Msanii Belle 9 amewakosea nini Watanzania? Kwanini anapuuzwa? Ni wapi anakosea?

Msanii Belle 9 amewakosea nini Watanzania? Kwanini anapuuzwa? Ni wapi anakosea?

Tatizo kubwa la game ya muziki wa Tanzania, kuna watu fulani usipowapigia magoti na 'kuwalamba' kutoboa ni ngumu sana. Kwa sababu kuna kundi fulani ndio liliwashika hadi wadhamini wakubwa, huwezi kwenda tu let's say Tigo, Voda, TBL, SBL na makampuni mengine makubwa ya udhamini bila 'mgongo' wao. Na nikiiangalia life style ya Belle 9 hana management ya namna hiyo ndo maana jamaa wanabana kinoma. Naamini kabisa wanajua kwamba dogo yuko vizuri na akipewa nafasi anaweza kuwafunika wengi tu.

Mwisho kabisa, katika kufikia full success kwenye maisha BAHATI ina play pati kubwa mno!
 
Management ni kitu muhimu sana.. pia awe karibu na fans wake kwenye social networks so that they can request his songs.....

Take my words Belle

pia atafute kiki atembee na mdafada/kishkwambi yeyote pale bongo muvi itakua amazing
 
Mbona wapo wengi tu ambao muziki wao haupigwi?
Ruttashobolwa uweke huo muziki wake hapa ili tuusikie;

Mtie moyo tu, hata ubuyu ulianza kama mchicha.

Mmh hata kama ubuyu ulianza kama mchicha hakika kwa upande wa Bell 9 hakuwai kukua kimziki na hakuanza leo na hakuna matunda yeyote..na unaweza kukuta kuna kitu alikiacha na kuwaaminisha wanao mzunguka muziki utamtoa lakini mambo yamekwenda tofauti.
 
Pamoja nakumkubali umewai kujiuliza ni wangapi wanao mkubali kama wewe huchagua nyimbo zake kwenye radio stations zichezwe? Kila mtanzani ukimuuliza utasikia ana msifu na kusema nyimbo zake ni nzuri na anazipenda lakini ukichukua wasaha wakusikiliza radio hata nusu saa huwezi kusikia nyimbo yake ikiombwa..hivi kuna nini
Hapo kwenye redio utanisamehe tu.Mimi sio msikilizaji mzuri labda itokee tu bahati mbaya.
 
Belle 9 kama matonya tu wanaimba vizuri ila ndo hivo...hadi nimehisi kuwaonea huruma

Mwl nahisi wewe humuonei huruma kabisa yani kuna siku nilimuona ana hojiwa sehemu nika sikitika sana huwa nahisi kuna kitu labda amewakosea wadau hawataki kumwambia wana muacha tuu!

Na unaweza kukuta mtu kama huyu aligombana sana na familia yake kuingia kwenye muziki na pengine hata shule ali drop na akiamini muziki utamtoa lakini mambo yamekuwa kinyume na huko wana mwambia tulikwambie wewe hukusikia...its too late..! Au atumie style ya kick au scandal atatoka?
 
kamfanya masogange kuwa maarufu zaidi kuliko yeye kwa kumtumia kama video queen.

Hakika yani Masogange kawa maarufu kumzidi..bila shaka angetoa wimbo unge hit kabisa..
 
Labda kwasababu hachukui wadada wakali macelebrities wa bongo.Huoni Nuhu Mziwanda pamoja na utahira wa ubongoni ana jina sasa kisa anamchukua shishi baby?

Hii ndiyo bongo.
Hili nalo limekua kama fashion siku hizi lakini mimi sikubaliani hata kidogo na hii mbinu ya kipuuzi.
Mbinu nzuri kufanya mziki mzuri tu na kujiweka karibu na mashabiki (kwenye social networks).Pia nidhamu kwa hawa walioshikilia soko la muziki hapa bongo.

Mbona Kiba na mavoko wanatoa miziki mizuri tunawakubali? Lini umeona wakitoka na hao macelebrity?
Hao ndio wasanii wa ukweli sasa.
 
Labda kwasababu hachukui wadada wakali macelebrities wa bongo.Huoni Nuhu Mziwanda pamoja na utahira wa ubongoni ana jina sasa kisa anamchukua shishi baby?

Hii ndiyo bongo.
Yani bado najiuliza tatizo kick na scandal? yani Nuhu kutokana na shilole alitoa wimbo uka hit na akapata show.duu!
Kuna Bar fulani nilikuwa nimekaa ulipigwa wimbo wake mpya jamaa tuliyekuwa tumekaa nae akasema huyu jamaa kwanini hapendwi? hajui kucheza na akili za watanzania? jamaa alikwenda mbali zaidi akasema jamaa anacho takiwa kwa sasa ni kutafuta scandal tuu hata kwa kubaka mbuzi maana watanzania ndio wanacho penda...daa nilicheka sana aiseee..
 
Wana jamvi wasalaam...
Wana jamvi katika adhabu ambayo anaweza kupewa mtu na ikamuumiza sana na akashindwa kujua la kufanya au suluhu ni adhabu ya kupuuzwa.

Adhabu ya kupuuzwa ndio aliyo pewa msanii Bell 9 na watanzania walio wadau wa muziki!
Bell 9 ni mmoja wa wasanii wenye sauti nzuri,mtunzi mzuri na mwimbaji mzuri lakini hakuwai kufurahia matunda ya kipaji chake kama wengine!

Bell 9 pamoja nakujua hayo yote na baadhi ya watanzania kusifu nyimbo zake lakini zimekuwa zikikosa muda wa hewani wa kutosha kama nyimbo nyingine na ni vigumu nyimbo kupata muda wa hewani kwenye radio station na Tv kama walaji hawauchagui wimbo husika!
Watanzania, Bell 9 amewakosea nini? Kwanini mna mpuuza kiasi hiki? Pamoja na msanii huyu kutoa wimbo mpya hivi karibuni lakini kwa utafiti nilio ufanya mapokeo yake ni madogo na ya kukatisha tamaa pamoja na wimbo husika kuwa mzuri sana.

Msanii Bell 9 anakosea wapi?
Aina ya studio anayo record?
Aina ya management aliyo nayo?
Aina ya utunzi anao utumia au nyimbo anazo imba?
Amejiweka mbali na mashabiki?
Kwakuwa hana kick au scandal?

Nimejiuliza maswali mengi lakini nimekosa majibu kabisa juu ya msanii huyu Bell 9 na huwa namuonea huruma pamoja na kuonesha juhudi lakini ana puuzwa sana ....hakika kwa jinsi anavyo puuzwa huyu msanii ningekuwa ndugu yake ninge mshauri atafute shughuli nyingine ya kufanya.
Kuna nyimbo zinapata air time ya kutosha hadi una shangaa huyu Bell 9 ana shida gani?

Msanii Bell 9 amewakosea nini watanzania? ni wapi ana kosea?
Karibuni wana jamvi.

Nakubaliana na wewe, belle 9 ana kipaji kizuri sana, kuna kipindi uko nyuma aliwahi kupambanishwa na diamond, ni msanii mzuri ana sauti nzuri na anajielewa.

Anachotakiwa kufanya ni kuvumilia tu, ukifika wakati wake atatusua, japokuwa inakatisha tamaa sana, maana kama kuimba kashaimba sana.

Unapotoa lawama kwa mashabiki kuwa hapokelewi vizur unakosea, kwani wimbo wake wa masogange ulifanya vzur sana na kumuweka apo alipo sasa ivi
 
Mwl nahisi wewe humuonei huruma kabisa yani kuna siku nilimuona ana hojiwa sehemu nika sikitika sana huwa nahisi kuna kitu labda amewakosea wadau hawataki kumwambia wana muacha tuu!

Na unaweza kukuta mtu kama huyu aligombana sana na familia yake kuingia kwenye muziki na pengine hata shule ali drop na akiamini muziki utamtoa lakini mambo yamekuwa kinyume na huko wana mwambia tulikwambie wewe hukusikia...its too late..! Au atumie style ya kick au scandal atatoka?

hivi muziki haufiki sokoni bila kupitia radio?
sijui itamgharimu shiling ngapi akiamua kuwapa mshiko baadhi ya daladala ili wawe wanapiga nyimbo zake angalau wakati wa peak time.
je itagharimu pesa nyingi iwapo atazunguka kwenye majumba ya starehe na kuwakatia mshiko baadhi ya ma-dj kupiga muziki wake?

dah! labda haya ni mawazo ya sisi old-school ingawa nadhani yanaweza msaidia angalau kuzoesha masikio ya wadau.
 
Tatizo kubwa la game ya muziki wa Tanzania, kuna watu fulani usipowapigia magoti na 'kuwalamba' kutoboa ni ngumu sana. Kwa sababu kuna kundi fulani ndio liliwashika hadi wadhamini wakubwa, huwezi kwenda tu let's say Tigo, Voda, TBL, SBL na makampuni mengine makubwa ya udhamini bila 'mgongo' wao. Na nikiiangalia life style ya Belle 9 hana management ya namna hiyo ndo maana jamaa wanabana kinoma. Naamini kabisa wanajua kwamba dogo yuko vizuri na akipewa nafasi anaweza kuwafunika wengi tu.

Mwisho kabisa, katika kufikia full success kwenye maisha BAHATI ina play pati kubwa mno!

Sidhani kama swala ni kuwapigia magoti labda kuwa karibu na wadau wamuziki lakini nini kina mshinda?
 
Nakubaliana na wewe, belle 9 ana kipaji kizuri sana, kuna kipindi uko nyuma aliwahi kupambanishwa na diamond, ni msanii mzuri ana sauti nzuri na anajielewa.

Anachotakiwa kufanya ni kuvumilia tu, ukifika wakati wake atatusua, japokuwa inakatisha tamaa sana, maana kama kuimba kashaimba sana.

Unapotoa lawama kwa mashabiki kuwa hapokelewi vizur unakosea, kwani wimbo wake wa masogange ulifanya vzur sana na kumuweka apo alipo sasa ivi

Kama ni swala la kusubiri nafikiri amesha subiri sana.. kuna watu wametoka wanamuacha kila leo! Nuhu mziwanda alitoa wimbo ukapokelewa vyema lakini yeye vipi? Nawapa lawama mashabiki kwakuwa wao ndio wachaguzi wa nyimbo kila leo! labda uniambie tatizo ni nini? lakini kwa swala la kusema aendelee kusubiri ni kumdanganya.
 
hivi muziki haufiki sokoni bila kupitia radio?
sijui itamgharimu shiling ngapi akiamua kuwapa mshiko baadhi ya daladala ili wawe wanapiga nyimbo zake angalau wakati wa peak time.
je itagharimu pesa nyingi iwapo atazunguka kwenye majumba ya starehe na kuwakatia mshiko baadhi ya ma-dj kupiga muziki wake?

dah! labda haya ni mawazo ya sisi old-school ingawa nadhani yanaweza msaidia angalau kuzoesha masikio ya wadau.

Pengine hili linaweza kumsaidia kidogo maana sio jinsi labda ajaribu hilo!
 
Msaidie ili atoke,
Mfanyie promo kwenye vyombo vya habari;

Mmh hata kama ubuyu ulianza kama mchicha hakika kwa upande wa Bell 9 hakuwai kukua kimziki na hakuanza leo na hakuna matunda yeyote..na unaweza kukuta kuna kitu alikiacha na kuwaaminisha wanao mzunguka muziki utamtoa lakini mambo yamekwenda tofauti.
 
Mi mwenyewe namkubali ila inafikia kipindi huwa namsahau kabisa coz nyimbo zake siziskii redion always.ajaribu kuchange either management or style ya kupenyeza mziki wake .ni nyimbo kali but kama watu hawazikii mpaka wazitafute nadhani watu watabakia walewale.namtakia mafanikio zaid sokoni
 
Back
Top Bottom