Msanii Harmonize kuzindua album yake kesho

Msanii Harmonize kuzindua album yake kesho

Hayawi sasa yamekuwa.. Yule msanii Mwenye Mwili kama Pipaa.. Anayejiita Jeshi, ila watanzania wakasema hapana, wewe ni Tembooo.. hatimae kesho atazindua rasmi Album yake ndani ya viwanja vya mlimani City..

Mliopata mwaliko msisite kutupa updates iyo kesho...
Kajitahidi.

Kwa album zilizotoka hivi karibuni, AFRO EAST ni FIIIIREEEEE
 
Hii nyimbo ya Burnaboy nilisikilize intro nilikubali ngojea niisikie sasa hivi.
 
Njia pekee ya kumsapoti msanii ni kununua kazi zake kwenye platforms mbalimbali zinazouza mziki na kuhudhuria show zake.

Tatizo sisi wabongo kazi za wasanii hatununui tunapenda vya bure,tunasubiria djmwanga,kidebwoy aweke sisi tupakue bire.

Hii album unaweza ukakuta kuna mpuuzi mmoja anainunua online alafu anaiweka kwenye account yake Youtube watu wanaipakua free.
Uyo anaeweka wapakue bure, ndo mzalendo haswa[emoji849]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ashawalipa bana.....

Si ndio alisema ameuza mpaka nyumba zake ili alipe deni. Ashamalizana na WCB
Wasanii wa Tanzania 99% ni vinga'ang'a a.k.a ving'asti. Nyumba gani hizo alizonazo huyu king'ang'a wa Sarah. Unazijua million 500 wewe?
 
Back
Top Bottom