Msamaha: Mzee Kinana amuangukia Rais Magufuli kufuatia mazungumzo yake na makada wenzake wa CCM yaliyovuja

Msamaha: Mzee Kinana amuangukia Rais Magufuli kufuatia mazungumzo yake na makada wenzake wa CCM yaliyovuja

Alipewa NAFASI adhimu sana na kufaidi utumishi serikalini yeye na nduguze kiukweli alipaswa kuomba radhi kwani kujitia jeuri kungemgharimu sana yeye na watuwake wakaribu.
Umekula weeee Leo kusemwa kidogo unamkashifu prezoo? Ile ilikuwa ni kuvimbiwa bora angetulia kijijini kwake ale pensheni taratibu na kushauri kiutaratibu sio kiuwanaharakati.
Amefanya vyema kuomba radhi maana watu tunakosea muhimu kujirudi na kujirekebisha
 
Baada kinana na makamba kutikiswa,nimeona kuwa mjeda ni uboya tu kama maboya wengine.

Bado miaka mitano kwa roho mbaya zenu hamtapumua maana mioyo yenu imejaa giza,
Msigwa kamuomba msamaha kinana lakini hukusema hovyo,
Kinana kumuomba radhi magufuli iwe nongwa.
 
Umemsikiliza vizuri Kinana? Umemuelewa? Unajua ethics za uongozi wewe? Unajua umuhimu wa kipindi hiki kwa chama kuelekea uchaguzi mkuu?

Sasa elewa kuwa mzee Kinana ameombwa radhi ili kunusuru chama na kimaadili kaombwa aseme yale hadharani kurudisha imani ya wanachama.

Ndio maana hata lugha yake (tone) ilikuwa na dharau ndani yake. Mavuvuzela hamuwezi kuelewa hapo hata mpigwe nyundo kichwani
Duh.. Kwahiyo mwananchi na mpiga kura wa kule Nanjilinji alikuwa hana imani tena na ccm sababu ya ukimya wa Kinana?

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Ndio sababu mnasema Mbowe asipokuwa mwenyekiti hapo chadema inakufa?
 
Mkuu kama ulikua wrong, una haki pia ya kutuomba msamaha, kwani huwa tunaziamini sana porojo zako.
I was wrong on my opinion kumhusu Kinana, kuwa na wrong opinion, sio kosa la kuombea msamaha!.
Mfano sasa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais na wabunge, nikiandika opinion kuwa Tundu Lissu atamshinda Magufuli, ikitokea ni Magufuli ameshinda, nitasema I was wrong on my opinion on Lissu lakini sio kosa la kuombea msamaha!.
P
 
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana amejitokeza na kumuomba radhi Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Dkt. John Magufuli kufuatia matukio yaliyojitokeza siku za nyuma ikiwemo mazungumzo ya simu baina yake na baadhi ya viongozi wakongwe wa CCM yakimlenga moja kwa moja Rais Magufuli.

Kauli hiyo ya Kinana ameitoa akiwa jijini Arusha, ambapo pia alipata nafasi ya kukutana na viongozi wa CCM mkoa wa Arusha akiwemo Mwenyekiti wa chama Mhe. Zelote Steven na Katibu wake Mussa Matoroka ambao wamemshukuru kwa hatua hiyo.

Kinana ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe wa CCM, baada ya kustaafu alijiikuta katika malumbano na wanasiasa wenzake na pia viongozi wake ambazo hata hivyo hakuwahi kuzizungumzia.
====

My take: Waliokuwa wanadhani JPM ni moto wa mabua sasa wametambuwa kuwa walivyodhani haikua sahihi

kutofautiana na mkubwa hairuhusiwi
 
Mkuu hayo ni mawazo yako lakini yeye amesema anafikiri alikwenda mbali zaidi baada ya kukeleka. Hivyo hata msamaha ameomba kwa kufikiri tu lakini haamini kama anakosa.
 
Nakumbuka we jamaa niliwahi kukuletea clip juu ya kufufua reli ya Moshi toka Dar mwaka 2017 nadhani ukanambia hzo ndoto tu huyo Rais wenu hana uo ubavu! Nikakuambia muda utaongea ila nimeona mwaka jana December wachaga wakila nyama choma kwa mabehewa!

Acha nicheke kwanza, nenda leo hii ukaone kama hiyo treni kama inaoperate. Kisha uje na maelezo kwanini haioperate.
 
Pale Maiti inapoomba msamaha kwa msukule. kuna jipya gani?
Kama sio wewe atakuwa baba yako ndo yule msukuma aliefukuzwa kwa ajili ya kasuku pale ikulu.
Una hasira na huu utawala, utakufa mapema shauri yako.
 
I was wrong on my opinion kumhusu Kinana, kuwa na wrong opinion, sio kosa la kuombea msamaha!.
Mfano sasa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais na wabunge, nikiandika opinion kuwa Tundu Lissu atamshinda Magufuli, ikitokea ni Magufuli ameshinda, nitasema I was wrong on my opinion on Lissu lakini sio kosa la kuombea msamaha!.
P
Mkuu kwanza niseme, umefanya haraka sana kujiona ulikosea, ungesubiri kidogo, pazidi kupambazuka, naona kama hapa pia umefanya kosa kukubali ulikosea.

Ndugu PM, wewe unamjua Kinana Vizuri sana kushinda wengi humu JF, bado hujatupa maoni yako ya ukweli na yaliyo moyoni mwako, na pia hatuyategemei hivi karibuni.

Mountains, towers and the strongest structures on earth, can be brought down by an earthquake if a ritcher scale of 6.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha nicheke kwanza, nenda leo hii ukaone kama hiyo treni kama inaoperate. Kisha uje na maelezo kwanini haioperate.
Usikubali kujificha kwenye kichaka cha unafiki! Kuto kuto kutoa huduma kwa siku kudhaa si kumetokana na uhalibifu wa miundombinu yake kuharibiwa na mvua? But haimaanisha kuwa tren ndo mwisho wakutoa huduma mzee, same na daraja kukatika tu litafanyiwa matengenezo na magar yataendelea kupita
 
Tatizo liko wazi kuwa ni mradi uliofanywa bila upembuzi yakinifu ili kusaka sifa za kisiasa, hivyo kujikuta hailipi. Ingekuwa inalipa hilo daraja lingetengezwa.
 
Kipenga tu nasubiri
Ila mjihadhari na muwe na social distancing
 
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana amejitokeza na kumuomba radhi Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Dkt. John Magufuli kufuatia matukio yaliyojitokeza siku za nyuma ikiwemo mazungumzo ya simu baina yake na baadhi ya viongozi wakongwe wa CCM yakimlenga moja kwa moja Rais Magufuli.

Kauli hiyo ya Kinana ameitoa akiwa jijini Arusha, ambapo pia alipata nafasi ya kukutana na viongozi wa CCM mkoa wa Arusha akiwemo Mwenyekiti wa chama Mhe. Zelote Steven na Katibu wake Mussa Matoroka ambao wamemshukuru kwa hatua hiyo.

Kinana ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe wa CCM, baada ya kustaafu alijiikuta katika malumbano na wanasiasa wenzake na pia viongozi wake ambazo hata hivyo hakuwahi kuzizungumzia.
====

My take: Waliokuwa wanadhani JPM ni moto wa mabua sasa wametambuwa kuwa walivyodhani haikua sahihi

Mtu kama huyu alishika nafasi kubwa bila sifa. Lugha anayotumia kuomba radhi inaonesha hajui hata kupanga maneno. unawezaje kuomba radhi kwa kutumia neno 'labda?' Anaomba radhi kwa watu aliowaudhi halafu anasema labda niliwaudhi. Ni tabia ya kuomba radhi lakini uonekane ni shujaa. Hii ni hovyo! Nina hakika ameteta na marafiki zake na ndo wakashuri ajidai kuzungumza hayo. Na huenda walimteta tena Mkiti wao na kucheka na kuambizana ukisema hivi na vile atafurahia.
 
Duru za hakika kabisa zinatabanaisha ndugu Kinana huenda akagombea ubunge katika Jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya CCM.

Sababu kuu mbili zilizo mfanya agombee ubunge ni kwanza mzee yule anaheshimiwa mno na wana Arusha na sifa hiyo pekee uhakika wa yeye kutangazwa mshindi itakuwa mapema tu pengine hata saa mbili na nusu asubuhi haitafika!

Pili mara tu atapo kuwa mbunge ndugu Rais atamteua kuwa Waziri wa maliasili na utalii 😊.

Mungu ibariki Tanzania na Timu ya Yanga.
 
Back
Top Bottom