Msanii Ray C azidiwa na Madawa ya Kulevya; asaidiwa na Polisi

Msanii Ray C azidiwa na Madawa ya Kulevya; asaidiwa na Polisi

Apelekwe kwa wakinga kule ataacha kabisa hiyo mwanamke wa kihindi (unga)
Na yale macho yaleee.... kha mbona mateja sherehe watakuwa na wao wana kesha na kuomba asiwatoke chamani!
Au atokee msamaria mwema amuoe.
 
Kama hiyo ni reference ya utumiaji wa hayo makitu yawezekana kuna jambo la kujifunza. Hebu tujifikirishe kidogo, mbona ni muda mrefu amekuwa akijishughulisha na kuwashawishi watu wasitumie hayo makitu au alikuwa anafanya kinyume chake?
Pengine katika huo muda mrefu alioutumia kushawishi watu wasitumie hayo madawa kuna baadhi yao walibadilika na kuwa clearheaded aidha kwa kuacha kabisa katika hatua zao za mwanzo kabla ya kuanza kuathirika au kwa kuamua kuhudhuria sober homes. Kuna walimu wa ujasiliamali hawana ujasiliamali wowote lakini wanafunzi wao wametumia elimu waliyopewa na hao walimu na kuwa wajasiliamali wakubwa.
 
Kama hauna ndugu wa karibu ambaye amewahi kuwa mtumiaji wa dawa za kulevya basi huwezi kuelewa tatizo linalo mkabili ray c kwa undani zaidi.

Mdogo wangu aliwahi kuingia katika matumizi ya dawa za kulevya nami ndipo niliweza kujionea mwenyewe uzito na ukubwa wa tatizo hili kwa nchi yetu. Namshukuru mungu aliweza kuacha baada ya kumpeleka rehab kigamboni lakini alifanikiwa kuacha kwa sababu tuliwahi kumsaidia. Addiction ni kama roho ndani yako ambayo huwa inataka mahitaji yake ndani ya mwili wa mtu na ili uishinde inahitaji zaidi ya human will.

Bila kumshirikisha mungu zile temptation zinaendelea kuwepo tu na mwishoe mtu anarudi kule kule. Ray c anahitaji msaada wa kimwili kwa kurudi tena rehab lakini pia msaada wa kiroho ili kuweza kupambana na hiyo spirit ya addiction. Hata nchi za magharibi wana mastaa wao ambao rehab zimeshindwa kuwasaidia kwa sababu addiction ni zaidi ya physical, mental war ni spiritual pia, kwa mfano marehemu Amy winehouse, Paul gascoine (gazza) nk.
 
Mi nadhani kwa wale walioguswa na matatizo ya Ray C tusiwakatishe tamaa waacheni walie na kama kuna uwezekano wakiweza wamsaidie. Na kwa wale wasioona umuhimu wa kumsaidia hiyo ni roho yako isikufanye kuwashawishi na wengine wenye kuhitaji kumsaidia.( ni kweli wenye matatizo ni wengi na makubwa zaidi ya hili,lakini hata huyo utakayemuona wewe ni zaidi kuna wa zaidi yake yeye na huenda hayupo tz, sasa je tutafute dunia nzima ili tuwapate wenye matatizo ya kuzidi wengine ndio wasaidiwe..... jibu hapana msaidie yule aliyekugusa kulingana na maono yako na kama kulipwa utalipwa kulingana na ulichojitolea na si ulimsaidia nani ........ na wale wengine nao watasaidiwa hao wengine)
 
Mimi nitaanza na maombi...kwa video niliyoona tunakazi mbele kubwa kumkomboa, kubwa sana lakini tusikate tamaa.

Wenye instagram mnaweza search Globapublishers ama obbytheng mtamwona anavyochopolewa na poliisi usiku mawindoni
 
Mmmh! .unamhurumiaje mtu asiyejihurumia? Ndo maisha aliyojichagulia ! Kwani mkulu alitumia kiasi gani kumtibia?then?
Tatizo ujui nini maana ya mtu kuwa addicted pole sana ila ukipata ndugu yako kawa addicted na unga ndio utakua kwanini RAY C yupo ivi, she needs our help hata kwa maombi tu sizani kama itakupunguzia kitu
 
images
 
Tatizo ujui nini maana ya mtu kuwa addicted pole sana ila ukipata ndugu yako kawa addicted na unga ndio utakua kwanini RAY C yupo ivi, she needs our help hata kwa maombi tu sizani kama itakupunguzia kitu
Lakini mkuu mbona huyu Dada alisharudi katika hali yake ya kawaida tena akaanza kuwashauri na wenzake akina lord eyes waache kutumia mihadarati kilichomfanya arudie tena Kitu gani?
 
M ntaanza NA maombi...kwavideo niloona tunakazi mbelekubwa kumkomboa kubwasana lakini tusikate yatamaa..wenye instagram mnaweza search globapublishers AMA obbytheng mtamwona anavyochopolewa NA poliisi usiku mawindoni
Labda akipata Mume anaweza kutulia, nadhani hiyo ndiyo njia pekee iliyobaki ya kumsaidia
 
kweli kabisa mdau wako watu wengi wanashida hapa duniani kuna wafungwa,wagonjwa,wajane na yatima
Wote hata hao waliotumbukia kwenye janga la mihadarati ni wakuomba Mola awasaidie.
 
Lakini mkuu mbona huyu Dada alisharudi katika hali yake ya kawaida tena akaanza kuwashauri na wenzake akina lord eyes waache kutumia mihadarati kilichomfanya arudie tena Kitu gani?
Unga sio kama pombe au sigara au kujichua mana ukiwa addicted na unga ni kama kuna kishetani kwa ndani ya moyo kila saa kinataka urudi kwaiyo kutibiwa ni moja ila inabidi na mazingira au style ya maisha ibadilike uwe associated na watu wa dini sana hii itasaidia ila uwezi kuacha afu marafiki wale wale, tusimuhukum bali tumsaidie
 
Back
Top Bottom