Msanii DJ Choka anavyo thibitisha kwa vitendo mantiki ya Making Kayumba Schools Great Again ( Makaga campaign) ya Likud

Msanii DJ Choka anavyo thibitisha kwa vitendo mantiki ya Making Kayumba Schools Great Again ( Makaga campaign) ya Likud

DJ Choka, ambaye ni mmoja wa ma-DJ wa zamani na nguli katika historia ya muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, anaandika;

"NAOMBENI MNIPE USHAURI KWENYE HILI LEO

1. Kwenye MFUKO wangu nina AKIBA ya Shillings LAKI TATU (300,000/=) ambayo niliiweka kwaajili ya kuitumia kesho Sept 14 kwenye DIALYSIS.

2. Mtoto wangu anafungua SHULE leo Sept 13 yupo BOARDING na kesho anatakiwa aendelee na masomo yake na anatakiwa aende na Risiti ya BANK ya malipo yakumalizia muhula huu wa mwisho wa masomo ambayo natakiwa kulipia LAKI SABA (700,000/=)

HAYA NDUGU ZANGU MNANISHAURIJE KWENYE HILI SWALA LANGU, Je mtoto asiende Shule asikilizie nyumbani mpaka nipate hiyo school fees ambayo sijui nitaipata lini kwa maana kila salio nalolitafuta linaishia kwenye DIALYSIS.

Au hii laki tatu niliyonayo ya dialysis ndio nikalipie kama kianzio akubaliwe kurudi kuendelea na masomo yake huku nikiitafuta hela nyingine ya dialysis.

NASOMA COMMENTS ZENU LABDA NITAPATA JIBU".

..............

DJ Choka anawakilisha maelfu ya wazazi wa kitanzania ambao wanao jistress kulipa mamilioni kwenye shule za EMS .

Haya sasa twende kazi........View attachment 3669922
Dj Choka kachoka huwezi mtumie kwenye sampling yako.
 
Hiyo inaitwa kufake life
Nipiganie malengo yangu unaniambia nafake life
Watu wote waliofanikiwa walikuwa na ambitious kubwa ambayo ilipelekea kufanya kazi kwa bidii

Ndo maana wazungu walikuwa na makoloni kila kona ya dunia ilihali europe ni kibara kidogo sana na hakina rasilimali

Tofautisha mimi kupigania malengo yangu kwa siri na kwa nguvu zote na kufanya show off hivi ni vitu viwili tofauti
 
Usipende kuishi kwenye comfort zone akili italala
Kuwa na malengo makubwa ili akili ichangamke

Ukae ukijua mimi sio moja ya wajinga unaowafahamu.

Malengo makubwa ni tofauti kabisa na matumizi yaliyonje ya uwezo wako ambayo matokeo yake hayatakuwa na faida.

Uwezo wako 500k
Unapeleka shule ya 2M
Hayo sio malengo. Ni ujinga.

Maisha ni kuishi sasa bila kuharibu kesho.
Na kuweka malengo ya kesho yasiyoharibu sasa.

Ishi ndani ya mipaka yako
 
Nionyeshe sehemu nimekuita ni mjinga kabla sijaendelea

Nimekuambia ukweli umeumia sasa unanzushia mambo ya uongo nionyeshe hiyo sehemu niliyokuita ni mjinga
 
Nionyeshe sehemu nimekuita ni mjinga kabla sijaendelea

Nimekuambia ukweli umeumia sasa unanzushia mambo ya uongo nionyeshe hiyo sehemu niliyokuita ni mjinga

😀😆
Labda ulichoandika hukukielewa.
Kasome comment yako then urudi hapa.

Akili italala.
Akili ichangamke huku ukihusisha na Malengo makubwa.
Kwamba kipi hukielewi?
 
😀😆
Labda ulichoandika hukukielewa.
Kasome comment yako then urudi hapa.

Akili italala.
Akili ichangamke huku ukihusisha na Malengo makubwa.
Kwamba kipi hukielewi?
Ukweli ni kwamba ili ufanikiwe lazima uwe na malengo makubwa zaidi ya kipato chako na ambitious kubwa ndo utafanikiwa

Akili inafanya kazi ikiwa under-pressure na sio tofauti na hapo

Lazima uwe mtu wa kuforce
Lakini sikushangai watanzania wengi tunapenda kurithika
 
Kusomesha mtoto shule za gharama kubwa nje ya kipato chako sio malengo makubwa. Ni ufinyu wa uelewa na mambo ya elimu ya fedha.

Unapomsomesha shule ya 2M alafu uwezo wako ni 500K embu eleza unataka ufanikishe nini kwenye huo mkakati?
 
Moja ya ujinga na ulimbukeni walionao watu ni kupeleka watoto shule za binafsi huku wakijijua uwezo wao ni mdogo.
Sio ujinga wewe huna hela tulia,Mfano ilishawahi kukutana na mtoto wa GSM au King Msukuma anasoma Buguruni sekondary? Hebu punguza ujinga shule za English medium pia ada yao inategemeana kwa maana kuna za hadhi ya juu na zingine za kawaida.
 
😆😀😀

Kwani GSM na Msukuma watoto wao ni kina nani? Wanatofauti gani na watoto wako?

Sisi Watibeli tutazidi kuwa mbele na bora kwenu mpaka mtakapokuwa na Akili.

So wewe unapeleka mtoto English Medium kwa sababu GSM anapeleka?
Kwako GSM ni mtu mkubwa na wamaana sana eeg?
 
Nionyeshe sehemu nimekuita ni mjinga kabla sijaendelea

Nimekuambia ukweli umeumia sasa unanzushia mambo ya uongo nionyeshe hiyo sehemu niliyokuita ni mjinga
Achana naye ukute hapo alipo ni mlevi na malaya haoni hizo gharama anatumia kulewa na kuhonga. Hakuna kitu unapata kwa wepesi.

Mtu ananunua gari kwa kujibana na anapambana kufanya kazi kwa bidii ili afford gharama za maisha.

Hawa ndo wale wanasema siwezi kupanga nyumba nzuri ina gharama bora nikakae mabondeni kwenye kodi ndogo ila utashangaa miaka nenda rudi hawana maisha na wanatembea kwa mguu tu.
 
Kusomesha mtoto shule za gharama kubwa nje ya kipato chako sio malengo makubwa. Ni ufinyu wa uelewa na mambo ya elimu ya fedha.

Unapomsomesha shule ya 2M alafu uwezo wako ni 500K embu eleza unataka ufanikishe nini kwenye huo mkakati?
Kusomesha mtoto shule za gharama ni malengo na uwekezaji
Unafikiri mimi nayemsomesha mtoto IST au breburn na wewe unayemsomesha kayumba watakuwa sawa

Huyu wa kwangu IST classmate wake tu wanatosha kumpa connection za maisha sababu wazazi wao ni matajiri na wanamiliki viwanda

Wewe wa kwako wa kayumba clasmate wake wazazi wao ni wamachinga, mama ntilie, walimu, wafanyakazi wa serikali wewe unafikiri watakuwa sawa hawa huko baadae
Akimaliza akifeli au akikosa kazi baada ya kumaliza masomo anakuwa bodaboda, winger, au mmachinga ndo option inayomsubiria sababu hata uwezo wa kumpa mtaji wa maana huna

Mimi nilikuwa nafanya kazi sehemu flani miaka ya nyuma kuna mfanyakazi alikuwa analipwa laki 8 ila kapanga nyumba ya million watu walimuona mjinga ila kwa malengo jamaa aliyokuwa nayo alikuwa ni mpiganaji na anaforce vibaya mno sahivi jamaa yuko mbali sana sababu ya akili yake ya kuforce waliokuwa wanamsema wako vilevile sana sana wameimprove kidogo sana

Maisha yako ni uchaguzi wako
 
Achana naye ukute hapo alipo ni mlevi na malaya haoni hizo gharama anatumia kulewa na kuhonga. Hakuna kitu unapata kwa wepesi.

Mtu ananunua gari kwa kujibana na anapambana kufanya kazi kwa bidii ili afford gharama za maisha.

Hawa ndo wale wanasema siwezi kupanga nyumba nzuri ina gharama bora nikakae mabondeni kwenye kodi ndogo ila utashangaa miaka nenda rudi hawana maisha na wanatembea kwa mguu tu.
Wengi wetu tunamani mafanikio ila hatutaki kuyapigania kwa sababu yana gharama sisi tunataka mafanikio yaje kama fluke

Mimi nilikuwa nafanya kazi sehemu flani miaka ya nyuma kuna mfanyakazi alikuwa analipwa laki 8 ila kapanga nyumba ya million watu walimuona mjinga ila kwa malengo jamaa aliyokuwa nayo ilibidi apigane alikuwa ni mpiganaji sana na anaforce vibaya mno sahivi jamaa yuko mbali sana sana sio kodogo sababu ya akili yake ya kuforce malengo makubwa aliokuwa nayo
waliokuwa wanamsema wako vilevile sana sana wameimprove kidogo sana
 
Back
Top Bottom