Msanii Mr. II aka Sugu akataa "posho" ya TSh. 2m kutumbuiza kwenye tamasha la miaka 30 ya Bongo Flava

dronedrake

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2013
Posts
24,847
Reaction score
61,886
Sugu anadai: Walianza kuniita kwenye wimbo, Madee alinipigia simu tukaenda studio, sasa tunatoka studio aliponishusha akanitumia mkwanja Milioni 2, I was like mimi sijawahi kulipwa hela kufanya featuring na nimefanya featuring na watu wengi nikwambia Madee.....

Sugu akaongeza: Hii game naijua niambie kuna nini kipo nyuma ya hii? Najua huna hiyo hela kwahiyo niambie nini kinaendelea kama ni mpango endelevu isije fika huko mbele mkaniweka kwenye project ambayo sitakuwa comfortable kuifanya.

Sugu akahitimisha kwa kusema: Ndio baadae sasa wakaja na hii idea ya Miaka 30 nikawaambia thank you so much ila siwezi

Ikumbukwe tu, msaani Mr II aka Sugu ni muanzilishi wa BongoFlava Honors, tamasha la kimuziki linalolenga kuwatunuku tuzo za heshima wasanii wa Bongo Flava wa "kitambo" Tanzania (na kidogo Uganda/Kenya) ambalo hufanyika kila baada ya miezi kadhaa

============================================================================

reeet.PNG
 
Hakusema 2M kwa ajili ya show ila alipewa 2M ili aje aingizwe ktk miaka 30 kama sehemu ya waandalizi na mipango

Yote kwa yote Sugu ana Ego anaamini kuwa yeye ni Bora kuliko watu wengine kitu ambacho sio kibaya ila kwa Ile show ya mliman City ilienda vizuri
 
Wasanii wa sasa wanatumika kama puppets wa wafanyabiashara wakubwa ili kuwanyonya wakongwe kijanja.

Kwanza ana tamasha lake la BongoFlava Honors kwanini akubali kufanywa msanii wa kusindikiza kwenye project ya wapinzani wake?
 
Sugu huwezi kumpa milioni 2 ya kufanya show! Nina imani hiyo ni pesa ndogo sana kwake.
Pesa ndogo kwa msanii yeyote yule lakini lile tamasha ni just heshima tu,Zile show za Super Bowl Marekani wasanii huwa hawalipwi lakini wasanii wote wanajisikia fahari kutumbuiza kwenye show zile..Wasanii matajiri kabisa kama kina Jay z,Michael Jackson,Dr Dre nk wameshatumbuiza hapo sema tu ni vile Sugu huwa ana Ego ya kujisikia
 
Basi kiufupi ni project ambayo imeandaliwa kimiyeyusho na ipo hivyo na ndio mana sugu aligoma….usiklinganishe na SUPER BOWL😎
 
Pesa ndogo kwa msanii yeyote yule lakini lile tamasha ni just heshima tu,Zile show za Super Bowl Marekani wasanii huwa hawalipwi lakini wasanii wote wanajisikia fahari kutumbuiza kwenye show zile..Wasanii matajiri kabisa kama kina Jay z,Michael Jackson,Dr Dre nk wameshatumbuiza hapo sema tu ni vile Sugu huwa ana Ego ya kujisikia
Huanda pia aliona Tamasha lina harufu ya siasa ( Mwana FA ) alianza leta siasa waka mtupa.. Na lengo huenda lilikuwa lile la FA mengine ilikuwa njia ya kufikia hapo. Mwisho wa siku kila mtu ana maamuzi yake
 
Pesa ndogo kwa msanii yeyote yule lakini lile tamasha ni just heshima tu,Zile show za Super Bowl Marekani wasanii huwa hawalipwi lakini wasanii wote wanajisikia fahari kutumbuiza kwenye show zile..Wasanii matajiri kabisa kama kina Jay z,Michael Jackson,Dr Dre nk wameshatumbuiza hapo sema tu ni vile Sugu huwa ana Ego ya kujisikia
issue ni why umpe hela mkuu. Anakodiwa au. Respect ni ya maana kuliko izo pesa.
 
Nilivyoelewa hiyo 2m aliilamba kwa ajili ya kufanya ule wimbo wao wa kina madee ,madee alimpa kama shukrani ila ndiyo akamuuliza mbona umenipa mtonyo wa nini isije kuwa kama mtego wa kuja kunibana huko mbele.
 
Pesa ndogo kwa msanii yeyote yule lakini lile tamasha ni just heshima tu,Zile show za Super Bowl Marekani wasanii huwa hawalipwi lakini wasanii wote wanajisikia fahari kutumbuiza kwenye show zile..Wasanii matajiri kabisa kama kina Jay z,Michael Jackson,Dr Dre nk wameshatumbuiza hapo sema tu ni vile Sugu huwa ana Ego ya kujisikia
99% ya wasanii ni chawa watiifu wa ccm..

Sugu alihisi kitu hakipo sawa, na akaheshimu hisia zake..

Mi naona alikuwa sawa.. sio suala la kujiona bora kuliko wengine..

Hali ya hewa imechafuka, lazima uishi kwa tahadhari sana..
 
Back
Top Bottom