Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Kusomesha mtoto shule za gharama ni malengo na uwekezaji
Unafikiri mimi nayemsomesha mtoto IST au breburn na wewe unayemsomesha kayumba watakuwa sawa
Huyu wa kwangu IST classmate wake tu wanatosha kumpa connection za maisha sababu wazazi wao ni matajiri na wanamiliki viwanda
Wewe wa kwako wa kayumba clasmate wake wazazi wao ni wamachinga, mama ntilie, walimu, wafanyakazi wa serikali wewe unafikiri watakuwa sawa hawa huko baadae
Akimaliza akifeli au akikosa kazi baada ya kumaliza masomo anakuwa bodaboda, winger, au mmachinga ndo option inayomsubiria sababu hata uwezo wa kumpa mtaji wa maana huna
Mimi nilikuwa nafanya kazi sehemu flani miaka ya nyuma kuna mfanyakazi alikuwa analipwa laki 8 ila kapanga nyumba ya million watu walimuona mjinga ila kwa malengo jamaa aliyokuwa nayo alikuwa ni mpiganaji na anaforce vibaya mno sahivi jamaa yuko mbali sana sababu ya akili yake ya kuforce waliokuwa wanamsema wako vilevile sana sana wameimprove kidogo sana
Maisha yako ni uchaguzi wako
Kuna watu wanavipaji vikubwa na wanakufaa njaa nenda uko uswahilini uoneUnafurahisha sana.
Kwamba usomeshe mtoto Shule za gharama ili kununua Connections?😀😀😀🫢
Mimi sijasoma hizo shule za international school lakini mbona Nina Connections nzuri tuu inayonitosha?
Kina Diamond, Mwakinyo, Lisu, Samia, na watu wote unaowajua unafikiri Connections walizo nazo zinatokana na kusoma international?
Connections inajengwa na tija na mchango wako kwenye jamii au mazingira uliopo.
Kama huna tija au mchango wowote hakuna atakayetaka ukaribu na wewe.
Mtu anaangalia nitapata nini kwako. Kisha nawe utapata nini kwake.
Sasa unasomesha mtoto international alafu hana tija yoyote hiyo Connection anapataje?
Wekeza kwenye ujuzi wa mtoto. Mtoto awe mbobevu kupita kiasi katika jambo fulani. Connections ni uhakika.
Kama ni gitaa apige gitaa kwa kiwango cha juu. Wakubwa watamuita.
Ni sawa useme unaenda Hotel ya nyota 5 au kanisa au msikiti wanaosalia washua ili upate Connections. Ni ujinga mtupu.
Sio ujinga wewe huna hela tulia,Mfano ilishawahi kukutana na mtoto wa GSM au King Msukuma anasoma Buguruni sekondary? Hebu punguza ujinga shule za English medium pia ada yao inategemeana kwa maana kuna za hadhi ya juu na zingine za kawaida.
Kuna watu wanavipaji vikubwa na wanakufaa njaa nenda uko uswahilini uone
Tatizo unapenda sana kuongelea story za kufikirisha
Ukitembelea Nyumba tatu moja wapo utakuta watoto wenye degree ila kuna watu wengi wenye degree na wanaendesha bodaboda ujuzi wanao hawana kazi
Sema watanzania wako gizan sana ndo maana nchi iko hivi kama ilivyo mtuDegree sio ujuzi. Bali ni theory tu.
Harmonize, nandy wala diamond hawana degree ya music ila wanaujua mziki kuliko graduate wa udsm mwenye degree ya music.
Hivyo connections wanazipata wenye ujuzi ila sio wenye degree
Kabisa,huyu bwana alilaumu watu miaka mitano au sita iliyopita kisa hawakuonekana kumjali alipokutwa na TB!! Nilimshangaa sana!!
Kwa huyo hao akina Diamond wamefanikiwa kuliko waliopitia shule? Wewe unawajua Mainjinia wanamakamouni Makubwa ya ujenzi mfano kampuni ya Derm mwenye Derm tower Makumbusho inahusika na nguzo za zege nchi nzima unalinganishaje mafanikio ya Eng Mrigo na hao waimba nyimbo wako?Degree sio ujuzi. Bali ni theory tu.
Harmonize, nandy wala diamond hawana degree ya music ila wanaujua mziki kuliko graduate wa udsm mwenye degree ya music.
Hivyo connections wanazipata wenye ujuzi ila sio wenye degree
Dudubaya alikosa bahati ya kuwa na famili bora kuna muda namuona kama angebahatika kutumia muda na familia yake angekuwa mbali ila ndo tunayosema hapa mtoto unamwacha anasoma Mbagala sekondari anakutana na watoto wasio na maadili anapotea lakini kuna uwezekano angejinyima akasomesha watoto shule nzuri mambo yangekuwa tofauti.Dudubaya kampa laki 5 huyu Cash juzi tu.
Angeongeza na hiyo 3 angeshalipa Ada hiyo.
Kanywea pombe
Issue za Figo zisikie kwa JIRANI huko acha bwana.DJ Choka, ambaye ni mmoja wa ma-DJ wa zamani na nguli katika historia ya muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, anaandika;
"NAOMBENI MNIPE USHAURI KWENYE HILI LEO
1. Kwenye MFUKO wangu nina AKIBA ya Shillings LAKI TATU (300,000/=) ambayo niliiweka kwaajili ya kuitumia kesho Sept 14 kwenye DIALYSIS.
2. Mtoto wangu anafungua SHULE leo Sept 13 yupo BOARDING na kesho anatakiwa aendelee na masomo yake na anatakiwa aende na Risiti ya BANK ya malipo yakumalizia muhula huu wa mwisho wa masomo ambayo natakiwa kulipia LAKI SABA (700,000/=)
HAYA NDUGU ZANGU MNANISHAURIJE KWENYE HILI SWALA LANGU, Je mtoto asiende Shule asikilizie nyumbani mpaka nipate hiyo school fees ambayo sijui nitaipata lini kwa maana kila salio nalolitafuta linaishia kwenye DIALYSIS.
Au hii laki tatu niliyonayo ya dialysis ndio nikalipie kama kianzio akubaliwe kurudi kuendelea na masomo yake huku nikiitafuta hela nyingine ya dialysis.
NASOMA COMMENTS ZENU LABDA NITAPATA JIBU".
..............
DJ Choka anawakilisha maelfu ya wazazi wa kitanzania ambao wanao jistress kulipa mamilioni kwenye shule za EMS .
Haya sasa twende kazi........View attachment 3669922
Nimesikitika sana mic kwetu wanywa pombeDudubaya alikosa bahati ya kuwa na famili bora kuna muda namuona kama angebahatika kutumia muda na familia yake angekuwa mbali ila ndo tunayosema hapa mtoto unamwacha anasoma Mbagala sekondari anakutana na watoto wasio na maadili anapotea lakini kuna uwezekano angejinyima akasomesha watoto shule nzuri mambo yangekuwa tofauti.
Huyo akipata laki tano anaenda kushinda bar na washikaji wanazisaga hela zote. Anyway kila mtu na maisha yake.
Ukweli mchungu.Shule zenyewe za ESM nyigi ni vituko na hazina walimu wenye weledi wa kuongea kiingereza. ukisikiliza watoto wanavyoongea english utacheka uvunjike mbavu, wanaongea kiingereza kibovu wanachofundishwa na walimu wao. shule zilianzishwa kibiashara tu na si kihuduma. Zilianzishwa kwa kufuata mkumbo kwa kuwa soko huria linaruhusu basi kila mwenye mtaji anaanzisha shule kwa lengo la kibiashara
Umekurupuka na kujitungia swali lako kisha unajijibu mwenyewe unataka kuhamisha hoja.Kwa huyo hao akina Diamond wamefanikiwa kuliko waliopitia shule? Wewe unawajua Mainjinia wanamakamouni Makubwa ya ujenzi mfano kampuni ya Derm mwenye Derm tower Makumbusho inahusika na nguzo za zege nchi nzima unalinganishaje mafanikio ya Eng Mrigo na hao waimba nyimbo wako?
Kuna Qwihaya Enterprise inamagari zaidi na 500 anachimba makaa ya mawe huku kusini na anazalisha nguzo za umeme nchi nzima ni msomi na mjasiliamali unaweza kumlinganisha na Diamond?
Acha ujinga wa kudharau elimu kama wewe hujafanikiwa kwa kutumia elimu kaa kimya.
Wewe acha lengo lako ni kubagaza elimu ila mimi nakwambia familia nyingi zenye mafanikio hasa kwa Watanzania weusi zimesomesha watoto vizuri.Umekurupuka na kujitungia swali lako kisha unajijibu mwenyewe unataka kuhamisha hoja.
Degree ya muziki wapi na wapi na enginer?
Mfano wa diamond umetajwa kwenye muziki, wapi mfano huo umemtaja engineer ??
Kasome tena vizuri kisha ndio uje hapa