Msalaba wa hili kanisa la African Independent Pentecostal Church of Africa(AIPCA) unamaanisha nini?

Mashahidi wa Yehova wanasema haukuwa msalaba bali mti uliosimamishwa tu kama nguzo!
 
Tuseme ukweli tu, hii misalaba ya ajabuajabu ipo hata kwenye skafu, kanzu na kofia zile wanazovaa maaskofu wa makanisa yanayoheshimika na yana waumini wengi.
 
Pale kona ya Morocco jijini dar kuna kanisa linaitwa watakatifu wa siku za baadaye wao wameweka kitu kama mkuki badala ya msalaba kama ilivyozoeleka kuwa ni alama ya kanisa. sasa kile ni kitu gani? cha ajabu nje ya kanisa hilo la kifahari kuna uwanja wa basketball
 
NYOKA WA SHABA alitundikwa juu ili kila atakayepatwa na matatizo akimuangalia apate kupona. Hiyo ndio kusema alama iliyokuwepo kwenye noti ya shilingi mia tano na alama inayotumiwa na taasisi nyingi za afya tena wakati mwingine ni nyoka aliyejiviringisha msalabani ni concept ya nyoka wa shaba-mponyaji/tiba?
 
Kwa kifupi misalaba mingi tunayoiona si msalaba aliyotesewa Yesu Kristo na kutundikwa pale Golgotha. Hiyo ni misalaba ya kimasoniki, ina maumbo ya ajabu, angalieni hata ile ya makaburini maumbo yake. Ni misalaba ya vyama vya siri (secret society)
"Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa Pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anayefanana naye hata mmoja."
(Qur'an 112:1-4)
 
"Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa Pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anayefanana naye hata mmoja."
(Qur'an 112:1-4)
Inahusiana vipi na huu uzi ??
 
Nyie kina malaria2 na wenzako kina FaizaFoxy piteni kimyakimya, msiharibu mjadala huu hauwahusu, hapa hamjui kitu mnaona giza tu. subirini mjadala wenu uje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…