Uchaguzi 2020 Msajili: Mgombea aliyesema ataingiza watu barabarani kama akishindwa Urais ametoa lugha za vitisho, siyo ustaarabu

Itabidi athibitishe huo uwezo mahakamani kwanza
 
Akisndwa kwa halali ni tofauti na kushindwa kwa kuibwa kura zake eti.
 
CCM itapata pigo kuuuuubwa sana pigo moja tu pigo takatifu pigo lililonyooka kabla ya uchaguzi mkuu ujao,moto unaofukuta kutokana na spana za wajumbe lazima utawababua tu.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Lissu sio kama lile tutusa lao ambalo tulidhani ndiye kumbe siye.
Lissu haangalii makunyanzi Bali anapiga mulemule, na muziki wake mtaucheza mwaka huu
 
Kwahiyo akishindwa anaingia barabarani. Barabara hizihizi zilizojengwa na Magufuli?
 
lisu kasema akiibiwa kura,hajasema akishindwa uraisi,majitu majinga Haya yako kama roboti
 
Msajili tuliza mukari,ccm tutashinda

Halafu najaribu kujiuliza mbona kama vile huyu Sisty Nyahuza amekua na publicity kubwa sana na wakati ni msaidizi kupita hata Francis Mutungi mwenyewe??

Au kwakua Mutungi ni mtungi?
 
Hajasema endapo atashindwa (feli) bali endapo kura zake zitafanyiwa figusi figusi na kuibiwa au kuchakachuliwa. Waweke sawa maneno yao na ana wasi wasi gani kama anajua hakuna wizi
 
Mwanzoni wanaanzaga hivyo hivyo ila baada ya matokeo ndo tunamuachia Mungu zinafata
 
Shida kubwa tuliyonayo katika nchi hii ni kua na taasisi dhaifu sana za umma zinazoongozwa na vibaraka wa rais anayetawala.

Wapinzani wakiibiwa kura wakachukua hatua ni uvunjifu wa sheria lakini ccm wakiiba kura ni halali tu wala haina shida.

Mwaka kesho lazima tupate katiba mpya ili ijulikane kama kuna umuhimu wa kuwa na ofisi kama hizi na kama kuna umuhimu viongozi wake wapatikaneje na ofisi ziwe huru zisiwe ni matawi ya ccm kama ilivyo sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…