Tetesi: Msanii Alikiba ampa talaka tatu mkewe chanzo kikiwa ni ndugu na kurogana

Tetesi: Msanii Alikiba ampa talaka tatu mkewe chanzo kikiwa ni ndugu na kurogana

Hata mimi nilipoia sikutaka ndugu wa kukaa muda kwangu tuachiwe nafasi na mke wangu ase
 
Case kama hii ilitokea kwa msanii blueface wa marekani ila yeye alichoamua ni kuwafurumusha mama yake na dada yake ili aishi na madem zake kwenye jumba lake kwa amani!!

Ukioa jitahidi kuwa na maisha yako mbali na familia hata mkeo atakuwa na uhuru zaidi na ndoa yake!!
 
harusi zenye mbwembwe zikifanywa na maskini hazifikagi mbali..

alikiba anatoka ukoo maskini kitendo cha kufanya harusi ya mbwembwe tu ilikuwa kama analeta mkosi..

hela za harusi ya ali kiba zingewapa ndugu zake ali kiba mtaji.. wasingekomaa kuishi kwa alikiba..


ila harusi mnatumia hela nyingi huku ukooo wenu ni maskini.. mtagombana tu
+1
Nimejikuta nakumbuka rafiki yangu mmoja alilazimisha harusi ya gharama na mkopo wa benki juu, alivyorudi honey moon , yaliyoendelea katika maisha yake yanasikitisha
 
+1
Nimejikuta nakumbuka rafiki yangu mmoja alilazimisha harusi ya gharama na mkopo wa benki juu, alivyorudi honey moon , yaliyoendelea katika maisha yake yanasikitisha
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Bala sanaa... Mkopo ukaanza kumtesa sasa
 
+1
Nimejikuta nakumbuka rafiki yangu mmoja alilazimisha harusi ya gharama na mkopo wa benki juu, alivyorudi honey moon , yaliyoendelea katika maisha yake yanasikitisha
[emoji23][emoji23]
 
Bongo kila kitu miyeyusho tu, yaani Amina alitaka kuingilia maslai ya upigaji wa watu, wakamshtukia wameona bora wamtimue mke wa ali kiba ili maslai yao/tumbo lao yaendelee kushiba
 
Ukisoma humu comments za wanawake/wasichana utagundua kuwa hawapendi kabisa ndugu wa wame zao

Yani wengi wanatamani sana kuolewa na mtu aliyefiwa na ndugu wote kitu ambacho hakiwezekani kabisa!
 
This is sad,pole Amina..uwe haupendani na ndugu za mumeo na mumeo anawa support ndugu zake..hio atmosphere ni ngumu...bora ukapumue mwaya!!

Ndio tatizo lililopo kwenye ndoa za Kiswahili. Halafu mtu unaanzaje kwenda kuishi kwa nduguyo hadi kuleta mtafaruku kwa wanandoa? Binafsi ninakuwa inclined kumuunga mkono mke vs ndugu wa mume na mume vs ndugu wa mke.
 
Ila ya choyo mbaya sana!

Halafu tena ulozi kuingia humo?!
Mbona kuna familia huwa wanaishi pamoja na kuelewana tu?!

Choyo au kitu gani?
Yaelekea na wewe unaendekeza sana KUJAZANA alikoolewa au kuoa ndugu yako. Neno CHOYO unalitumia kama silaha ya kuonesha ubaya wa mwanamke, lakini kuna mambo unapaswa uyatambue kuhusu mahusiano.

Unapoamua kuwa na familia yako na kuingia kwenye mahusiano wa ndoa na mwenza, uhusiano wako na familia unayotokea unaingia mipaka. Ni uswahili uliopitiliza mipaka kwa mijitu 8 mitu mizima na public hair zao kwenda kujazana kwa ndugu yao ambaye ana mke na watoto as if hiyo ni kambi ya wakimbizi.

Ukioa MKE usimjazie nyumbani ndugu zako as if umeajiri MATRON. Mamaako ana BWANAAKE (babaako) akae huko kwa mumewe, kakaako na dada zako nao pia wana wake zao na waume zao, kuna haja gani ya kujazana nyumbani kwako mpaka mkeo akose privacy? Uswahili huo!

Na kama wewe ni wa kike, ukiolewa haimaanishi mmeolewa ukoo mzima kiasi familiako ijitoe fahamu kuhamia ulikoolewa kama mahayawani. Ndoa ni taasisi ya watu wawili na sio ukoo. Umaskini nao uwe na limits za kuudisplay

Hayo majitu hovyo yaliyojazana kwa ndugu yao ndio MACHOYO, yanamnyima binti wa watu nafasi ya kuwa na mumewe. Unajua na hawa watani zangu wameathiriwa sana na uwepo wa kambi za wakimbizi huko Kibondo. Yaani wana hamu ya kujazana sehemu moja kama nguchiro kiasi hawana haya. Na hata hivyo muha na mwehu wamepishana padogo sana, ndio maana huyu naye anaachana na mkewe kisa ukoo wa nguchiro
 
Mara nyingi kunakuwa hakuna maelewano. Uishi na mumu, mama mkwe,mawifi, na watoto wa mume uliowakuta , loh hata mie yangenishinda
Kwani wakati unaolewa ukuyajua hayo? Walivyokuwa wanasema muwe mnaangalia familia za kuoa au kuolewa nazo ndo kama haya,kama uliwakuta wanaishi hivo na ukakubali kuolewa huna budi kuishi nao,labda kama maisha yalibadilika baada ya wewe kuolewa
 
Kama alijua basi apambane na hali yake. Why muishi nyumba moja ukoo mzima wakati uwezo wa kila mtu kukaa kivyake upo?
Ni matatizo ya kujitakia..inajulikana kabisa mke, mama mkwe na mawifi ni Mara chache sana wanapatana. Kwanini usababishe matatizo kwa kujitakia? Raha ya ndoa hasa kama ni changa mke na mume wakae peke yao kwa raha zao ndugu waje kutembea na kuondoka.

Kaambali
 
Back
Top Bottom