Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Nakumbuka kwangu enzi nipo Arusha miaka ya 2016 , Nlikuwa na kawaida ya kwenda club D maeneo ya Moshono.

Siku ya siku wakaja kina Mr Blue na Rommy Jons ambae alipewa u DJ.

Cha ajabu hatukuwa wengi sana, hatukufika hata 30,

Basi ikawa Mr Blue ananipa mic sana tu niwe nafuatiliza nyimbo zake maana nilikuwa nimezikariri nyingi.

Ilikuwa poa sana ile siku kwangu, Jamaa yupo peace hana makuu
Nimepiga sana story na Best nasso
Tuliongea machache.
Ila na Saida karoli.
Tulibonga tukaweka na photo moja japo kwa bei.
 
Huyu hapa
FB_IMG_1609358774311.jpeg
 
Mie nakutana sana na mchekeshaji Mkwere ninajenga Kimara (nyumba ya kupangisha) jirani na kwake. Uwa tunapiga sana story . Prof. J pia mshikaji tunaongea nae, Afande Sele mwanangu mno na kuna msanii mmoja wa kike maarufu nilishapita nae kinyumba enzi zangu
JD
 
diamond platnumz maeno ya sinza vatcan..alipokua anataka kuwapangishia dancers wake..hiyo nyumba alokua anaitaka..ipo jirani na ninapoishi.. jamaa anaongea haraka haraka mno[emoji23][emoji23]

pia bwana Juma Mchopanga (JAY MOE) ni jirani yangu..huwa tunapiga sana stori kijiweni kwa mkenya[emoji28][emoji28]
Mkenya muuza rangi za magari?
 
Nakumbuka kwangu enzi nipo Arusha miaka ya 2016 , Nlikuwa na kawaida ya kwenda club D maeneo ya Moshono.

Siku ya siku wakaja kina Mr Blue na Rommy Jons ambae alipewa u DJ.

Cha ajabu hatukuwa wengi sana, hatukufika hata 30,

Basi ikawa Mr Blue ananipa mic sana tu niwe nafuatiliza nyimbo zake maana nilikuwa nimezikariri nyingi.

Ilikuwa poa sana ile siku kwangu, Jamaa yupo peace hana makuu
lil wayne nilikuatana naye new orleans, louisiana pale kuna uwanja fulani wa mecedes benz superdome ,,ila nilimpa hai tuu akaitikia na kisauti chake cha kiteja
 
STORY 1
Ilikua mwaka 2018 stamina shorobwenzi alikua ana mchepuko sehemu nilipopanga mimi. Siku nimekaa kibarazani naona imekuja toyota crown mara bidada huyo anatoka ndani anaingia kwenye ile gari ila kwa mbali nilimuona Stamina ila sikuamini hivyo sikutilia maanani.

Siku ilofuata mishale ya saa moja jamaa huyo na ndiga yake anakuja kumchukua bidada mara akakwama kwenye matope. Ndo bidada kuja kuomba msaada tukasukume gali ndo kumuona stamina basi tukamsaidia gari lilivotoka jamaa akaweka pembeni tukapiga story sana akatuhadithia historia ya maisha yake mpaka kutoka kimuziki. Pia namna alivotengeneza ukaribu na Roma. Akamchukua bidada wakasepa.

STORY 2
Nilikua kwenye mishe zangu za kila siku sina hili wala lile mishale ya saa nane mchana simu yangu iliita baada ya kuitizama niligundua ni brother anaefanya kazi karibu na ofisi yetu ndo alikua akinipigia. Nilipokea akanipa maelekezo kwamba kuna mwanadada anatokea Mbeya utampokea kisha utamuonesha magari ya kwenda Songea nikamkubalia kisha baada kama ya saa mwanadada akapiga kunipa maelekezo kua keshafika nimfuate alipo.

Basi nikaazima boda ya mtu wangu wa karibu nikaenda mpaka yule dada alipo ila nilishikwa na butwaa kidogo nikijisemea moyoni mbona huyu dada namfahamu. Basi nikagundua ni msanii Chemical muimbaji wa miondoko ya HIP HOP. Basi nikambeba mpaka ofisini kwetu kwakua aliomba apumzike kabla hajaendelea na safari. Nikapiga nae sana story then nkampeleka stand akakwea Gari huyo akasepa.

HIZI KUMBUKUMBU KWANGU HUA ZINANIFARIJI NIKIZIKUMBUKA.
 
Msanii wa bongo au? Labda awe wa Hollywood kwa hapa sitaki kuambukizwa zero brain
 
Mboso ..tangu hajawa star Hadi sasa tukikutana maeneo ya kwao akija kutembea na Mimi nikiwa maeneo hayo salamu za hapa na pale..yupo poa Sana

Godzila (r.i.p)..enzi hizo naishi mbezibeach tulikuwa tunakutana mida ya jioni pale belinda kwa story za hapa na pale na marafiki zangu

Dullyskyes..kwa mara ya Kwanza tulikutana yahya boutique kino..mazoea yakaanzia hapo jamaa yupo straight hapindishi ukizingua

Nitarudi
Afu wewe ngoja nicheke[emoji28][emoji23][emoji23]

Mod wamekufanya nini
 
Back
Top Bottom