Msajili asaidiwe asiinajisi Ofisi ya Umma. CCM + TLP, CHADEMA + ACT hawajavunja Sheria

Msajiri wa vyama vya siasa ijapokuwa ni jaji na muhudumu wa sheria, katika hili anahitaji msaada zaidi kuitafsiri sheria hii na kutafsiri matukio ya kisiasa kuliko kukariri na kuendesha ofisi kilumumbalumumba tu[emoji1534][emoji1548][emoji1536]
 
Hakuna walipoungana hakuna makubaliano yoyote ya kuungana..hebu msome tena Yeriko
 
Kuungana, kushirikiana, hayo maneno yanafanana na yanaweza kutumika interchangeably?
 
Again Mutungi and NEC have decided to sit on their brains!!....... Wanaisaidia CCM wazi wazi kabisa.
 
Hivi huyu msajili kweli ni professional? Yaani kwa level yake asijue kutafsiri sheria kweli?🤔 Au ndo wale wale wanaojipendeza ili waweze kuishi maana vinginevyo hawez kusimama kwa miguu yake professionally akawa na ajira ya kuaminika.

Aibu sana 🤔🤔

Anashindwa kutofautisha kati ya COOPERATION na COALITION kweli? Sheria inaongelea Coalition (Muungano) na si cooperation (Ushirikiano) ambao wanao CCM na TLP.

Kama alikuwa amepanga akibebe chama chake kupitia hili AMECHEMKA
 

Tatizo unasoma sheria ukiwa na mindset potofu. Kuunga mkono ukiwa siyo magombea ni tofauti kabisa na wewe kuiomba tume ikuteua kuwa mgombea wa madaraka fulani, halafu ukishauruhusiwa kugomea madaraka hayo unatumia nafasi hiyo kumnadi mgombea mwingine kabisa badala ya kujinadi mwenyewe.

Hiyo ni kuvunja sheria, kwa sababu unakuwa unatumia raslimali za Tume kama Mgombea aliyetuliwa na tume kwa kuhakikishiwa ulinzi wa serikali na kinga ya kutumia vyombo vya habari vye aumma bila kusumbuliwa kumfanyia kampeini mdombea mwingine ambaye naye ametuliwa na tume na anatumia pia raslimali za tume hizo hizo; wanasheria wengine huiita double jeopardy.

CHADEMA na ACT wanachoweza kufanya ni kwa mmoja wao kujiondoa kwenye kinyanga'anganyiro ili afutwe kwenye daftari kuwa siyo mgombea tena anayehitaji ulinzi wa serikali ndipo aanze kumnadi mtu wake; lakini siyo wote kusimama pamoja kama wagombea wakati mmoja anamnadi mwingine.

TLP wanaomnadi magufuli, wanafanya hivyo kama raia tu, siyo kama mgombea aliyeteuliwa na tume.
 

Kwa hiyo ccm na tlp waliungana?
Akili mavi kabisa!
 
Usidanganye watu hata kama umeteuliwa kugombea tume haikulazimishi kufanya kampeni, mfano ukiishiwa pesa ya kampeni NEC au Msajili atakupa?
 
Usidanganye watu hata kama umeteuliwa kugombea tume haikulazimishi kufanya kampeni.
Ndipo unapokosea; haulamishiwi kufanya kampeini, lakini huwezi kutumia nafasi ya kuteuliwa kumfanyia kampeni mteuliwa mwingine; tafuta wadadavuzi wa sheria wakueleweshe tafsiri inayoitwa double jeopardy.

Hata sheria ya kunyongwa inalazimika kuongeza maneno "hadi kufa" kutokana na msingi huo huo. Nina imani Wakili msoni naye anajua hilo labda anataka kulivunja kwa makusudi tu.
 
Leta MO yao kati ya TLP na CCM, au waliungana vipi?
 
Alie kuambia wanaungana ni nani?
 
Mmeishiwa HOJA nyie. Kuna tofauti kati ya "KUUNGANA" na "KUSHIRIKIANA"
 
Tunazungumzia sheria ya uchaguzi kifungu cha 11A Sura 258 inasema COALITION kwa kiswahili MUUNGANO, unataka kusema mgombea akisema kura zangu mpeni fulani tayari wameungana, mbona iko wazi tu CCM mnafeli wapi.
 
Hawa jamaa wameamua kuweka taaluma zao pembeni na kutumikia matumbo. Ni wote tu - mahakama, polisi, NEC, Uhamiaji, TRA, nk. very sad. CCM itaondoka Watanzania watakapoamua. Siyo kwa kura lakini. Kivingine.
Ni ngumu sanaa kuitoa Ccm madarakani... mwalimu wangu wa constitutional law aliwai kuniambia Ccm wanabebwa na katiba ambayo ilitungwa kwa copying and pasting kutoka katiba ya tanu....
 
What about this?
 
Nimesoma hicho kifungu cha sheria husika na pia barua ya msajili wa vyama. Barua ya msajili wa vyama inaonya kuhusu "ushirikiano" wa vyama lakini kifungu cha sheria ya vyama vya siasa kinaongelea "muungano" wa vyama.

Barua aliyoandika msajili imepotosha sheria kwa malengo ya kukibeba chama fulani. Kwa hiyo hivi vyama mfano ACT, Chadema, Chauma na wapenda haki wote kama TLS, LHRC n.k vitoe barua za wazi kumuuliza huyu msajili anayetumika kuwa ni kifungu gani cha sheria kinaongelea "ushirikiano" hata "endorsement"? Ni hicho tu.
 
Good Idea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…