Msanii Ray C azidiwa na Madawa ya Kulevya; asaidiwa na Polisi

dawa pekee ni kukaa sehemu ambayo atakuwa hapati madawa, iwe jela au popote pale
 
Mtoto wa kike kutumbukia kwenye ulevi wa aina hii Allah atunusuru na vizazi vyetu InshaAllah.
 
Anahitaji msaada wa hali na mali.ni khatari sana hii mkuu.
 
Kuna lundo la mateja linahitaji msaada achana na Ray C ambae hataki msaada ashaamua maisha yake.
Nadhani huelewi maana halisi ya 'addiction'. Mtu ambaye yupo addicted hayo mawazo kama yako inakuwa magumu kuyapata. Anaweza akawa ana nia lakini nia pekee itafeli. Hawa watu wanahitaji msaada ili watoke kwenye mtego wa addiction. Wanahitaji uangalizi wa hali ya juu, mwenyewe hawezi.
Na njia kuu ya kuwasaidia watu kama Ray C na mateja wengine ni kupambana na wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya pamoja na wasambazaji wao.
 
DUH kweli yanaenda kasi alikuwa anamtafuta CHID BENZ amasaidie kuacha unga leo yy ndio kapotea mazima wkt Chid ka recover!
 
mkuu Serikali haiko siriasi kuhusu hili suala je sisi tufanyaje?
 
Wote hata hao waliotumbukia kwenye janga la mihadarati ni wakuomba Mola awasaidie.
ndiyo wote ni wakuombewa lakini ukipata msaada wakutoka huko ulipo siyo vyema kurudia tena japo tunajua binadamu ni viumbe dhaifu lakini isiwe sababu
 
Daaaaah..inasikitisha sana kwakweli...inauma zaidi pale ninapofikiria kuwa tutamsaidiaje mtu huyu tukiwa kama individual au taasisi flani....ilihali mtu huyu huyu alishapata msaada kutoka ikulu kabisaaaa yaaan raisi wa nchi kabisaaaa..but alishindwa.....tumuombee tuuu hamna namna.
 
M ntaanza NA maombi...kwavideo niloona tunakazi mbelekubwa kumkomboa kubwasana lakini tusikate yatamaa..wenye instagram mnaweza search globapublishers AMA obbytheng mtamwona anavyochopolewa NA poliisi usiku mawindoni
hasaidiki huyu mwanamke shenzi zake
 


Nguvu hizi naona tungezitumia Zaidi kushinikiza serkali ipambane na waingiza na wauzaji wa hayo madawa ya kuelevya. Hili ni tatizo la jamii kwa ujumla. Hautumii lakini tunao mitaani na twajua wanafanya nini. Wala unga wakamwatwe wawaulizwe wananunua wapi, wakikamatwa wanauza watapeleka kwa wauzaji chanzo. Tz hatupo serious na kupambana na hili janga. Hakuna hasiyejua madhara ya dawa za kulevya. Inakuwaje nguvu zisielekekezwe kupambana na biashara hii.
Kama kweli tunapinga dawa kulevya wala madawa ni waalifu na wapo wazi wakamatwe wachukuliwe hatua na waonyeshe walipozitoa na waliowapa wakamatwe pia mwisho atapatikana papa
 
mtu anakula starehe zake nyie mnalia lia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
unafiki tu wengi wajita wanahuruma kweli kisa anajina lakini kuna mateja wangapi mtaani,kunavijana wangapi wame blind future zao sababu ya haya madudu,jamii haichukui hatua serikali haichukui hatua ..ndo ivyo mchuma janga hula na wakwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…