Msanii gani ambaye ulitokea kumkubali/ulipenda nyimbo zake lakini ALIPOTEA na unatamani arudi kwenye game

Msanii gani ambaye ulitokea kumkubali/ulipenda nyimbo zake lakini ALIPOTEA na unatamani arudi kwenye game

Tuvumiliane tulipotoka ni mbali, sahau yote yaliyopita..
Caz T naona hamumtaji.
 
Joselin
TiD
Baraka da Prince
Lady jay dee wa zamani, huyu wa sasa sjui anaimba vitu gani
Wakali kwanza + Enika
 
TID ,RAY C, Lady jaydee, Saida karoli, hawa walifanya enzi za utoto wangu nifurahie sana , nikiiskiliza nyimbo ya Zeze nakumbuka mara ya kwanza kuoona kwenye Tv nilikua natoka kuogeshwa na shangazi.
Nikikumbuka nyimbo ya "Mapenzi matamuu niwapo nawe mpenzi" nakumbua ndoa ya baba yangu mdogo iliingizwa kwenye video ya ndoa yao niliiona nikiwa mtoto enzi hizo

Nikikumbuka nyimbo ya "chambua Kama karaga" namkumbuka Samira nilicheza nae kibaba na mama, nikikumbuka "Siwemaa usinipe mateso ya moyooo" namkumbuka jackline shule ya msingi nilimpenda Ila sikuwahi kumwambia hadi leo sijui Yuko wapi
 
Kwa upande wangu kuna hawa jamaa yani wanasauti nzuri sana tena huenda kuzidi baadhi ya msanii wanao sumbua kwasasa

[emoji2389] Mb dog
Huyu jamaa alisumbua sana miaka ya 2005 na kidogo,,anasauti nzuri sana alipeta na vibao vyake kama latifa,si ulinambi, mapenzi kitu gani na vingne vingi ,,anavocal nzuri sana sijui saa hizi yuko wapi,,natamani sana arudi kwenye game najua kiti chake bado kipo atakifuta vumbi tu

[emoji2390] Z anto
Huyu jamaa nae alitikisa sana enzi hizo na vibao vyake kama mpenzi jini,binti kiziwi,, na vingne lakini alipotea kwenye game gafla inasemekana alichanganya mapenzi na kazi lakini napenda nimuone sikuona akirudi Kwenye game

[emoji2391] Mo music
Huyu kijana alikuwa ni kinda ambae anakuja vizuri sana na vibao vyake kama basi nenda,n.k mara gafla akapotea kwenye game sijui shida nini na sijui yuko wapi ila natamani nimuone siku moja anarudi kwenye game naamini bado ananafasi yake inamsubiri

[emoji2393] Neyba
Huyu jamaa alikuwa ni chorus killer ukimshirikisha kwenye wimbo wako anaunogesha lazima utapendwa tu sijui yuko wapi, sijui anafanya nini natamani nimuone siku moja tena kwenye game

Nawe ongezea wako,unaowatamani warudi tena kwenye game ya muzidi wa bongo fleva
[emoji2394]

[emoji2395]

[emoji2396]

[emoji2397]

[emoji647]
Hivi momba mzee wa mdundiko yuko wapi
 
TID ,RAY C, Lady jaydee, Saida karoli, hawa walifanya enzi za utoto wangu nifurahie sana , nikiiskiliza nyimbo ya Zeze nakumbuka mara ya kwanza kuoona kwenye Tv nilikua natoka kuogeshwa na shangazi.
Nikikumbuka nyimbo ya "Mapenzi matamuu niwapo nawe mpenzi" nakumbua ndoa ya baba yangu mdogo iliingizwa kwenye video ya ndoa yao niliiona nikiwa mtoto enzi hizo

Nikikumbuka nyimbo ya "chambua Kama karaga" namkumbuka Samira nilicheza nae kibaba na mama, nikikumbuka "Siwemaa usinipe mateso ya moyooo" namkumbuka jackline shule ya msingi nilimpenda Ila sikuwahi kumwambia hadi leo sijui Yuko wapi
Anhaaa Lucha
 
captain Jacob Kindole AKA Roho Saba dah jamaa alkua anajua sana sema jeshi limempenda zaidi

Mwingine Gwamaka Kahiula AKA King Crazy GK dah Kigugumiz styl
 
captain Jacob Kindole AKA Roho Saba dah jamaa alkua anajua sana sema jeshi limempenda zaidi

Mwingine Gwamaka Kahiula AKA King Crazy GK dah Kigugumiz styl
FEROOZ , Huyu mnyama ni hatateee ,,atafutwe asaidiwe please ,,,
 
Back
Top Bottom