Labda huyu msajili atuambie Chama cha TLP kinachomnadi mgombea wa ccm ndugu Magufuli sio chama cha SIASA.
Kwa tafsiri ndogo ya kifungu cha 11A cha sheria ya vyama vya siasa Sura 258 iliyonukuliwa na msajiri hapo, ni kwamba sheria inahusu KUUNGANA KWA VYAMA yaani kwa kizungu wanaita merging/mergermation au Coalition.
Sio hii inayotumika na Chadema na ACT wala inayotumika na CCM na TLP ambayo sio muungano bali ni gentlemen agreement au Cooperation. Au kwa siasa za Marekani huitwa endorsement.
Chadema na ACT walijua tangu mwanzo kwamba ccm na msajiri wametegesha zengwe hili ili kusiwepo na muungano kama ule wa UKAWA ndiomaana utaratibu huu wa KUUNGA MKONO mgombea mmoja wapo wa wagombea ulichelewa.
Kwa lugha rahisi ya kitaalamu, hakuna muungano wowote uliopo kati ya Chadema na ACT wala hakuna muungano wowote uliopo kati ya CCM na TLP. Kilichoko kitaalamu huwa kinaitwa kuunga "mkono mgombea flani" ama huitwa endorsement kwa siasa za kimagharibi hasa za USA na UK, Cooperation ama kijeshi hasa kijasusi huitwa gentleman's Agreement. Tena kwenye ujasusi hutumika pale mnapogongana kwenye anga la espionage.
Msajiri wa vyama vya siasa ijapokuwa ni jaji na muhudumu wa sheria, katika hili anahitaji msaada zaidi kuitafsiri sheria hii na kutafsiri matukio ya kisiasa kuliko kukariri na kuendesha ofisi kilumumbalumumba tu.
Endelea kujipatia Kitabu cha Ujasusi kwa OFA MAALUMU ya 25,000/= badala ya bei halisi ya 80,000/=.
Lipia 25,000 kwa 0788887887 (Yericko Nyerere) kisha tuma majina yako na mahali ulipo.
Kwa Dar Kitabu kitaletwa ulipo Bureeee. Nje ya Dar utalipia usafiri 8,000/=
Na Yericko Nyerere
Pia soma > Uchaguzi 2020 - Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa: Vyama vya Siasa vinavyotaka kushirikiana Uchaguzi Mkuu vimeshachelewa kwa mujibu wa Sheria