TANZIA Msanii Mkongwe Mohammed Fungafunga (Mzee Jengua) afariki Dunia

TANZIA Msanii Mkongwe Mohammed Fungafunga (Mzee Jengua) afariki Dunia

Innalillah waynnayilah rajiun, huyu mzee ndo msanii aliyekua kabaki nikiangalia movie zake nafurah baada ya kututoka mzee majuto..

Kafanya makubwa sana kwenye tasnia, Sadly watu Hawa hata wakifaliki huwa hawasaminiwi ila akifa mwanasiasa unaskia soko flani linapewa jina lake inasikitisha sana
 
Nimemkumbuka early 2002 alipokuwa anaigiza kama mjomba wake Norah alipomfukuza dk cheni na panga,kipindi hiko jumamosi saa 21:00 hunikosi mbele ya runinga ya mjomba nikiwasubiria hawa jamaa na kupitia maigizo yao vijana wa enzi zile tuliokuwa bado tunakua wakubwa zetu walikuwa wakituonya kwa kutumia mifano iliyotokana na michezo ile,ilikuwa inafundisha sana na waigizaji wake walikuwa wanauvaa uhusika vizuri sana.huyu ni mmoja wa watu niliokuwa napenda uigizaji wao na yule Mashaka aliigizaga kama tajiri mara mlala majalalani pia alikwepo jamaa mmoja akiitwa somebody Seki/Sheki akiigiza uhuni na mvuta bangi na jamaa mmoja akiitwa Swebe

Tutoto twa 2000s tutakwambia huyu kaanza kuigiza bongo movie juzi juzi,alikuwa vizuri sana akiigiza upande wa kulinda maadili na utamaduni hasa akiitumia sauti yake ya ukali huku macho ameyakaza na sura imekunjamana,alikuwa na kipaji haswa.

Mungu amrehemu marehemu Jengua.
 
TANZIA!! TANZIA!!

Chama cha waigizaji Dar-es-salaam Tanzania. TDFAA.

IMG_9317.jpg



Tunayo masikitiko makubwa mno! Kutangaza kifo cha Muigizaji mwenzetu almaarufu mzee Jengua .

Kilichotokea Leo 15-12-2020 majira ya asubuhi nyumbani kwa mtoto wake mkuranga.

Tumethibitisha taarifa Hizi kutoka kwa mke wake.

Tuzidi kuiombea Familia pamoja nakushiriki katika kuwafariji.

Taratibu za mazishi zitatolewa hapo baadae na familia.
Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina Lake lihimidiwe. [emoji1431][emoji1431]

Doricy Kente

*Katibu mkoa Dar-es-salaam
 
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi amini..
 
Hakuna ushahidi wa hii habari hivyo ni vema iondolewe
 
Back
Top Bottom