Msalaba wa hili kanisa la African Independent Pentecostal Church of Africa(AIPCA) unamaanisha nini?

Msalaba wa hili kanisa la African Independent Pentecostal Church of Africa(AIPCA) unamaanisha nini?

Huu Msalaba Ni Aina Ya Misalaba Ya Zamani saana Kabla HaijaBoreshwa Na Roman Catholic..

Huo Msalaba Ulitumiwa/Unatumiwa mpaka leo na Eastern Orthodox Church au russioan Orthodox..

Nini maana Ya Hizo Cross Zote..

Hiyo cross Beam Ya kwanza Ina Represent Kile Kibandiko cha Maandishi kwenye Ule msalaba Uliowekwa na Pilato kwa ajili ya Kumsulubisha Yesu Na Hiyo Beam ndo Ile Sehemu Iliyobandikwa KiBao Cha INRI [Iesus Nazarenus Rex Iudaeorum.] au kwa Waswahili tunasema "Huyu ni Yesu Mnazareth Mfalme wa Wayahudi"

Hiyo Cross Beam ya Pili
kama Ukiiangalia Utajua Ni Beam ndefu kuliko Zote zo inawakilisha Sehemu ambayo Bwana Yesu walipomgongelea Mikono yake Kwenye Msalaba..

Hiyo Cross Beam ya Tatu Ukiangalia Vizuri Hiyo beam Ni kama iko Slanted/Sloped Yaani kiswahili Ni Kama Imeinama..Kwanza Inarepresent Kitu Kinaitwa suppedaneum, Yaani Pumziko La miguu..Hiyo ndiyo Sehemu Yesu alipopumzisha Miguu yake ..

swali Linakuja Kwanini Imepinda? Imeinama Na imepishana na Beam zingine mbili..?

kwa sababu Inarepresent Salvation During the Cross..

Upande wa Juu ulioinama Unawakilisha Yule Mwizi aliyekuwa Msalabani na Yesu Wa Upande w Kulia Kwake ambaye Alifutiwa Madhambi na Kuingia Peponi..

Upande wa Chini Ulioinama Unawakilisha Yule mwizi aliyekuwa Msalanami na Yezu Upande wa kushoto na Alimtukana yesu na Aliyekataa Ukombozi

View attachment 3154200

View attachment 3154225
Mashahidi wa Yehova wanasema haukuwa msalaba bali mti uliosimamishwa tu kama nguzo!
 
Tuseme ukweli tu, hii misalaba ya ajabuajabu ipo hata kwenye skafu, kanzu na kofia zile wanazovaa maaskofu wa makanisa yanayoheshimika na yana waumini wengi.
 
Pale kona ya Morocco jijini dar kuna kanisa linaitwa watakatifu wa siku za baadaye wao wameweka kitu kama mkuki badala ya msalaba kama ilivyozoeleka kuwa ni alama ya kanisa. sasa kile ni kitu gani? cha ajabu nje ya kanisa hilo la kifahari kuna uwanja wa basketball
 
NYOKA WA SHABA alitundikwa juu ili kila atakayepatwa na matatizo akimuangalia apate kupona. Hiyo ndio kusema alama iliyokuwepo kwenye noti ya shilingi mia tano na alama inayotumiwa na taasisi nyingi za afya tena wakati mwingine ni nyoka aliyejiviringisha msalabani ni concept ya nyoka wa shaba-mponyaji/tiba?
 
Kwa kifupi misalaba mingi tunayoiona si msalaba aliyotesewa Yesu Kristo na kutundikwa pale Golgotha. Hiyo ni misalaba ya kimasoniki, ina maumbo ya ajabu, angalieni hata ile ya makaburini maumbo yake. Ni misalaba ya vyama vya siri (secret society)
"Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa Pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anayefanana naye hata mmoja."
(Qur'an 112:1-4)
 
"Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa Pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anayefanana naye hata mmoja."
(Qur'an 112:1-4)
Inahusiana vipi na huu uzi ??
 
Nyie kina malaria2 na wenzako kina FaizaFoxy piteni kimyakimya, msiharibu mjadala huu hauwahusu, hapa hamjui kitu mnaona giza tu. subirini mjadala wenu uje
 
Back
Top Bottom