Nimemkumbuka early 2002 alipokuwa anaigiza kama mjomba wake Norah alipomfukuza dk cheni na panga,kipindi hiko jumamosi saa 21:00 hunikosi mbele ya runinga ya mjomba nikiwasubiria hawa jamaa na kupitia maigizo yao vijana wa enzi zile tuliokuwa bado tunakua wakubwa zetu walikuwa wakituonya kwa kutumia mifano iliyotokana na michezo ile,ilikuwa inafundisha sana na waigizaji wake walikuwa wanauvaa uhusika vizuri sana.huyu ni mmoja wa watu niliokuwa napenda uigizaji wao na yule Mashaka aliigizaga kama tajiri mara mlala majalalani pia alikwepo jamaa mmoja akiitwa somebody Seki/Sheki akiigiza uhuni na mvuta bangi na jamaa mmoja akiitwa Swebe
Tutoto twa 2000s tutakwambia huyu kaanza kuigiza bongo movie juzi juzi,alikuwa vizuri sana akiigiza upande wa kulinda maadili na utamaduni hasa akiitumia sauti yake ya ukali huku macho ameyakaza na sura imekunjamana,alikuwa na kipaji haswa.
Mungu amrehemu marehemu Jengua.