Msanii namba 1 Afrika kwa sasa, Diamond Platnumz ajenga nyumba ya Ibada (Msikiti)

Msanii namba 1 Afrika kwa sasa, Diamond Platnumz ajenga nyumba ya Ibada (Msikiti)

Halafu siku ya uzinduzi wa msikiti wataanza kuwaponda wa upande wa pili kwa kuwaita makafiri kwa sababu ya kuvaa hereni, kata k na uzinzi!
9b4389839c07de152fdb60de9fe6d56f.jpg
 
Faman Ya'amal Mithqaala Dharratin Khayran Yaraa.

Waman Ya'amal Mithqaala Dharratin Sharran Yaraa.

ALLAHU YA'ALAM.
 
Kwa kweli mimi ni shabiki wa Diamond lakini kusema yeye ajenge msikiti na watu wakaswali kabisa siungi mkono. Anayo yafanya sidhani kama dini ina yaunga mkono.

Ni sawa sawa na jay z ajenge kanisa, au davido ajenge kanisa. Yaan haija kaa poa.
Kwani unadhani misikiti na makanisa yote yamejengwa kwa pesa za halali? Ndio maana ikawepo touba, na hakuna mkamilifu ila Allah, tumuombe tu atujaalie mwisho mwema nae Allah amjaalie mwisho mwema aamiyn..
 
Hili ni jambo la kheri,halipaswi kabisa kubezwa.
Pamoja na madhaifu yake kama binadamu ila kwa hili nampongeza.

Ifikie mahali tuache unafiki,ni nani asiye na dhambi kati yetu?Kuvaa kwake hereni hakumzuii kujenga msikiti, ingekuwa ndio hivyo basi hata swadaka tulio wengi tusingetoa misikitini maana kama ni utimilifu ndio kigezo cha kutoa swadaka hakika hakuna aliye kamili zaidi ya Mtume Muhammad (S.A.W)

Allah akuzidishie kheri Nasib,uzidi kujenga misikiti mingine mingi watu wapate kufanya ibada na kumcha Mola wetu.
Swadakta
 
Misikiti mingi huku mitaani inajengwa kwa swadaka na michango mbalimbali yetu sisi waumini.
Kuna anayejua kila swadaka/mchango wa muumini chanzo chake ni khalal?
Ni wapi swadaka ya muumini imewahi kukataliwa msikitini?
Tena wengine ni 'madon' wa sembe na Masheikh wanajua fika ila swadaka zao wanazipokea.

Allah ndiye hakimu,atamhukumu kila mmoja wetu kwa kadiri ya aliyoyatenda.
Period
Na huo ndio ukweli.
 
Bado miaka kumi na moja kustaafu kazi na hata yale mafao ya mpaka ufikishe 55years, kwangu wakinitumbua sasa sina presha kivile!! Ole wako wewe unayewaza shule sasa!!!!
Basi pole kumbe adult afu unaandika hiki kitu
 
Nyumba ya ibada haijengwi na mtu mmoja, atofautishe dini na misaada mengine. Ndio maana tumefundishwa unapotoa swadaka hata mkono wakushoto usijue, hapa maana yake usitangaze. Amefanya jambo la kheir ila namuomba asilifanye public namna hii. Achote busara kwa Bakhresa na matajiri wengine wa Kiislamu ambao hutoa kimya kimya kwenye mambo yahusuyo dini.

Allah amjaalie zaidi azidi kusaidia wengine.
Ina maana ukichangia mambo yasiyohusiana na dini yakupasa kupayuka au!!?
 
Kwani unadhani misikiti na makanisa yote yamejengwa kwa pesa za halali? Ndio maana ikawepo touba, na hakuna mkamilifu ila Allah, tumuombe tu atujaalie mwisho mwema nae Allah amjaalie mwisho mwema aamiyn..
Post #64 na #73
Nimejitahidi kueleza hoja yangu na nadhani ina nguvu kabisa kabisa _aysher
 
Pamoja na kuupenda muziki sana. Ila uislam unatambua kuwa muziki ni Haram. So hata ukajenga nn kwa fedha za haramu haitakua na faida kwako baada ya kifo zaidi ya kupoteza swala za waswaliji wa msikiti huo
 
Je ! hiyo biashara ya huo muziki anaoufanya kwa sheria za dini ni " HALAL" Kama ndio good job na amepata thawabu zake, kama sio wanazuoni wanazungumziaje kuhusu zawadi hiyo waamini waliopwa ila wawe wanaswalia hapo?
We nawe unafanya mchezo na hela wewe.. Hilo jaribu anayeliweza ni Yesu pekee
 
Ila Nahisi Jamaa Yupo Vizuri hata Huko Kwenye Pete nyekundu n.k... Yaani Kwa Dunia ya Sasa Hivi mtu unaangaika Unapatwa na Vikwazo kwenye Biashara mpka Unachanganyikiwa ..

Diamond Wasanii wenzake Watakuwa Wameshajaribu Kumroga ashuke Ila Jamaa Arogeki... Maana Wasanii kwa Kuoneana wivu hawajambo
Kamzuia nan kwenye mziki mpaka arogwe kama sio yy ndo mrogaji
 
Pamoja na kupata mafanikio makubwa kwenye muziki msanii number moja Afrika D. Platnumz Dangote pia amerudisha kwa jamii baada ya kutoa misaada mbalimbali na sasa atawasaidia waathirika wa mafuriko huko Iringa, pia anamalizia kujenga msikiti kwa ajili ya Ibada.

Ni mfano wa kuigwa sana huyu kijana. Wengine wanaishia kuvaa vaa mipete mara ya kijani,nyekundu,bluu sasa sijui wanaabudu majini na mazombi.

View attachment 445640
mbona msikiti mdogo jaman? angetengeneza bonge la msikiti
 
Hili ni jambo la kheri,halipaswi kabisa kubezwa.
Pamoja na madhaifu yake kama binadamu ila kwa hili nampongeza.

Ifikie mahali tuache unafiki,ni nani asiye na dhambi kati yetu?Kuvaa kwake hereni hakumzuii kujenga msikiti, ingekuwa ndio hivyo basi hata swadaka tulio wengi tusingetoa misikitini maana kama ni utimilifu ndio kigezo cha kutoa swadaka hakika hakuna aliye kamili zaidi ya Mtume Muhammad (S.A.W)

Allah akuzidishie kheri Nasib,uzidi kujenga misikiti mingine mingi watu wapate kufanya ibada na kumcha Mola wetu.
Umenena vema
 
Back
Top Bottom