ya nchi hii. Mfano Museveni, Ndayishimie na Chikwera
Usahaulifu na uchumia tumbo ndivyo vinaongoza watendaji wengi
 
Msajili wa vyama vya siasa amemtaka mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Maalim Seif ajieleze kwanini alisafiri hadi Kilimanjaro na kupanda jukwaa moja na Tundu Lissu wa CHADEMA kumpigia kampeni.

Kiongozi wa chama Zitto Kabwe amesema wanatarajia na mwenyekiti wa TLP mzee Mrema atajieleza pia.

Maendeleo hayana vyama!
View attachment 1608349

======

Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa imekiandikia barua Chama cha ACT Wazalendo ikikitaka kijieleze kwa nini kisichukuliwe hatua baada ya Mwenyekiti wake, Maalim Seif Sharif Hamad kupanda jukwaa la mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu katika mkutano uliofanyika Moshi mjini Oktoba 19, 2020.

Akizungumza na Mwananchi Digital Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alikiri ofisi hiyo kuipatia ACT barua hiyo

Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 22, 2020 na Mwananchi, Naibu Katibu mkuu wa ACT Wazalendo, Joran Bashange amekiri kupokea barua hiyo na amesema wanaijibu.

“Ni kweli tumepokea barua, kosa letu ni mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kusimama jukwaa la mgombea mwingine,” amesema Bashange.

Pia, amesema barua hiyo inahoji ni kwa nini mikutano ya ACT Wazalendo inahudhuriwa na viongozi wa vyama vingine na wa dini wanaowaunga mkono.

“Sheria ya vyama vya siasa iko wazi inasema, mtu anapovunja sheria anahukumiwa, yaani ahukumiwe na mahakama, sasa yeye anatafsiri anataka atupe adhabu, adhabu gani? aende mahakamani,” amesema Bashange.

Chanzo: Mwananchi
Hawa ni Matapeli wa Kisiasa tu...Rais ni Dr.Magufuli na Dr.Mwinyi wengine hawana cha kutuambia
 
ni kuzingatia za vyama vyao ACT wazalendo hairuhusu mgombea au mwanachama kumuunga mkono mgombea wa chama kingine akifanya hivyo anakuwa kajivua uananchama

View attachment 1607397
Haya tuseme hoja yako ni sawa. Tuoneshe sehemu ya katiba ya TLP inaporuhusu kupanda jukwaa moja na mgombea wa chama kingine na pia kuvalishwa kofia ya chama kingine.
 
Kusema kuwa na Mrema naye aandikiwe barua kwa kuwa naye amefanya hivyo ni utetezi wa kitoto sana.

Nilidhani kabla ya kufanya jambo linaloweza kuwatia kwenye mgogoro basi walau Mtu uwe na hoja zinazokuacha salama badala ya kusema tu "mbona na fulani amefanya".

Katika mazingira kama haya ya tume iliyopo nilidhani Wapinzani wangekuwa makini zaidi badala ya kukiuka sheria makusudi na kusubiri uadhibiwe ili utafute huruma ya Wananchi.

Na tunavyoijua tume mnaweza mkaadhibiwa na Mgombea wa ccm akaachwa na ikabaki hivyo...sasa sijui itakuwa mmepata au mmepunguza.
Wewe ndo una hoja za kitoto zaidi. Tume hawawezi kufanya unachofikiria sababu boss wao keshafanya hayo wanayoyabainisha. Hii inaifanya tume kukosa nguvu za kusimamia unachokihofia.
 
Hawa bendera fuata upepo wanajua hilo? Hawajui kwamba ukisimamisha mgombea wa urais halafu ukaenda kumpigia kampeni mgombea wa chama kingine ni sawa na kufanya coalitions.
Hata kumuombea kura mgombea asiye wa chama chako ni sawa na kufanya coalision. So Mlema yuko mlemle.!!
 
Wa
Ukisikia watu weusi tunaitwa manyani unaweza kuchukia lakini ndio ukweli wenyewe. Msajiili anamuandikia mtanzania ajieleze kwanini mtanzania apande jukwaa moja na mtanzania mwenzake, kisha yuko kimya huku watu wa nje wakiwa wamepanda kwenye jukwaa na Rais kumuombea kura ndani ya nchi hii. Mfano Museveni, Ndayishimie na Chikwera
Watanzania viongozi wanatudharau kweli sijui hata wanatuonaje, wanaona kama hatuelewi chochote kinachoendelea katika nchi hii 😂😂 sema Waafrika ni Waafrika
 
Kaandika barua wakati anakabidhi barua katoka tu magufuli nae yupo na mrema jukwaa moja, huyu msajili anaagaika na vitu vidogo sana.
 
Back
Top Bottom