TANZIA Msanii Mkongwe Mohammed Fungafunga (Mzee Jengua) afariki Dunia

TANZIA Msanii Mkongwe Mohammed Fungafunga (Mzee Jengua) afariki Dunia

Mzee Mohammed Fungafunga maarufu katika tasnia ya filamu kama "Jengua" amefariki dunia leo Desemba 15, Mkuranga mkoani Pwani baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Chanzo: mtanzanianews

Wiki iliyopita nilipoona tu Msanii na Mwigizaji Nguli nchini Wema Sepetu analia na kututaka tumuombee nilianza Kumuelewa hasa juu ya kile 'Kinachomsibu' Kiafya ila na hii taarifa ya leo juu ya Kifo cha huyu 'Jamaa' aliyejua Kuuvaa vyema 'Uhusika' nimeamini kuwa huenda huko mbeleni Wasanii na Wanamuziki wengi nchini Tanzania 'wakatuacha' Kimaajabu ajabu kwa Ugonjwa wa Nyani.
Kama kirusi cha nyani ndo chanzo cha kudedi basi foleni ni ndefu kama mabehewa ya treni...
 
Jamanii huyu Baba alikuwa ananichekeshaga sana, na nilimpenda kweli yan
Mimi pia alikua mkali mwenye maneno ya kuchekesha ndani yake,
Nimesikitika sana kwa kifo chake,
Atangulie kwa amani na sisi tutaenda.
 
Nawaonea sana Huruma hapa hasa Baba na Mwana 'Napiga Soga Chalinze' ambao kwa Nyakati tofauti wote wamepita kwa 'Tenda Wema' uondoke.
Duuuu, hii pesa na umaarufu ni vitu vizuri lkn ni hatari sana.
 
Yeah ni level za kina mzee Majuto nakumbuka alikua na mtoto wake anaitwa Peace kwenye maigizo ya kidedea enzi hizo da alikuwaga noma sana dingi mkali mtoto anatoroka kwenda disco
Peace alishafariki, hakuwa mtoto wake ila alikuwa ni mwanamke ambaye Jengua alikuwa anamtaka halafu Peace anamchomolea. Peace alikuwa ni mpangaji kwenye nyumba ya mama mdogo wake John.

Mtoto wa Jengua aliyekuwa anatoroka toroka alikuwa anaitwa Tabia (naye kama sikosei alikwishafariki dunia).

Chemchem Sanaa Group..kitambo sana
 
Hakuna atakayeishi milele. Kama ni sahihi pumzika kwa amani mzee wetu.
 
Niliacha kuangalia bongo movie 2013 ....

nikarudi kutazama tamthilia hiyo bila kukosa episode hata moja .....
wahusika walijitahidi Sana kuvaa uhalisia....niliipenda
Wahusika walipendeza sana, Binafsi nilivutiwa na Clara, Mke wa Mtawala, Koku, kwa ufupi huwa sichoki kuitazama hii
 
Wahusika walipendeza sana, Binafsi nilivutiwa na Clara, Mke wa Mtawala, Koku, kwa ufupi huwa sichoki kuitazama hii
Mwinyi mkuu , kitale, mtawala ,kobelo ....
walinivutia sana kila mmoja Kwa nafasi yake....
Mzee wa kulukutata mantetele.....
 
Na kinachoniuma zaidi ni kwamba Baba Chalinze 'napiga Soga' na Mwanae Chalinze 'napiga Soga' Wote wamepita hapo kwa nyakati tofauti tofauti.
Ahahahah sema ukiwa na hela huu ugonjwa hautishi kivile
 
MKONGWE wa Tasnia ya Maigizo nchini Mohammed Fungafunga maarufu Kama Mzee Jengua amefariki dunia asubuhi ya Disemba 15 huko Mkuranga, mkoani Pwani.

Marehemu alikua akisumbuliwa na Maradhi ya Kiharusi.

Enzi za uhai wake, Mzee Jengua alikua akiigiza Maigizo kama vile Kidedea, Handsome wa Kijiji, Kashinde na zingine nyingi.

Mungu aiweke roho yake mahala pema.

Ameen.

=======

Jengua amefariki leo asubuhi, kwa taarifa ya awali tunatarajia kumzika kesho saa nne asubuhi Mburahati, amefia nyumbani kwa Mtoto wake Mkuranga, sio vyema kusema maradhi ya Mwenzetu kwasababu Daktari ndiye anaweza kuthibitisha kifo ila ameumwa kwa muda kidogo, nashindwa kusema hapa kifo kimetokana na nini”-Chiki Mchoma, Mwenyekiti wa Waigizaji

View attachment 1650591View attachment 1650592
Picha: Mzee Jengua enzi za Uhai wake
Rip
 
Back
Top Bottom