Rubawa
JF-Expert Member
- Dec 25, 2015
- 2,055
- 3,254
Msanii CPWAA ameaga dunia mapema alfajiri ya leo wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa msanii huyo ni kwamba marehemu aliukuwa anaugua ugonjwa wa Nimonia uliopelekea kifo chake.
CPWAA ambaye aliwahi kuunda kundi la Park Lane akiwa na msanii mwenzake Suma Lee kabla ya kundi hilo kuvunjika mwanzoni mwa miaka ya 2000.
CPwaa pia alikuwa ni Mhandisi wa mifumo ya TEHAMA, elimu aliyoipata katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)
Update
Baada ya familia ya Cpwaa kukaa kikao, wamekubaliana kwamba atazikwa siku ya leo saa 10 jioni kwenye makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.