Msanii "Pasha" kwa sasa yuko wapi?

Right eye

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
1,149
Reaction score
1,994
Hello..
Nilikua kwenye pitapita zangu nikakuta sehemu zinapigwa ngoma za zamani za bongo fleva..
Ghafla ikapigwa ngoma ya namuimbia ya Pasha aiseeh ilinisafirisha mbali sana kihisia huyu mwamba yuko wapi kwa sasa?..
Alikua amekamilika kuanzia vocal mpaka uandishi..
Kwenye hii ngoma ilipigwa biti na vinanda vya hatari kutoka kwa Mapigo na Saidi Komelei metro studio ndipo lilipopikwa hili dude..
 
Jamaa alikuwa anajua sana kuanzia utunzi,sauti na kucheza na biti.
Nyimbo zake zote ni nzuri na huwezi kusikia matusi kwenye nyimbo zake
 
Muulize hbaba walikuwaga washikaji sana. Leo nmetoka sikiliza ngoma yake ya kitu gani
 
Nazikibli ngoma zake mbili tu yaani Hidaya na ni Soo.
 
Industry ya muziki ni ngumu sana kumaintain ndio maana watu wengi ambao walikua na vipaji halisi walipotea na wengi ambao wapo ni wale ambao wako kwenye strong management kidogo au wameonekana hawana madhara au wanafuata kile ambacho mfumo unahitaji wakifuate na wengine wapo ili mzani uweze kubalance kwa maana asili ya muziki ni kushindana... Indirect Monopolism iko applicable sana kwenye muziki.

Nakumbuka huyo jamaa wakati anatoka walitoka wasanii wengi sana kama kina matonya, kina Z Anthony, kina Jay I na kina Alikiba walitoka nyakati hizo nadhani, hata malow nae ni generation hiyo kama sikosei, kina spark, kina mb dog na kadhalika.

Yaani ilikua huku ukiskia si vibaya kumpenda mtoto hidaya, unakaa kidogo unaskia vailet, mara kidato kimoja, hujakaa sawa bembeleza hii hapa, mara paap kidato kimoja, huku na huku sinderela hii hapa, mara shwaaaaa mpenzi kiziwi huyu hapa, hujatulia vizuri inamana hii hapa ya mb dog...
 

Hapo kwenye Hidaya umechanganya madesa, Hidaya ilikuja baadaye sana wakati kashazinguana naa KGT hapo alikuwa anarudi tena kwa mara ya pili hiyo ni kama 2010.
Ila uko sahihi hao wote ni generation moja kuanzia 2006 hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…