TANZIA Msanii Ilunga Khalifa maarufu 'C Pwaa' afariki dunia Hospitali ya Taifa Muhimbili

TANZIA Msanii Ilunga Khalifa maarufu 'C Pwaa' afariki dunia Hospitali ya Taifa Muhimbili

Rubawa

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2015
Posts
2,055
Reaction score
3,254
Msanii CPWAA ameaga dunia mapema alfajiri ya leo wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa msanii huyo ni kwamba marehemu aliukuwa anaugua ugonjwa wa Nimonia uliopelekea kifo chake.

CPWAA ambaye aliwahi kuunda kundi la Park Lane akiwa na msanii mwenzake Suma Lee kabla ya kundi hilo kuvunjika mwanzoni mwa miaka ya 2000.

CPwaa pia alikuwa ni Mhandisi wa mifumo ya TEHAMA, elimu aliyoipata katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)

Update
Baada ya familia ya Cpwaa kukaa kikao, wamekubaliana kwamba atazikwa siku ya leo saa 10 jioni kwenye makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.

CPWAA.jpg
 
Kwa mujibu wa media za bongo msanii CPWAA, ameaga dunia mapema alfajiri ya leo baada ya kulazwa kwa siku kadhaa.
CPWAA ambaye aliwahi kuunda kundi la ParkLane, akiwa na msanii mwenzake Suma Lee kabla ya kundi hilo kuvunjika,mwanzoni mwa miaka ya 2000, baada ya kutamba na kibao chao "Nafasi Nyingine".

20210117_090500.jpg


Tutamkumbuka ndugu yetu kwa Crank kali zilizoenda chuo kikuu ambazo hadi sasa bado hazijavunjwa rekodi,kama vile:
-Cpwaa ft ngwear and chege
-Problem
-Action ft MsTrinity,Ngwear na Dully
-Six in the morning.
 
Cpwaa ni nani?, jina lake kamili, anaishi wapi, ni mkongo au mbantu, amefia WAP, kwa ugonjwa gan, taarifa umezipata wapi n.k
Ni msanii wa bongo fleva.. kitambo flani walikuwa na kundi lao linaitwa Park leen ( sina hakika kama nime spell well)

Miongoni mwa nyimbo alizopata kuimba ni kama:
1. Nafasi nyingi
2. C Pwaa
3. Action

Alipata kuwa na sauti matata sana..
 
Back
Top Bottom