PreGE2025 Msajili asitisha ruzuku CHADEMA, atishia kusimamisha shughuli za chama wakiendelea kukaidi na kuwatambua viongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania kulingana na Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 18(6) cha sheria ya Vyama vya siasa, ametangaza leo Jumanne Mei 27, 2025 kusitisha kutoa ruzuku kwa Chama Cha Demokrasia na maendeleo Chadema hadi pale watakapotekeleza maelekezo ya Ofisi ya Msajili kutokana na Chadema kutokuwa na Viongozi wanaoweza kusimamia mapato, matumizi na marejesho ya fedha hizo za Umma.

Hatua ya Ofisi ya msajili wa Vyama vya siasa imefikiwa mara baada ya kueleza kuwa Chadema imekaidi mara kadhaa maamuzi ya Ofisi ya msajili, ikiwemo taarifa ya Mei 25, 2025, ambapo Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche akisoma Maazimio ya Kamati kuu ya Chama, alieleza kuwa maamuzi na maelekezo ya Msajili wa Vyama vya siasa kuhusu malalamiko ya Bw. Lembrus Mchome ni batili na hawatoyafanyia kazi.

Aidha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa imeendelea kusisitiza kuwa Bw. John Mnyika, Amani Golugwa, Ali Ibrahim Juma, Godbless Lema, Dkt. Rugemeleza Nshala, Rose Mayemba, Salima Kasanzu na Hafidhi Ali Salehe sio viongozi wa Chadema samvanva na watendaji wengine wote walioteyluwa katika Kikao cha Baraza kuu la Januari 2025.

Taarifa ya Msajili wa Vyama vya siasa iliyochapishwa na kusainiwa na Abuu Kimario, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na elimu ya Uraia, imewasihi pia wananchi, wadau na mamlaka na taasisi za serikali na binafsi kutowapa ushirikiano na huduma wanachama walioorodheshwa hapo juu, endapo watakuwa wakihitaji huduma fulani kama Viongozi wa Chadema, ambapo imeelezwa
kuwa Viongozi halali wa Vyama vya siasa ni wale tu wanaotambuliwa na Msajili wa Vyama vya siasa nchini.

Msajili huyo pia amebainisha kwamba endapo Chadema wataendelea kukaidi kutekeleza maamuzi na maelekezo waliyopatiwa basi Mamlaka husika zitatakiwa kuchukua hatua za kisheria na kijinai pamoja na kuwasimamisha wanaojifanya kuwa Vionglzi wa Chadema katika kufanya shughuli za kisiasa kwa mujibu wa Kifungu cha 21E cha sheria ya Vyama vya siasa nchini.

Msajili pia amekumbusha kwamba kwa mujibu wa sheria anayo mamlaka ya kusimamisha usajili wa Chadema endapo kitaendelea kuwatambua wanaojiita Viongozi wa Chama hicho, akivitaka Vyama vya siasa kuheshimu sheria ili kuepuka migogoro na mivutano isiyokuwa ya lazima.

Mkurugenzi wa Sheria wa Chadema, Dk Nshala Rugemeleza amesema wameona taarifa ya Msajili, hivyo watakwenda kupambana naye kisheria.

Majibu ya Mwanasheria wa CHADEMA kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi
“Nimesoma taarifa ya msajili wa vyama vya siasa, ina upotoshaji mkubwa na madaraka ambayo amesema anayatumia ni kutaka kuiua Chadema kwa makusudi .

Sasa majibu atakayopambana nayo yatakuwa ya kisheria yeye si mtu mwisho wa kutafsiri sheria.”

“Tutapambana naye kisheria dhidi ya hatua zake alizozichukua, maana amekiuka sheria ni ajenda ya siri ya kutaka Chadema ife,”amesema Dk Rugemeleza.
Duh! 🤕🤕 Sasa hapa chadema wataendesha vipi shughuli zao za kisiasa?? Najua Ina vyanzo vya mapato binafsi Ila sio kwa ukubwa huo kutosheleza uhitaji wake.
Kweli wameamua kumaliza chadema mazima huku wanateka na huku wanaziba mirija kiuchumi na Sasa njaa ikianza kushika Kasi tutahitaji zaidi ya Umoja kukaa sawa.
 
Kuna viongozi waliteuliwa baada ya uchaguzi wa mwenyekiti Lisu,,sasa Mr Liberata mchome akadai Kuna viongozi wa kamati kuu,waliteuliwa kiholela bila kufuta katiba,,yaani waliteliuliwa na jopo ambalo halikuwa linatambulika kikatiba
Nadhani hoja iliyopo kwa huyo msajili uchwara ni kuhusu akidi kwamba haikutumia..Je,nani ni mkweli kati yao??

Maana wao Chadema walisema kila utaratibu waliufuata .Japo juzi baada ya kamati kuu walikuja na lingine kwamba huyo msajili hata hana mamlaka ya kile anachokifanya.

Je,na hilo ukweli upo wapii?
Maana huyo ni Jaji mstaafu .Japo Siasa zimewafanya wengi kuweka uweledi wao pembeni.
 
Watakufa njaa.
Heche hana pa kula tena. mirija imekatwa.
Watajuta kumtukana Mbowe.
Mh. Mbowe aliwatahadharisha kuwa acheni kuwapa chama hawa wahuni! sasa matokeo ndio haya.
Hapo walipo wanaendelea bila ruzuku, sasa watakufaje njaa?
Kampeni zote hizo wanapiga bila ruzuku kwa taarifa yako tu
 
Wafuate sheria,wameshindwa kufuata hata sheria zao wenyewe mpaka mwenzao akaenda shitaki
Mealijili alikuwepo kwenye uchaguzi wa chamba mpaka uteuz wa viongozi, mbona hakusema kipindi chote hiko kuwa kuna dosari? Alikua wapi bwana?

Asingepitisha tu mwanzon kabisa angeeleweka, kwa record tu cdm haijavunja sheria kokote, kama wangevunja wangeburuzwa mahamani sikunyingi
 
Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania kulingana na Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 18(6) cha sheria ya Vyama vya siasa, ametangaza leo Jumanne Mei 27, 2025 kusitisha kutoa ruzuku kwa Chama Cha Demokrasia na maendeleo Chadema hadi pale watakapotekeleza maelekezo ya Ofisi ya Msajili kutokana na Chadema kutokuwa na Viongozi wanaoweza kusimamia mapato, matumizi na marejesho ya fedha hizo za Umma.

Hatua ya Ofisi ya msajili wa Vyama vya siasa imefikiwa mara baada ya kueleza kuwa Chadema imekaidi mara kadhaa maamuzi ya Ofisi ya msajili, ikiwemo taarifa ya Mei 25, 2025, ambapo Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche akisoma Maazimio ya Kamati kuu ya Chama, alieleza kuwa maamuzi na maelekezo ya Msajili wa Vyama vya siasa kuhusu malalamiko ya Bw. Lembrus Mchome ni batili na hawatoyafanyia kazi.

Aidha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa imeendelea kusisitiza kuwa Bw. John Mnyika, Amani Golugwa, Ali Ibrahim Juma, Godbless Lema, Dkt. Rugemeleza Nshala, Rose Mayemba, Salima Kasanzu na Hafidhi Ali Salehe sio viongozi wa Chadema samvanva na watendaji wengine wote walioteyluwa katika Kikao cha Baraza kuu la Januari 2025.

Taarifa ya Msajili wa Vyama vya siasa iliyochapishwa na kusainiwa na Abuu Kimario, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na elimu ya Uraia, imewasihi pia wananchi, wadau na mamlaka na taasisi za serikali na binafsi kutowapa ushirikiano na huduma wanachama walioorodheshwa hapo juu, endapo watakuwa wakihitaji huduma fulani kama Viongozi wa Chadema, ambapo imeelezwa
kuwa Viongozi halali wa Vyama vya siasa ni wale tu wanaotambuliwa na Msajili wa Vyama vya siasa nchini.

Msajili huyo pia amebainisha kwamba endapo Chadema wataendelea kukaidi kutekeleza maamuzi na maelekezo waliyopatiwa basi Mamlaka husika zitatakiwa kuchukua hatua za kisheria na kijinai pamoja na kuwasimamisha wanaojifanya kuwa Vionglzi wa Chadema katika kufanya shughuli za kisiasa kwa mujibu wa Kifungu cha 21E cha sheria ya Vyama vya siasa nchini.

Msajili pia amekumbusha kwamba kwa mujibu wa sheria anayo mamlaka ya kusimamisha usajili wa Chadema endapo kitaendelea kuwatambua wanaojiita Viongozi wa Chama hicho, akivitaka Vyama vya siasa kuheshimu sheria ili kuepuka migogoro na mivutano isiyokuwa ya lazima.

Mkurugenzi wa Sheria wa Chadema, Dk Nshala Rugemeleza amesema wameona taarifa ya Msajili, hivyo watakwenda kupambana naye kisheria.

Majibu ya Mwanasheria wa CHADEMA kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi
“Nimesoma taarifa ya msajili wa vyama vya siasa, ina upotoshaji mkubwa na madaraka ambayo amesema anayatumia ni kutaka kuiua Chadema kwa makusudi .

Sasa majibu atakayopambana nayo yatakuwa ya kisheria yeye si mtu mwisho wa kutafsiri sheria.”

“Tutapambana naye kisheria dhidi ya hatua zake alizozichukua, maana amekiuka sheria ni ajenda ya siri ya kutaka Chadema ife,”amesema Dk Rugemeleza.
CHADEMA WAACHE JEURI SI WAFANYE TU UCHAGUZI KWA KUZINGATIA AKIDI HATAKAMA MTAWACHAGUA WALEWALE.
 
Yani chadema bhana, muda mwingine hawaoni mbali, hivi wangesaini kanuni wangepungukiwa na nn? Maana walikuwa hawana shida na kanuni, maana muda sio mrefu watakoza kufanya siasa , kwa hoja ya kwamba wapisheni wanaoshiriki, mbili itisha baraza kuu, pitisha wale wale, ni kweli siku ya baraza kuu kuna wajumbe waliingia ambao sio wajumbe, ukitaka kuwa mpinzani lazima uwe smart zaid ya mtawala wasitumie njia moja tu, ya kugoma ......
Watumie njia zote za
Siasa za Akili
Siasa za nguvu
 
Huyu hapigani vita peke yake. Huyu ni askari mmoja tu katika jeshi zima. Inatakiwa kutumia akili nzito kukabiliana na ujinga wa namna hii. Papara hazisaidii kitu. Utulivu utasambaratisha mbinu za kijinga aina hii.

CHADEMA, na wote wanaoitakia Tanzania mema ni lazima kupambana na hawa kwa utulivu na mpangilio unaoeleweka
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kutoa mapendekezo ya kuwakabili hawa.

Mimi naanza kwa kupendekeza kuwa Mtungi awe mtu wa kwanza kuwa katika orodha ya adui wa mabadiliko ndani ya nchi hii. Wengine wote wanaofanya shughuli za kuizuia CHADEMA watambuliwe, mmoja baada ya mwingine, na mbinu za kuwadhibiti ziainishwe.

haisaidii kitu chochote kulia juu ya uonevu kijumlajumla tu, bila ya kujuwa adui hasa ni nani anayesababisha uharibifu mkubwa

Utalia CCM ni waonevu, na mambo chungu nzima, lakini hutaweza kupigana na CCM wote, na wala siyo CCM wote wanatoa maamuzi ya hovyo kama ya huyu mmoja na taasisi yake; pamoja na kwamba maamuzi yake yanaisaidia CCM.

Hawa watu ni lazima watambuliwe, na njia sahihi za kuwadhibiti zipatikane.

Kila mmoja wao atambue kuwa atawajibika moja kwa moja kwa matendo yake mwenyewe.
Sahihi .

Tunaanza na Mtungi
 
Mealijili alikuwepo kwenye uchaguzi wa chamba mpaka uteuz wa viongozi, mbona hakusema kipindi chote hiko kuwa kuna dosari? Alikua wapi bwana?

Asingepitisha tu mwanzon kabisa angeeleweka, kwa record tu cdm haijavunja sheria kokote, kama wangevunja wangeburuzwa mahamani sikunyingi
Hiyo si inatokana na mwanachadema kulalama akidi haikutimia!!
 
Chadema kinajifuta chenyewe kwenye orodha ya vyama vya siasa nchini mwetu. Hii inatokana na ubabe wao wa kutotii sheria za vyama vya siasa, kutotii mamlaka ya Msajili wa vyama vya siasa. Chadema imeamua kubaki kuwa chama cha wanaharakati Tanzania. Kikajisajili tu huko BRERA
 
Kuna kazi huwa Ni Ngumu sana zimejaa Laana sana imagine katika Turbulence kama hii Msajili wa vyama anapewa maagizo ambayo yanaweza Kupose hatari kwenye maisha yake na familia yake ila anapaswa kutekeleza

Kule Kenya alikuwepo Mtu anaitww Wafula Che ukati he was the chairperson wa Tume ya Uchaguzi ya kenya

Kuelekea 2027 General Election naona amekuwa Eliminated kwa Kifo tata sana
 
Daah na huyo Msajili ni Mwanasheria nikisema Elimu yetu ina mashaka sana wasizwa wanapinga..
Mkuu, mtu anaweza kubobea sheria kiasi cha kuweza kuipindisha bila wewe kujua.

Ndivyo wanafanya wanasheria na mawakili wengi duniani kote.

Wanatafuta upenyo wa kuingilia na kutokea kwa kila mstari wa sheria.

Hao unaweza kusema ni legal hackers (wadukuzi wa sheria)!
 
Kuna kazi huwa Ni Ngumu sana zimejaa Laana sana imagine katika Turbulence kama hii Msajili wa vyama anapewa maagizo ambayo yanaweza Kupose hatari kwenye maisha yake na familia yake ila anapaswa kutekeleza

Kule Kenya alikuwepo Mtu anaitww Wafula Che ukati he was the chairperson wa Tume ya Uchaguzi ya kenya

Kuelekea 2027 General Election naona amekuwa Eliminated kwa Kifo tata sana
Chebukati was already retired (January 17, 2023). He died of brain cancer, hypertension and diabetes.
 
Back
Top Bottom