PreGE2025 Msajili asitisha ruzuku CHADEMA, atishia kusimamisha shughuli za chama wakiendelea kukaidi na kuwatambua viongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
"Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa inapenda kuwakumbusha wanachama na Viongozi wa Chadema kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 19 cha sheria ya Vyama Vya siasa, Msajili anayo Mamlaka ya kusimamisha usajili wa Chama hicho endapo kitaendelea kuwatambua wanachama wake wa sasa inayodai kuwa ni Viongozi wa Chama hicho (Wale waliopatikana katika kikao cha Baraza kuu la Chadema la Januari 22, 2025).

Soma Pia: Msajili asitisha ruzuku CHADEMA, atishia kusimamisha shughuli za chama wakiendelea kukaidi na kuwatambua viongozi

Ofisi inaviasa Vyama vya siasa kuheshimu na kutekeleza sheria ya Vyama vya siasa na sheria nyingine za nchi ili kuepuka misuguano na mivutano isiyokuwa la lazima."- Taarifa ya Msajili wa Vyama vya siasa iliyochapishwa na kusainiwa na Abuu Kimario, Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano na elimu ya Uraia.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Siasa zimewashinda mpira kwapani.😂😂😂

Hiyu Msajili anaona CCM inavyovunja sheria na kupora chaguzi lakini anajifanya haoni
 
Hili lizee linataka kutuletea vurugu nchini. Shida ya mtungi ni nini? Mwisho wa siku watu wanaanza vurugu. Jamani waache wafanye siasa. Anatengeneza usugu kwa chadema.
 
LOOOooh, hii ni VITA iliyo wazi kabisa.
Huyu MSAJILI; ndiye anashikilia hatma ya nchi hii mikononi mwake; kweli?

Yeye ndiye anaye amua waTanzania wawe na siasa za mwelekeo anao upenda yeye?
Huyu ni MSAJILI wa VYAMA vya Siasa anaye ifanyia kazi CCM?

Nadhani kuna umuhimu wa kuwaweka viongozi wa taasisi kama hizi katika kumbukumbu maalum. Hawa siyo watu wa kuwaacha tu wavuruge matumaini ya waTanzania kwa manufaa yao binafsi.
Hawa ni lazima wajibu maswali muhimu huko mbele ya safari mambo yakisha tengemaa.
 
Nampongeza msajili kwa kuchukua hatua dhidi ya wakaidi. Msajili mitano tena
 
Jamani Mimi nina mchumba wangu ambaye tumeanzisha uchumba hivi karibuni.

Dogo ni bikra na sikutaka nifanye naye mapenzi kama alivyohitaji. Kuna siku nilimwamby nahitaji kwenda mbali kwa utafutaji, nkamwamby akimpata mtu amuoe.

Hiyo ilileta shida kwake kiadi cha kuugua sababu ananipenda na mimi ndo mtu wake wa kwanza, hapa nifanye nini niweze kumuacha bila ya maumivu
Kaafilwe huko na maujinga yako.
 
Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania kulingana na Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 18(6) cha sheria ya Vyama vya siasa, ametangaza leo Jumanne Mei 27, 2025 kusitisha kutoa ruzuku kwa Chama Cha Demokrasia na maendeleo Chadema hadi pale watakapotekeleza maelekezo ya Ofisi ya Msajili kutokana na Chadema kutokuwa na Viongozi wanaoweza kusimamia mapato, matumizi na marejesho ya fedha hizo za Umma.

Hatua ya Ofisi ya msajili wa Vyama vya siasa imefikiwa mara baada ya kueleza kuwa Chadema imekaidi mara kadhaa maamuzi ya Ofisi ya msajili, ikiwemo taarifa ya Mei 25, 2025, ambapo Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche akisoma Maazimio ya Kamati kuu ya Chama, alieleza kuwa maamuzi na maelekezo ya Msajili wa Vyama vya siasa kuhusu malalamiko ya Bw. Lembrus Mchome ni batili na hawatoyafanyia kazi.

Aidha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa imeendelea kusisitiza kuwa Bw. John Mnyika, Amani Golugwa, Ali Ibrahim Juma, Godbless Lema, Dkt. Rugemeleza Nshala, Rose Mayemba, Salima Kasanzu na Hafidhi Ali Salehe sio viongozi wa Chadema samvanva na watendaji wengine wote walioteyluwa katika Kikao cha Baraza kuu la Januari 2025.

Taarifa ya Msajili wa Vyama vya siasa iliyochapishwa na kusainiwa na Abuu Kimario, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na elimu ya Uraia, imewasihi pia wananchi, wadau na mamlaka na taasisi za serikali na binafsi kutowapa ushirikiano na huduma wanachama walioorodheshwa hapo juu, endapo watakuwa wakihitaji huduma fulani kama Viongozi wa Chadema, ambapo imeelezwa
kuwa Viongozi halali wa Vyama vya siasa ni wale tu wanaotambuliwa na Msajili wa Vyama vya siasa nchini.

Msajili huyo pia amebainisha kwamba endapo Chadema wataendelea kukaidi kutekeleza maamuzi na maelekezo waliyopatiwa basi Mamlaka husika zitatakiwa kuchukua hatua za kisheria na kijinai pamoja na kuwasimamisha wanaojifanya kuwa Vionglzi wa Chadema katika kufanya shughuli za kisiasa kwa mujibu wa Kifungu cha 21E cha sheria ya Vyama vya siasa nchini.

Msajili pia amekumbusha kwamba kwa mujibu wa sheria anayo mamlaka ya kusimamisha usajili wa Chadema endapo kitaendelea kuwatambua wanaojiita Viongozi wa Chama hicho, akivitaka Vyama vya siasa kuheshimu sheria ili kuepuka migogoro na mivutano isiyokuwa ya lazima.

Mkurugenzi wa Sheria wa Chadema, Dk Nshala Rugemeleza amesema wameona taarifa ya Msajili, hivyo watakwenda kupambana naye kisheria.

Majibu ya Mwanasheria wa CHADEMA kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi
“Nimesoma taarifa ya msajili wa vyama vya siasa, ina upotoshaji mkubwa na madaraka ambayo amesema anayatumia ni kutaka kuiua Chadema kwa makusudi .

Sasa majibu atakayopambana nayo yatakuwa ya kisheria yeye si mtu mwisho wa kutafsiri sheria.”

“Tutapambana naye kisheria dhidi ya hatua zake alizozichukua, maana amekiuka sheria ni ajenda ya siri ya kutaka Chadema ife,”amesema Dk Rugemeleza.
Anachokitafuta atakipata. Hilter also had a vision on a new Germany
 
Mjomba WA moshiii
kaondoka n. ruzuku y chamaaa hahaa siasa nyokonkweli zinahamia ch@umaaa
 
Mwanzo 18:14
Hakunagumu la kumshinda Mungu baba
 
Somen mithali 6:32

Nenden mith 28;4-16

Galatia 3:1...Ni nani al.....
 
Nilikuwa najiuliza hivi: hao viongozi waliteuliwa Januari 2025, na kosa halikuonekana, na limekuja kuonekana almost mwishoni mwa Mei. Na ni sheria gani waliotovunja waliteuliwa au aliyewateua, na adhabu yake pia ya kuwaengua ni kwa mujibu wa sheria gani? Naomba anayejua sheria iliyokiukwa anielimishe tafadhali.
 
Back
Top Bottom