Msanii gani ambaye ulitokea kumkubali/ulipenda nyimbo zake lakini ALIPOTEA na unatamani arudi kwenye game

Mo Music hiyo ngoma yake huwa inanikumbusha ex wangu. Fala sana yule, nilikutwa naimba huo wimbo wakati tuna mgogoro. Nikaambiwa namuimbia yeye, kibuti cha bw misosi kikanipitia
 
1)Abby skillz
2)Enika
3)Berry black
4)damian soul
5)rama dee
6) qjay
7)mack D
8)dogo ditto & mc koba
9)norah
10)mr blue
Rama dee kipaji sana yule mwamba,,, kwenye rnb hakuna kama yeye,,,alioa mzungu akaenda ughaibuni na mambo muziki yakaanza kupungua taratibu
 
Sio kwamba ana hardware kahama? Au me ndo nimechanganya?
Sijajua kama kabadili biashara saa hzi ila alikuwa anauza duka la spear,,,alikuwa karibu na mama yake pia alikuwa anaduka mtaa huo huo
 
Nakaya, Domo Kaya, Mr. Yebo,
Daaah nakaaya mr politician ilibamba sana sio mchezo,,nakaaya alikuwa chadema baada ya mda akasaliti chama akaenda ccm akagombea ubunge,wajumbe sio watu wazuri walimchinjilia mbali mpaka leo yupo kimya sana
 
Mo Music hiyo ngoma yake huwa inanikumbusha ex wangu. Fala sana yule, nilikutwa naimba huo wimbo wakati tuna mgogoro. Nikaambiwa namuimbia yeye, kibuti cha bw misosi kikanipitia
Hahaha[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Only MAN GWAIR
She got a gwa
mikasi
 
1. Young Dee

Enzi anaimba Kijukuu, Ticha etc lakini alivyoanza kua ukaribu na hawa vijana wa 26 namba, kwisha.

2. Jaji Hakim

Huyu aliimba Ninavyofanya. Aliimba vizuri sana lakini hajawahi kutoa tena wimbo.

3. Yakhi

Tonigh. Dah Hiki kipajincha Iringa ilikua noma na nusu.

4. Daz Nundaz

Hawa hawajawahi kukosea. Nilikununua hadi album yao aisee. Pini zote kali.

5. Jay Moe & Mwana FA

Wale wa zamani sio hawa wa sasa siwaelewi. Moe Tec na Falsafa walikua na unadishi flani amazing.

6. Dullayo

Nimeumia sana kuona uzi juzi Dullayo kawa mlevi aisee niliumia saaana.
 
Daaah dulayo inauma sana aise,,,,alituburudisha sana enzi hizo na 'naumia roho' n.k
 
Hivi pig black yuko wapi!

Sura yake hadi leo siijui ila alikuwa na sauti ya ajabu.ile ngoma yske ya "nini mnataka mazee" ilibamba sana.Majani ile beat ya hii ngoma alipigwa scratch za kibabe sana.daah noma

Halafu Big dog Pose nao wako wapi.Wazee wa "kumwambia na kumwimbia" daah

Old is gold
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…