Friends and Our Enemies,
Kila mwenye akili na uelewa wa mambo anafahamu kuwa chanzo cha machafuko haya yaliyotokea ni uongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo.
Chadema kupitia mwenyekiti wao Tundu Lisu na makamu wake John heche kwa nyakati tofauti fofauti walishawahi kunukuliwa wakisema nia yao ni kukinukisha ndani ya nchi hii ili matakwa yao ya katiba mpya na tume huru yaweze kufanyiwa kazi na mahasimu wao ccm.
Nanukuu kauli ya Lisu "Nyinyi wananchi kama mmejawa na uoga,kama hamtaki kuingia barabarani kupigania haki zenu,basi msilalamike,muache kulalamika,haki haipatikani kwa kuomba,haki inapatikana kwa kuidai kwa nguvu" ...mwisho wa kunukuu...
Kauli nyingine ya lisu..."kwa kuwa hawa jamaa wamegoma kukaa mezani,na wameonesha nia ya kutotaka majadiliano,dawa yake ni kukinukisha,tukikinukisha hapa.,watu wakaingia barabarani na kikawaka,hawa watakuja kukaa na kuelewa lugha yetu."..mwisho wa kunukuu...
Hayo na mengine mengi ni baadhi ya kauli ambazo chadema wamekuwa wanazitoa kuchochea fujo na umwagaji wa damu nchini.
Sasa kwa kuwa watu hawa siasa zimewashinda,msajili wa vyama vya siasa nchini usiwe na kigugumizi katika suala zima la kukifutia usajili chama hiki.
Kifute chama hiki kabla hakijazidi kulipeleka taifa letu kwenye machafuko kwa mgongo wa demokrasia.