U'Mjini' unawa cost vijana wetu.
Bado nasisitiza hawa vijana hawana mwongozo kabisa, wakishatoa vi 'single' vika hit basi wanajiona ni maceleb. Wanaona sifa na ufahari kunywa pombe kupitiliza, wanavuta bangi na kubwia unga hovyo hovyo.
Wasioona mbali wanamlaumu Ruge na Kusaga na Clouds FM. Kiukweli kina Ruge tunawaonea.
Vijana wameonesha wana vipaji lakini wanashindwa kuji manage both kama raia wema and financially. Naisihi serikali kwa kushirikiana na wadau wa muziki/sanaa na wanataaluma kukaa chini na kuja na structures zitakazosimamia hii entertainment industry.
Kuwepo na udhibiti wa kisheria, biashara ya muziki isifanyike kiholela holela. Serikali isitengeneze mifumo ya kutoza kodi kazi za sanaa pekee, ije na mpango mbinu wa kuhakikisha kazi za sanaa zinawanufaisha wahusika, wasanii wanasimamiwa (wanakuwa na management madhubuti).
Pili
Hatuwezi kupiga vita madawa ya kulevya kwa kuita waathirika ikulu na Rais kupiga nao picha.
Hili ni jukumu letu kama jamii. Wauza madawa wanaishi miongoni mwetu. Tuweke sheria kali (hata ikibidi adhabu iwe kunyongwa hadharani). Bila kuchukua hatua madhubuti hatuwezi kushinda vita hii.
Kwa kuwakumbusha tu, biashara ya madawa ya kulevya ni biashara kubwa sana duniani. Watu wengi wazito wananufaika na hii biashara kwa gharama za kaka zetu, dada zetu, watoto zetu na majirani zetu.
Licha ya kupoteza ndugu zetu, madawa ya kulevya yanaongeza mzigo kwa taifa. Watu wanakuwa tegemezi, uhalifu unaongezeka na tija kwenye shughuli za kiuchumi inadorora na hivyo kama taifa juhudi zetu za kujiletea maendeleo zinadumaa.
Kushinda hii vita hatuitaji kuongeza camera na wapiga picha ikulu, tunaitaji kutangaza madawa ya kulevya kama JANGA LA KITAIFA.
Bila kuchukua hatua madhubuti sasa, tutaendelea kulia kwa uchungu juu ya vifo vya ndugu zetu, jamaa zetu na watanzania wenzetu.
UPUMZIKE KWA AMANI MAREHEMU LANGA.