Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Nimepiga sana story na Best nasso
Tuliongea machache.
Ila na Saida karoli.
Tulibonga tukaweka na photo moja japo kwa bei.
 
JD
 
Mkenya muuza rangi za magari?
 
lil wayne nilikuatana naye new orleans, louisiana pale kuna uwanja fulani wa mecedes benz superdome ,,ila nilimpa hai tuu akaitikia na kisauti chake cha kiteja
 
STORY 1
Ilikua mwaka 2018 stamina shorobwenzi alikua ana mchepuko sehemu nilipopanga mimi. Siku nimekaa kibarazani naona imekuja toyota crown mara bidada huyo anatoka ndani anaingia kwenye ile gari ila kwa mbali nilimuona Stamina ila sikuamini hivyo sikutilia maanani.

Siku ilofuata mishale ya saa moja jamaa huyo na ndiga yake anakuja kumchukua bidada mara akakwama kwenye matope. Ndo bidada kuja kuomba msaada tukasukume gali ndo kumuona stamina basi tukamsaidia gari lilivotoka jamaa akaweka pembeni tukapiga story sana akatuhadithia historia ya maisha yake mpaka kutoka kimuziki. Pia namna alivotengeneza ukaribu na Roma. Akamchukua bidada wakasepa.

STORY 2
Nilikua kwenye mishe zangu za kila siku sina hili wala lile mishale ya saa nane mchana simu yangu iliita baada ya kuitizama niligundua ni brother anaefanya kazi karibu na ofisi yetu ndo alikua akinipigia. Nilipokea akanipa maelekezo kwamba kuna mwanadada anatokea Mbeya utampokea kisha utamuonesha magari ya kwenda Songea nikamkubalia kisha baada kama ya saa mwanadada akapiga kunipa maelekezo kua keshafika nimfuate alipo.

Basi nikaazima boda ya mtu wangu wa karibu nikaenda mpaka yule dada alipo ila nilishikwa na butwaa kidogo nikijisemea moyoni mbona huyu dada namfahamu. Basi nikagundua ni msanii Chemical muimbaji wa miondoko ya HIP HOP. Basi nikambeba mpaka ofisini kwetu kwakua aliomba apumzike kabla hajaendelea na safari. Nikapiga nae sana story then nkampeleka stand akakwea Gari huyo akasepa.

HIZI KUMBUKUMBU KWANGU HUA ZINANIFARIJI NIKIZIKUMBUKA.
 
Msanii wa bongo au? Labda awe wa Hollywood kwa hapa sitaki kuambukizwa zero brain
 
Afu wewe ngoja nicheke[emoji28][emoji23][emoji23]

Mod wamekufanya nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…