Tetesi: Msanii Alikiba ampa talaka tatu mkewe chanzo kikiwa ni ndugu na kurogana

Tetesi: Msanii Alikiba ampa talaka tatu mkewe chanzo kikiwa ni ndugu na kurogana

Kuishi nyumba moja na mama mzazi na mkeo uchague moja tu.
 
harusi zenye mbwembwe zikifanywa na maskini hazifikagi mbali..

alikiba anatoka ukoo maskini kitendo cha kufanya harusi ya mbwembwe tu ilikuwa kama analeta mkosi..

hela za harusi ya ali kiba zingewapa ndugu zake ali kiba mtaji.. wasingekomaa kuishi kwa alikiba..


ila harusi mnatumia hela nyingi huku ukooo wenu ni maskini.. mtagombana tu
Kwanini hela hizo harusi uzipigie hesabu za kuwapa ndugu?
 
Huenda ni zaidi ya inavyosemwa!
Ali Kiba atakuwa alivumilia Mengi toka kwa yule mwanamke!

Hadi kuamua kumwacha kwa talaka 3 hiyo tu inaonekana Ali amekasirika sana!

Yani hapo hakuna rejea[emoji108][emoji108]
Alichokasirika yeye mama kamshika mkewe uchawi,na mkewe atakuwa mchawi kweli(kwa akili za Kiba)mjuwe tu hawa vijana mama yao ndo kila kitu akisema huku msipite hawapiti hawa!
 
Ndio tatizo la ndoa za kishwahili mnapishana na ndugu kwenye korido Kama nzi. Afrika kuchomoka bado Sana unaweza kuishi na ndugu zaidi ya watano nyumba moja,Dada wa kazi anafanya kazi ya kupika kuanzia asubuhi Hadi usiku utadhan ni mpisha wa hotel.mnapika chakula kingi Hadi kinakosa ladha .
Acha uchoyo wewe mbona sisi tunaishi nao wengi tu.
 
Ni ushamba kupitiliza kurundika ndg nyumbani, kamwe huwezi kufurahia ndoa.
Kuna shida gani mwanaume kuwapatia wazazi makazi mengine?
Kwangu ni kwangu na mpenzi wangu.
Baba, mama, ndg wakija walijue kuwa wanaingia kwa himaya yangu tena kwa heshima.
Wansume tuwalinde wapenzi wetu dhidi ya ndg wakorofi au tufanyike kiungo.
Katiko hilo niko vyema kabisa.
This is sad,pole Amina..uwe haupendani na ndugu za mumeo na mumeo anawa support ndugu zake..hio atmosphere ni ngumu...bora ukapumue mwaya!!
 
Ila ya choyo mbaya sana!

Halafu tena ulozi kuingia humo?!
Mkuu zaweza kuwa ni fitina tu hizo.

Ushauri wa mwanamke ulikuwa sahihi. Hata kama wana uwezo, haikatazwi kusaidia ndugu, lakini si kwa kuishi pa1 maisha yote hata umri wa kujitegemea ushafika.

Kiba angeondoka na mwali wake kwenda kuanzisha maisha ama makazi mapya.

Huo mjengo angewaachia familia waliozowea kuishi pale, si ana pesa?

Mkamwana kuishi maisha yote na mkwewe ni jambo gumu sana, ndiyo maana yakaonekana hayo mauchoyo na mauchawi, lakini hivyo ni visa tu.

Sasa wamemvunjia mji ndugu yao, ambapo sifa hiyo ni mbovu sana hasa kwa watu wenye majina, maana inaonekana ni watu wasiofaa kwa ndoa na mifano ipo mingi.

Kama familia hiyo aliyoibeba Kiba ina mtindo huo wa maisha ya kizamani ya kurundikana, atamaliza wanawake kwa kuoa na kuacha.
 
Haya mambo hayaepukiki katika familia ambazo zilikuwa zinaishi watu 8 vyumba viwili na sebule ambayo ipo chumba cha nje kinajitegemea, wote kiba na diamond, maisha yao ndio hayo ndugu watajaa na wakuja hana nafasi wala neno kwenye familia na sababu kubwa ni kwamba tumepita wote pamoja

Mabaharia wenzangu, ukitaka kuoa anzisha mji wako, tofauti kabisa na unapoishi sasa kama una uwezo jengea wazazi wako (kama walikuwa wamepanga) kisha jenga kwako au panga uoe, nina imani baba yako angekuwa na akili kama za kiba usingejikuta kwenye familia ambayo ni baba mama na watoto, na wazazi pia mmeshaishi maisha yenu, waache watoto nao waishi yao
 
Kiba nae mjinga tu yani
Miaka yote had Leo ameoa
Na anaenda kuish Na ndugu wote
Kwema nyumba moja

Kwan alishindwa nn kuanzisha
Makaz yake

Wasanii wa bongo cjui wanakwama wapi
 
Mqanaume unaoa halafu unaishi na ndugu nyumba hiyohiyo hapo lazima maj yatazidi unga,raha ya ndoa uishi na mkeo na watoto wako. Vijana msiolee nyege au sifa hakikisha upo tayari kuishi na huyo mwanamle maana ndani ya nyumba ya wanandoa kuna mambo mengi sana ambayo ndugu hawatakiwi wayajue
 
Wasalaam wajamvi!

Msanii Alikiba a.k.a King Kiba amempa talaka tatu mkewe Amina raia wa kenya baada ya kushindwa kupata muafaka juu ya ugomvi wao na ndugu wa Alikiba na Mama wa Alikiba.

Ndoa ya King Kiba ilianza kuingia dosari baada ya Amina kutaka ndugu wa Alikiba wakajitafutie maisha yao na wajitegemee jambo ambalo lilizua taharuki na ugomvi mkubwa baini ya ndugu wa Alikiba na Amina..

Amina alidai ni vigumu kuishi na watu wengi vile ndani ya nyumba moja hata kama ni ghorofa na bado kuwe na amani...hivyo alimshauri alikiba awape mitaji wakajitegemee au awapangie nyumba nyingine.....

Hili jambo liliendeleza mgogoro mkubwa hadi Mama Alikiba kiingilia kati na kutaka Alikiba amuache Amina na akadai apendi hata watoto wa Alikiba kuwa pale....


Wakati hayo yakiendelea kutafutiwa uvumbuzi mtoto wa Alikiba aliugua na kupatwa ugonjwa ulio sababisha awe ana anguka kila muda.....hili lilichochea moto kwani ndugu na Mama Alikiba waliamua kufunga safari hadi kwa fundi ndipo alipotoa tv [emoji342] na kuwaonesha chanzo cha ugonjwa wa mtoto ikidawa amelogwa na Amina mke wa King [emoji146] kiba.


Hivyo basi Mama na ndugu baada ya kutoka kwa fundi walirudi na kumchana live Amina kuwa anataka kumuua mtoto wa King Kiba hivyo lazima aondoke jambo ambalo lilizua ugomvi mkubwa huku Amina akilia kama mtoto na kuwambie hawezi na hana tabia hizo labda kama wanataka aachane na ndugu yao lakini wasimsingizie....

Ugomvi ulikuwa mkubwa sana kupelekea Amina kubeba mwanae na kurudi kwao mombasa huku akitaka kupewa talaka maana ndoa imemshinda!


Mnamo mwezi wa nane mwisho King Kiba alimpa talaka Amina ili aendelee na maisha yake uku wakishirikiana kulea mtoto.


Wasalaaam
Ndio maana wakwe wa kiafrica siku zote mtoto akiwa na vijisenti vya kubadilishia mboga wanakuwa nuksi hata ingekuwa mimi ndio amina ningewatoa baru
 
Back
Top Bottom