Management ni kitu muhimu sana.. pia awe karibu na fans wake kwenye social networks so that they can request his songs.....
Take my words Belle
Mbona wapo wengi tu ambao muziki wao haupigwi?
Ruttashobolwa uweke huo muziki wake hapa ili tuusikie;
Mtie moyo tu, hata ubuyu ulianza kama mchicha.
Hapo kwenye redio utanisamehe tu.Mimi sio msikilizaji mzuri labda itokee tu bahati mbaya.Pamoja nakumkubali umewai kujiuliza ni wangapi wanao mkubali kama wewe huchagua nyimbo zake kwenye radio stations zichezwe? Kila mtanzani ukimuuliza utasikia ana msifu na kusema nyimbo zake ni nzuri na anazipenda lakini ukichukua wasaha wakusikiliza radio hata nusu saa huwezi kusikia nyimbo yake ikiombwa..hivi kuna nini
Belle 9 kama matonya tu wanaimba vizuri ila ndo hivo...hadi nimehisi kuwaonea huruma
Hili nalo limekua kama fashion siku hizi lakini mimi sikubaliani hata kidogo na hii mbinu ya kipuuzi.Labda kwasababu hachukui wadada wakali macelebrities wa bongo.Huoni Nuhu Mziwanda pamoja na utahira wa ubongoni ana jina sasa kisa anamchukua shishi baby?
Hii ndiyo bongo.
Yani bado najiuliza tatizo kick na scandal? yani Nuhu kutokana na shilole alitoa wimbo uka hit na akapata show.duu!Labda kwasababu hachukui wadada wakali macelebrities wa bongo.Huoni Nuhu Mziwanda pamoja na utahira wa ubongoni ana jina sasa kisa anamchukua shishi baby?
Hii ndiyo bongo.
kamfanya masogange kuwa maarufu zaidi kuliko yeye kwa kumtumia kama video queen.
Wana jamvi wasalaam...
Wana jamvi katika adhabu ambayo anaweza kupewa mtu na ikamuumiza sana na akashindwa kujua la kufanya au suluhu ni adhabu ya kupuuzwa.
Adhabu ya kupuuzwa ndio aliyo pewa msanii Bell 9 na watanzania walio wadau wa muziki!
Bell 9 ni mmoja wa wasanii wenye sauti nzuri,mtunzi mzuri na mwimbaji mzuri lakini hakuwai kufurahia matunda ya kipaji chake kama wengine!
Bell 9 pamoja nakujua hayo yote na baadhi ya watanzania kusifu nyimbo zake lakini zimekuwa zikikosa muda wa hewani wa kutosha kama nyimbo nyingine na ni vigumu nyimbo kupata muda wa hewani kwenye radio station na Tv kama walaji hawauchagui wimbo husika!
Watanzania, Bell 9 amewakosea nini? Kwanini mna mpuuza kiasi hiki? Pamoja na msanii huyu kutoa wimbo mpya hivi karibuni lakini kwa utafiti nilio ufanya mapokeo yake ni madogo na ya kukatisha tamaa pamoja na wimbo husika kuwa mzuri sana.
Msanii Bell 9 anakosea wapi?
Aina ya studio anayo record?
Aina ya management aliyo nayo?
Aina ya utunzi anao utumia au nyimbo anazo imba?
Amejiweka mbali na mashabiki?
Kwakuwa hana kick au scandal?
Nimejiuliza maswali mengi lakini nimekosa majibu kabisa juu ya msanii huyu Bell 9 na huwa namuonea huruma pamoja na kuonesha juhudi lakini ana puuzwa sana ....hakika kwa jinsi anavyo puuzwa huyu msanii ningekuwa ndugu yake ninge mshauri atafute shughuli nyingine ya kufanya.
Kuna nyimbo zinapata air time ya kutosha hadi una shangaa huyu Bell 9 ana shida gani?
Msanii Bell 9 amewakosea nini watanzania? ni wapi ana kosea?
Karibuni wana jamvi.
Mwl nahisi wewe humuonei huruma kabisa yani kuna siku nilimuona ana hojiwa sehemu nika sikitika sana huwa nahisi kuna kitu labda amewakosea wadau hawataki kumwambia wana muacha tuu!
Na unaweza kukuta mtu kama huyu aligombana sana na familia yake kuingia kwenye muziki na pengine hata shule ali drop na akiamini muziki utamtoa lakini mambo yamekuwa kinyume na huko wana mwambia tulikwambie wewe hukusikia...its too late..! Au atumie style ya kick au scandal atatoka?
kweliii
Tatizo kubwa la game ya muziki wa Tanzania, kuna watu fulani usipowapigia magoti na 'kuwalamba' kutoboa ni ngumu sana. Kwa sababu kuna kundi fulani ndio liliwashika hadi wadhamini wakubwa, huwezi kwenda tu let's say Tigo, Voda, TBL, SBL na makampuni mengine makubwa ya udhamini bila 'mgongo' wao. Na nikiiangalia life style ya Belle 9 hana management ya namna hiyo ndo maana jamaa wanabana kinoma. Naamini kabisa wanajua kwamba dogo yuko vizuri na akipewa nafasi anaweza kuwafunika wengi tu.
Mwisho kabisa, katika kufikia full success kwenye maisha BAHATI ina play pati kubwa mno!
Nakubaliana na wewe, belle 9 ana kipaji kizuri sana, kuna kipindi uko nyuma aliwahi kupambanishwa na diamond, ni msanii mzuri ana sauti nzuri na anajielewa.
Anachotakiwa kufanya ni kuvumilia tu, ukifika wakati wake atatusua, japokuwa inakatisha tamaa sana, maana kama kuimba kashaimba sana.
Unapotoa lawama kwa mashabiki kuwa hapokelewi vizur unakosea, kwani wimbo wake wa masogange ulifanya vzur sana na kumuweka apo alipo sasa ivi
hivi muziki haufiki sokoni bila kupitia radio?
sijui itamgharimu shiling ngapi akiamua kuwapa mshiko baadhi ya daladala ili wawe wanapiga nyimbo zake angalau wakati wa peak time.
je itagharimu pesa nyingi iwapo atazunguka kwenye majumba ya starehe na kuwakatia mshiko baadhi ya ma-dj kupiga muziki wake?
dah! labda haya ni mawazo ya sisi old-school ingawa nadhani yanaweza msaidia angalau kuzoesha masikio ya wadau.
Mmh hata kama ubuyu ulianza kama mchicha hakika kwa upande wa Bell 9 hakuwai kukua kimziki na hakuanza leo na hakuna matunda yeyote..na unaweza kukuta kuna kitu alikiacha na kuwaaminisha wanao mzunguka muziki utamtoa lakini mambo yamekwenda tofauti.
labda akajiweke kwa Lulu au Wolper..