Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Kusomesha mtoto shule za gharama ni malengo na uwekezaji
Unafikiri mimi nayemsomesha mtoto IST au breburn na wewe unayemsomesha kayumba watakuwa sawa
Huyu wa kwangu IST classmate wake tu wanatosha kumpa connection za maisha sababu wazazi wao ni matajiri na wanamiliki viwanda
Wewe wa kwako wa kayumba clasmate wake wazazi wao ni wamachinga, mama ntilie, walimu, wafanyakazi wa serikali wewe unafikiri watakuwa sawa hawa huko baadae
Akimaliza akifeli au akikosa kazi baada ya kumaliza masomo anakuwa bodaboda, winger, au mmachinga ndo option inayomsubiria sababu hata uwezo wa kumpa mtaji wa maana huna
Mimi nilikuwa nafanya kazi sehemu flani miaka ya nyuma kuna mfanyakazi alikuwa analipwa laki 8 ila kapanga nyumba ya million watu walimuona mjinga ila kwa malengo jamaa aliyokuwa nayo alikuwa ni mpiganaji na anaforce vibaya mno sahivi jamaa yuko mbali sana sababu ya akili yake ya kuforce waliokuwa wanamsema wako vilevile sana sana wameimprove kidogo sana
Maisha yako ni uchaguzi wako
Unafurahisha sana.
Kwamba usomeshe mtoto Shule za gharama ili kununua Connections?😀😀😀🫢
Mimi sijasoma hizo shule za international school lakini mbona Nina Connections nzuri tuu inayonitosha?
Kina Diamond, Mwakinyo, Lisu, Samia, na watu wote unaowajua unafikiri Connections walizo nazo zinatokana na kusoma international?
Connections inajengwa na tija na mchango wako kwenye jamii au mazingira uliopo.
Kama huna tija au mchango wowote hakuna atakayetaka ukaribu na wewe.
Mtu anaangalia nitapata nini kwako. Kisha nawe utapata nini kwake.
Sasa unasomesha mtoto international alafu hana tija yoyote hiyo Connection anapataje?
Wekeza kwenye ujuzi wa mtoto. Mtoto awe mbobevu kupita kiasi katika jambo fulani. Connections ni uhakika.
Kama ni gitaa apige gitaa kwa kiwango cha juu. Wakubwa watamuita.
Ni sawa useme unaenda Hotel ya nyota 5 au kanisa au msikiti wanaosalia washua ili upate Connections. Ni ujinga mtupu.