Msanii Langa afariki Dunia!

Msanii Langa afariki Dunia!

Wasaniii wenzangu imefika wakati sasa wa kuwa kitu kimoja tumekuwa apamoja kwenye msiba wa ndugu yetu albert naomba tuwe pamoja kwenye msiba wa langa na hata ikiwezekana aagwe sehemu ile alioagwa albert kuleta heshima na hili lisiwe tu kwaa ngwea na langa liwe kwa kila msaanii kama mnavyojumuika pamoja naamini kuwaona mko pamoja kwenye msiba huu na mungu wa mbinguni awasaidie tuyamalize tukamzike salama kaka yetu mdogo wetu ndugu yetu amen amen amen
 
Msiba upo king'oko Mikocheni A? Tupe direction anakaa nyuma ya kairuki au jirani na nyumba ya riz1?
 
Mkuu, heshima kwako.

Umeeleza vizuri sana, humu JF kuna watu wana jidhalilisha sana, haya yote ni kutokana na fake ID.

Kwa mtu mwenye akili timamu na anae jitambua, kamwe hawezi kuongea upuuzi alio usema huyo kijana ulie mjibu.

Amenisikitisha sana.

R.I.P Langa.
Kumbe wakati mwingine unakuwaga ni Timamu eh! Well said R.I.P Langa
 
msiba upo king'oko mikocheni a? Tupe direction anakaa nyuma ya kairuki au jirani na nyumba ya riz1?
ukiingia ile njia ya aar hospital..ukikutana hata na mwokota uchafu wanatembeaga pemben ya barabara muulize paalipo na msiba anakupelekea moja kwa moja kwa mkuu mitaa hiyo hiyo ya nyumba ya babake riz1..sina uhakika ni ya riz1 samahni kwa hili
 
Msanii wa Hip Hop Langa Kileo amefariki dunia kwa ugonjwa wa "malaria"






Pole mzee Kileo kwa kufiwa na mwanao. Ulimjali sana kwa juhudi zako za kumsomesha shule zenye hadhi nje na ndani ya nchi. Hata hivyo malengo yako Mzee Kileo hayakutimia kwani mwanao aliharibika kwa kufuata maisha ya wahuni wa magharibi kama kina Tupac na Snoopy Doggy wa marekani. Kwa maelezo yake marehemu mwenyewe hivi karibuni, anasema alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na akina Mangwea.

Vijana mnaojiita wa kizazi kipya na mashabiki wenu, Mrudieni Mungu, achaneni na uchu wa kutafuta umaarufu kupitia uchafu wa Miziki ya kijinga. Aliyewaumba anawasubiri!!!

Chanzo, Global Publishers

Na Mwandishi Wetu
MSANII wa Hip Hop, Langa Kileo, amefariki dunia, jana baada ya kuugua ugonjwa wa malaria.
Langa ambaye alitamba na wimbo wa Hoi, alioimba pamoja na memba wenzake wa lililokuwa Kundi la Wakilisha, Sarah na Witness, amefikwa na umauti kutokana na malaria kali ikiwa ni muda mfupi tangu alipolazwa kwenye Hospitali ya Muhimbili, juzi jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia juu ya taarifa hizo, Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Aminiel Eligaesha, alisema: “Ni kweli msanii Langa amefariki dunia leo (jana) majira ya saa 11 jioni, hatuwezi kutoa taarifa zaidi kwa kuwa hilo ni jukumu la madaktari pamoja na familia yake.”
Baada ya kupata taarifa hizo, Championi Ijumaa lilifika mpaka nyumbani kwao Langa, maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambapo lilikuta ndugu na jamaa wakiwa na huzuni.
Akizungumza na gazeti hili, baba mzazi wa msanii huyo, Mzee Kileo, aliliambia gazeti hili kuwa, ni kweli mtoto wake amefariki dunia na kuhusu taratibu za maziko ya mwili wa Langa, walitarajia kuafikiana jana usiku.

HISTORIA YA LANGA
Kipaji cha Langa kilianza kuonekana mwaka 2004 aliposhiriki katika shindano la kusaka vipaji la Coca Cola Pop Star, ambapo alikuwa ni miongoni mwa washindi watatu, akiungana na Sarah Kaisi ‘Shaa’ na Witness Mwaijaga.
Wakiwa watatu, waliunda kundi lililojulikana kwa jina la Wakilisha ambapo walitoa nyimbo kadhaa zikiwemo Hoi na Kiswangish, lakini baadaye Shaa alijitoa na kufanya kazi za kujitegemea.
Wakilisha walibaki wawili ambapo waliamua kubadili jina la kundi na kujiita Wakili na kutoa wimbo wa No Chorus, baadaye hawakudumu kwani kila mmoja aliendelea kufanya kazi zake za kujitegemea.
Langa aliendelea kufanya kazi zake na kutoa nyimbo kadhaa huku akishirikishwa kwenye nyimbo nyingi za wasanii wakubwa, lakini hakufanikiwa kupata mafanikio makubwa.

MATUMIZI YA MADAWA
Baadaye aliingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ambapo Langa aliwahi kukiri kutumia madawa hayo na kusema yupo tayari kuacha.
Kutokana na kujitangaza, Langa alipata msaada kutoka kwa wadau katika kujiondoa kwenye matumizi ya madawa hayo, ambapo baadaye alitamka kuwa amejiondoa na yupo safi.
Baadaye aliamua kufanya kampeni ya kuwashauri vijana kujiepusha na matumizi ya madawa hayo kwa kushiriki katika semina mbalimbali.

WIMBO WA MWISHO
Mpaka umauti unamkuta, alikuwa na muda mfupi tangu alipotoa wimbo wake mpya wa Rafiki wa Ukweli ambao pia wiki mbili nyuma aliitolea video yake.

AKOROFISHANA NA FID Q
Wiki mbili zilizopita, Langa alinukuliwa akilaumu kitendo cha msanii mwenzake wa Hip Hop, Fid Q kutumia mdundo ‘beat’ wake kwenye wimbo wa Sihitaji Marafiki, lakini Fid Q alijibu kuwa halikuwa kosa lake, bali alipewa na prodyuza wake.

ALIMUAGA MANGWEA
Muda mfupi baada ya kupata taarifa ya kifo cha Mangwea, Langa aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook:
“Nakumbuka tulizoea kupiga stori pamoja, kuvuta sigara wote, kunywa pamoja na kutaniana. Nilizoea kukuita Snoop Dogg, wewe ukaniita Tupac, tulitarajia kutengeneza wimbo pamoja lakini bahati mbaya umeondoka mapema. Pumzika kwa amani.
R.I.P Ngwea.”
 

Attachments

  • Picture1.png
    Picture1.png
    29.8 KB · Views: 126
  • langa.jpg
    langa.jpg
    39.8 KB · Views: 121
RIP Langa. Hip hop imepungukiw na kichwa muhimu. Nakumbuka mashairi yake kwenye wimbo wa Fid Q, Chagua moja.
 
Kama kawa! Watu weusi tumeshawazoea, yaani tayari mmeshaifanyia uchunguzi maiti na tayari mna majibu!! Unafki mtaacha lini ninyi waafrika!!?

Well said,,,yaani watu washafanya autopsy katika mind zao tayari and come out with the cause of dealth. How sad!!
 
"Mashati ya kaki,marashi ya issey miyake ukinchek mwenyewe msafiichokoza uone moto sitokei masaki natokea king'oko"

Rest in the perfect peace Ninja

kitu nanyonga mwenyewe
wala simwamini pusha,
hukawii kuuziwa ngano
ukaambiwa cha iran,
ganja navuta,
unga nabwia,
kwanja naruka,
unga wa kushea sindano
mi sijidungi,
hujui wamedunga wangapi mda uliopita
 
Duuh jamani haya madawa ya kulevya ni nomaaaaaaaaa sanaaaaaaaaa, vijana wajiangalie sana RIP Langa
 
kitu nanyonga mwenyewe
wala simwamini pusha,
hukawii kuuziwa ngano
ukaambiwa cha iran,
ganja navuta,
unga nabwia,
kwanja naruka,
unga wa kushea sindano
mi sijidungi,
hujui wamedunga wangapi mda uliopita


mabuti ya kijeshi uyaone mafupi mepesi//
yaani kama vile 'simple' toka nduki toka 'race'//
kama risasi ya bunduki au jeti/
no kunyuti no kuketi/
wape nafasi wakushuti kama Malcolm X//
usikubali kubaki uwe pimbi upewe kesi//
ikibidi jitose ndani ya dimbwi la kinyesi//
sio suala la uoga kuogopa ukunguru..\\
ila bora kulogwa kuliko kukosa uhuru\\
wapi sheikh Mponda wapi Jenerali Komba/
sirikali sera kali cheza mbali na wajomba/
kimbia,
mitihani imevuja nyie hamjasikia?//
ya nini kusoma huku elimu inanunuliwa//
kimbia,
nchi imeshauzwa hii hamna kusikilizia//
TANESCO,Madini hadi Air Tanzania//
watoto wa uswazi hawana matumaini/
ndoto za ujambazi sababu ya umasikini/
matapeli wenye shahada kila hatua tatu//
makahaba wa miaka kumi na tatu//
maskani kama msitu vicheche na machatu//
usipite pekupeku bila kuvaa viatu//

aaaaah!kimbiaa ♫♫♫

Lyrical And Natural Gifted African(L.A.N.G.A).
MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA LANGA KILEO.............
 
Pumzika kwa AMANI LANGA,
Dunia tunapita
 
kitu nanyonga mwenyewe
wala simwamini pusha,
hukawii kuuziwa ngano
ukaambiwa cha iran,
ganja navuta,
unga nabwia,
kwanja naruka,
unga wa kushea sindano
mi sijidungi,
hujui wamedunga wangapi mda uliopita
Demu wa usiku mmoja simpigi lita sijui wamepga wangap muda ulopita
 
Back
Top Bottom