Msanii Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya

Adhabu ibadilishwe iwe kifo au kifungo cha maisha
 
Wampe kifungo cha mwaka mmoja jela,akitoka atakuwa ameshasahau hayo madawa
 
Wanatafuta ushaidi,Hapo siasa itakuwa imeshaingia
 
Huyo mtu ni janga kwa familia na taifa kwa ujumla,ukichukulia kuwa yeye ni kioo cha jamii.
 
Ndiyo maana, China wanawapa zawadi ya bomba kumbe wao wanaelewa kabisa kuwa hawa jamaa huwa hawaachi hii kazi.

An way, RIP wote waliouliwa kwa dawa hizo, na pole sana kwa wote wanaotesaka kwa sababu ya hizi mambo za hawa punda.
 
Sijui ni kwa nini watu wengi hawakupenda ile kasi ya Mheshimiwa Makonda ambayo kwa upande wangu ilitoa picha halisi juu ya kiwango cha biashara hii haramu ya madawa ya kulevya na ukubwa wa madhara kwa nguvu kazi ya taifa hili! Sijui!!!
Ila ninachofahamu, ni juu ya jinsi gani jamii inavyoweza kuondolewa kwenye hoja za msingi kwa kuelekezwa kujadili watu!
Mbali na huyu kijana Chid Benz, ambaye nyota yake inaonesha kutoweka, kunao wengi ambao tunawaona kwa dhahiri wanavyoangamia kwa sababu tu hatukutaka kumuunga mkono Makonda ambaye ni mkuu wa mkoa ambao ni lango kuu la kuingizia madawa haya nchini.
Tujutafakari!
 
Sasa hata sielewi tena hii issue ya madawa. Nilidhani imekwisha hasa baada ya zile jitihada za Makonda na Mh. Raisi. Kumbe mambo yapo hadharani kama kawa.... Sasa inamaana zile jitihata zimefeli?
 
Unaweza kuwa na tatizo dogo lakini vile unalitatua lisikupe matokeo chanya au matokeo ya kuonekanika.Roho ii radhi lakini mwili u dhaifu. Kuna vitu vingine wakuna nafsi ndo inayougua sasa ukimpeleka magereza sana sana utamzika huyu mtu. Kuitibu nafsi lazima ujue alianzaje kuna stori ndefu. Kati ya haya mawili hakuna mwenye nia ya dhati ya kumsaidia huyu kijana au wote wanaojaribu kumsaidia hawajui jinsi ya kumsaidia.
 
Chidi kwa imani yangu kinachoumwa ni spirit being, nafsi yake iko mateka iko kifungoni ni spiritual zaidi, ukimfungia hata ufanye nini atarudia kwa sababu kinachomshikilia bado hakijaachia. Kama alivyosema Mshana jr vitu vingi vinaanzia ulimwengu wa roho ndo tunapata matokeo ulimwengu wa nyama na damu. Binadamu tunavitu viwili , tuna nafsi(roho) na mwili. Chakufanya kwanza ayakatae matendo ya mwili yaliyoleta madhara ya nafsi yake baada ya hapo kuingia kiroho kupambana ili nafsi yake iachiliwe ndipo tutaona matokeo chanya. Hakuna jambo linalomshinda Mungu. Tuliambiwa msinililie mimi zililieni nafsi zenu .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…