Msanii Langa afariki Dunia!

Msanii Langa afariki Dunia!

wakuu hbr za majukumu nipo njiani naelekea hm napata taarifa kwa rafiki zangu hapa ya kuwa msanii mwingine wa bongo fleva ameaga DUNIA habari hizi sina uhakika nazo ila aliyefariki dunia ni LANGA naomba msaada wa uthibitisho kwa mwenye uhakika na hbr hizi pls!
 
Wafe wote waisheko tukae kwa amani! Unga noma!

"mbele yake, nyuma yako" na falsalasa ya KIFO huwa ni moja hata wewe unanae haya leo UTAKUFA tu haijalishi ni lini, wapi, au kwa style gani. So keep in watch ts a matter ov tyme. Kadiri mshaale na sekunde za saa zifanyavyo kazi ndivyo na we muda unavyokukaribia wa pumzi na mapigo ya Moyo wako kukata/kugota. NI HAYO TU MKUU.
 
Hivi haya madawa yanauaje watu huku wanatembea wakionekana wazima?ina maana hakuna kuugua kwanza kwa mda mrefu?au kuna uwezekano watu wanauziwa sumu!
 
U'Mjini' unawa cost vijana wetu.

Bado nasisitiza hawa vijana hawana mwongozo kabisa, wakishatoa vi 'single' vika hit basi wanajiona ni maceleb. Wanaona sifa na ufahari kunywa pombe kupitiliza, wanavuta bangi na kubwia unga hovyo hovyo.

Wasioona mbali wanamlaumu Ruge na Kusaga na Clouds FM. Kiukweli kina Ruge tunawaonea.

Vijana wameonesha wana vipaji lakini wanashindwa kuji manage both kama raia wema and financially. Naisihi serikali kwa kushirikiana na wadau wa muziki/sanaa na wanataaluma kukaa chini na kuja na structures zitakazosimamia hii entertainment industry.

Kuwepo na udhibiti wa kisheria, biashara ya muziki isifanyike kiholela holela. Serikali isitengeneze mifumo ya kutoza kodi kazi za sanaa pekee, ije na mpango mbinu wa kuhakikisha kazi za sanaa zinawanufaisha wahusika, wasanii wanasimamiwa (wanakuwa na management madhubuti).

Pili

Hatuwezi kupiga vita madawa ya kulevya kwa kuita waathirika ikulu na Rais kupiga nao picha.

Hili ni jukumu letu kama jamii. Wauza madawa wanaishi miongoni mwetu. Tuweke sheria kali (hata ikibidi adhabu iwe kunyongwa hadharani). Bila kuchukua hatua madhubuti hatuwezi kushinda vita hii.

Kwa kuwakumbusha tu, biashara ya madawa ya kulevya ni biashara kubwa sana duniani. Watu wengi wazito wananufaika na hii biashara kwa gharama za kaka zetu, dada zetu, watoto zetu na majirani zetu.

Licha ya kupoteza ndugu zetu, madawa ya kulevya yanaongeza mzigo kwa taifa. Watu wanakuwa tegemezi, uhalifu unaongezeka na tija kwenye shughuli za kiuchumi inadorora na hivyo kama taifa juhudi zetu za kujiletea maendeleo zinadumaa.

Kushinda hii vita hatuitaji kuongeza camera na wapiga picha ikulu, tunaitaji kutangaza madawa ya kulevya kama JANGA LA KITAIFA.

Bila kuchukua hatua madhubuti sasa, tutaendelea kulia kwa uchungu juu ya vifo vya ndugu zetu, jamaa zetu na watanzania wenzetu.

UPUMZIKE KWA AMANI MAREHEMU LANGA.
 
Jide hakuna kihairisha Show ila iwepo nafasi ya kutoa heshima kwake....
 
amani kwa kaka voda milionea,tozi nyandu! vijana wako wanazidi kuteketea
daz baba...
ray c......
lod eyez...
dark master....
chid benz.....
bu nako.....
tid......
mr blue....
msafiri diof.....
banza stone.....
aisha madinda.....
christian bella......
...........
 
Msafir diouf, daz baba, feruz, t.I.D, ray c, lord eyez banza, bushoke na wengine kuweni makini
 
Watu saa hizi wako kazini kucopy kuedit na kupaste postmortam ya Emmy Winehouse kesho utaiona humu wakidai ya Langa! God will keep u where u deserve to be Jembe
 
R.I.P Langa...kinachonihuzunisha ni kuwa wasanii wetu mnakufa maskini while ur so talented!Kaka Kala Jeremiah ebu tuzo moja mpatie marehem tafadhali
 
Sad news n great loss indeed.I knw th dude from primary school to O level at Loyola,he could hav made it so far kama tungekuwa na institutes za kuendeleza vipaji.at Olimpio I knew he could draw sana tu,then later had passion for music wit hz crew Wu-Tang wa Loyola.I can't believe all this is gone,R.I.P comrade

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Well said mkuu, nlikua nae class moja loyola na alipenda sana hiphop na kikapu kimtindo. Soo sad newz RIP BRO.


Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
"mbele yake, nyuma yako" na falsalasa ya KIFO huwa ni moja hata wewe unanae haya leo UTAKUFA tu haijalishi ni lini, wapi, au kwa style gani. So keep in watch ts a matter ov tyme. Kadiri mshaale na sekunde za saa zifanyavyo kazi ndivyo na we muda unavyokukaribia wa pumzi na mapigo ya Moyo wako kukata/kugota. NI HAYO TU MKUU.

Mkuu, heshima kwako.

Umeeleza vizuri sana, humu JF kuna watu wana jidhalilisha sana, haya yote ni kutokana na fake ID.

Kwa mtu mwenye akili timamu na anae jitambua, kamwe hawezi kuongea upuuzi alio usema huyo kijana ulie mjibu.

Amenisikitisha sana.

R.I.P Langa.
 
Back
Top Bottom