Msanii Mr. II aka Sugu akataa "posho" ya TSh. 2m kutumbuiza kwenye tamasha la miaka 30 ya Bongo Flava

Msanii Mr. II aka Sugu akataa "posho" ya TSh. 2m kutumbuiza kwenye tamasha la miaka 30 ya Bongo Flava

Sugu anadai: Walianza kuniita kwenye wimbo, Madee alinipigia simu tukaenda studio, sasa tunatoka studio aliponishusha akanitumia mkwanja Milioni 2, I was like mimi sijawahi kulipwa hela kufanya featuring na nimefanya featuring na watu wengi nikwambia Madee.....

Sugu akaongeza: Hii game naijua niambie kuna nini kipo nyuma ya hii? Najua huna hiyo hela kwahiyo niambie nini kinaendelea kama ni mpango endelevu isije fika huko mbele mkaniweka kwenye project ambayo sitakuwa comfortable kuifanya.

Sugu akahitimisha kwa kusema: Ndio baadae sasa wakaja na hii idea ya Miaka 30 nikawaambia thank you so much ila siwezi

Ikumbukwe tu, msaani Mr II aka Sugu ni muanzilishi wa BongoFlava Honors, tamasha la kimuziki linalolenga kuwatunuku tuzo za heshima wasanii wa Bongo Flava wa "kitambo" Tanzania (na kidogo Uganda/Kenya) ambalo hufanyika kila baada ya miezi kadhaa

============================================================================


View attachment 3635455
Hiyo ni project ya Makonda kufubaza watu kuhusu mauaji kabla na baada ya uchaguzi wa 2025.
Bado lengo la Samia kupiga simu live sijui kama Mwanza itawezekana maana Dar mambo hayakwendwa kama yalivyopangwa.
 
Nilivyoelewa hiyo 2m aliilamba kwa ajili ya kufanya ule wimbo wao wa kina madee ,madee alimpa kama shukrani ila ndiyo akamuuliza mbona umenipa mtonyo wa nini isije kuwa kama mtego wa kuja kunibana huko mbele.
Hata mimi nimeelewa 2m ni ya kushirikishwa kwenye wimbo wa DANGER
 
2Proud, ndio oldest bongo fleva artist.
Kwa mara ya kwanza naanza kumsikia Febuary 1997 kipindi hicho nikiwa kifaranga kabisa.... RFA Fm radio

Enzi hizo wapo
1.Basil Mbakile
2. Rehema Salim
3. Peter Omary
4. Stella Mathius

ETYMOLOGY
Huyu SUGU Mnayemjua leo, alianza kujulikana kwa jina la 2 Proud.....aki- jaribu kufananisha jina lake na 2 PAc, Rapa wa Marekani...kama role model.
Mwaka 1998,
Akatoa Wimbo unaitwa "Niite Mr two" kuanzia hapo jina la awali la 2 proud likafa hapohapo..
Mwaka 2004
Akatoa wimbo akishirikiana na mraibu Pauline Zongo unaitwa "Wananiita Sugu"
Na likawa jina lake hata leo.
Wewe jamaa ama hujui au umesahau, Stara Thomas anakuwaje Pauline Zongo?
Ila kama ulianza kumsikia Sugu RFA sikushangai
 
Back
Top Bottom